Waziri Bashungwa: Mikataba 15 ya Ujenzi wa Barabara Yenye Thamani ya Trilioni 1.03 Kusainiwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,063
49,749
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema wakati wowote kutoka Sasa Serikali Kupitia TanRoads itasaini mikataba 15 ya Ujenzi wa Barabara na madaraja Nchi nzima tukio ambalo Litashuhudiwa na Mh.Rais Dk.Samia.

Waziri amesema thamani ya mikataba hiyo itakuwa ni zaidi ya Sh.Trilioni 1 hivyo Watanzania wakae mkao wa kula.

Hii mada ingekuwa ni kutukana Rais ingefika page ya 10 ila Kwa kuwa ni ya mambo mazuri ya Rais Samia haters wake wataishia kupita kimya kimya huku wakisonya 😂😂😂

Mungu mbariki Samia na Kazi iendelee 👇

-

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), inatarajia kusaini mikataba 15 kwa pamoja ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na daraja kwa thamani ya shilingi Trilioni 1.034 ili kuboresha huduma za miundombinu nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa wakati akitoa majibu ya nyongeza Bungeni jijini Dodoma katika kikao cha nne mkutano wa 13.

Bashungwa amesema kuwa miradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za miradi ya maendeleo na Serikali iko mbioni kuandaa tukio hilo.

“Mheshimiwa Rais ameshatoa kibali kama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyosema, na tumeona tuandae siku ambayo tutasaini mikataba hii kwa siku moja halafu baada ya hapo mimi na Naibu Waziri tutaambatana na Waheshimiwa Wabunge kwenda kuwakabidhi Makandarasi kwenye majimbo yenu”.amesema Waziri Bashungwa

Chanzo: TBC

My Take
Vishindo vya Rais Samia sio vya Nchi hii.Ikumbukwe mwaka huu mwezi wa 6 Jumla ya mikataba 7 ya ujenzi wa Barabara zaidi ya km 2,000 ilisainiwa Kwa utaratibu wa EPC+F.

View: https://youtu.be/YRk9qykVLW8?si=eIYHfJM9EzE3ilCQ
 
Mpumzisheni bi mkubwa hata hayo mambo ya kufanyika kimya kimya na yeye awepo, kazi nzuri itaonesha matokeo chanya baada ya kukamilika.
 
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema wakati wowote kutoka Sasa Serikali Kupitia TanRoads itasaini mikataba 15 ya Ujenzi wa Barabara na madaraja Nchi nzima tukio ambalo Litashuhudiwa na Mh.Rais Dk.Samia.

Waziri amesema thamani ya mikataba hiyo itakuwa ni zaidi ya Sh.Trilioni 1 hivyo Watanzania wakae mkao wa kula.

Hii mada ingekuwa ni kutukana Rais ingefika page ya 10 ila Kwa kuwa ni ya mambo mazuri ya Rais Samia haters wake wataishia kupita kimya kimya huku wakisonya

Mungu mbariki Samia na Kazi iendelee

-

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), inatarajia kusaini mikataba 15 kwa pamoja ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na daraja kwa thamani ya shilingi Trilioni 1.034 ili kuboresha huduma za miundombinu nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa wakati akitoa majibu ya nyongeza Bungeni jijini Dodoma katika kikao cha nne mkutano wa 13.

Bashungwa amesema kuwa miradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za miradi ya maendeleo na Serikali iko mbioni kuandaa tukio hilo.

“Mheshimiwa Rais ameshatoa kibali kama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyosema, na tumeona tuandae siku ambayo tutasaini mikataba hii kwa siku moja halafu baada ya hapo mimi na Naibu Waziri tutaambatana na Waheshimiwa Wabunge kwenda kuwakabidhi Makandarasi kwenye majimbo yenu”.amesema Waziri Bashungwa

Chanzo: TBC

My Take
Vishindo vya Rais Samia sio vya Nchi hii.Ikumbukwe mwaka huu mwezi wa 6 Jumla ya mikataba 7 ya ujenzi wa Barabara zaidi ya km 2,000 ilisainiwa Kwa utaratibu wa EPC+F.
Serikali ya Samia ni kama ya JK. Serikali ya laki si pesa. Hapa utasikia daraja la mil 700 ukiangalia wakati wa JPM lingejengwa kwa mil 15 au 50. Sasa ukisikia trilion usishtuke ni urefu wa kamba za watu tu huo ila utakutana na kitu cha bil 200 au 300
 
Una taarifa kamba Stand ya Magufuli inavuja?

Una taarifa kwamba zile hostel za expansion joints zimechakaa?

Una taarifa kwamba bwawa la Nyerere limeanza kuweka nyufa?

Wajinga Kama nyie ndio mnaoliwa.

Na mwisho Barabara ya Njia 8 ,km 2 zilifumuliwa na Mkandarasi akaanza Upya.
 
Back
Top Bottom