Ya Dangote ni ushahidi mwingine kuwa mikataba yote wa wawekezaji inapaswa kuridhiwa na Bunge

Kuna uwezekano pia kuwa kiwanda cha Dangote sio cha "Dangote", kwa asilimia 100%. Kwa nchi yetu siwezi kubisha sana, kuna wapigaji wengi walitumia majina ya watu kujiwekea hazina..Dah!!!
 
Maajabu haya ya kugawa maliasili bure utayapata Tanzania tu.

Tumeshakosea.Nahisi sio kwa Dangote tu,tupitie na Makampuni mengine hasa ya Madini tuone kuna nini ndani yake.
Kama tunaweza tutangaze azimio la Arusha jipya litakalohusu Mikataba.Athari zake ndio tuwe tayari kuzibeba maana dunia ya leo ni tofauti sana na ya 1967.
Tujifunze kwa Zimbabwe.
 
Mpwa wangu Salary Slip kwani kwa sasa tunasimamia tamko lipi mojawapo? Maana yamekua mengi, Kiwanda hakijafungwa kinafanya kazi, Kiwanda kimefungwa kwa ajili ya matengenezo, Kiwanda hakina nishati, Kiwanda kinunue makaa ya mawe ya ndani, kufungwa kwa kiwanda hakutaathiri upatikanaji wa Cement, Kiwanda ....
 
Mkuu, ndio maana nasema tulipofika jambo hili linahitaji uchunguzi ukweli ujulikane.
 
Bunge lipi mkuu?
Ni hili linalokatiwa kitu kidogo na kupitisha miswada?

TUONEE HURUMA BASI MKUU.
 
Back
Top Bottom