Yanayoendelea kati ya kampuni ya Dangote na serikali kuhusu mgogoro wa kiwanda cha Dangote cha kutengeneza saruji kusitisha uzalishaji wa bidhaal hiyo na kauli tata za mawaziri husika,ni ushahidi tosha kuwa mikataba kati ya serikali na wawekezaji inapaswa kuwa wazi na ni lazima ipite Bungeni kupata ridha ya Bunge.
Watanzania wenzangu, kwa mwendo huu,ni wazi tumechelewa kuwa na sheria ya aina hii na sakata hili lilipofika sasa ni dhahiri linahitaji intervention ya Bunge kuchunguza mkataba huu kupitia kamati ndogo itakayoundwa na Bunge na ambayo itapaswa kuwa na wajumbe kutoka upinzani na pia kuongozwa na mbunge kutoka upinzani.
Ni ajabua pia Raisi Magufuli anaesititiza kuwa serikali yake ni serikali ya viwanda mpaka sasa yuko kimya kuhusu sakata hil huku akituaminisha watanzania kuwa anataka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Watanzania wenzangu,wakati haya yanaendelea tunapaswa kwenda mbali zaidi na kujiuliza kama kiwanda hiki kweli kinamilikiwa na bwana Dangote kwa asilimia mia moja maana inashangaza kusikia waziri anaongelea swala la kiwanda hiki kutaka kuendelea kupewa nishati makaa ya mawe bure.
Kwa kifupi jambo hili linahitaji uchunguzi na pia waziri anapaswa kufafanua kauli yake hii na anapaswa pia kuuleza umma wa watanzania ni kwaninin siku zote wamekuwa kimya ila leo hii ndio anaamua kueleza haya na yatupasa pia kuanza kujiuliza ni nini kimetokea hapa katikati mpaka waziri anafikia hatua ya kusema kile alichokiri kutuficha watanzania na tujiulize pia alituficha kwa maslahi ya nani wakati sisi ndio wenye nchi na yeye kapewa dhamana tu ya kusimamia sekta hiyo kwa niaba yetu.
Watanzania hatupaswi kuishia hapo bali inabidi tuanze kujiuliza ni nini kilichomo katika mikataba ilyosainiwa katika awamu hii(mikataba kati ya Tanzania na mfalme wa Morocco,n.k) na mikataba mingine baina ya wawekezaji na serikali za awamu zilizopita.
Watanzania tunahitaji kujua ukweli wa haya yote na si kusubiri mpaka waziri aamue kusema ukweli bali waziri anapaswa kubanwa na sheria kuweka kila kitu wazi vinginevyo mambo haya yataendelea kujirudia kila siku.