Ya Dangote ni ushahidi mwingine kuwa mikataba yote wa wawekezaji inapaswa kuridhiwa na Bunge

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Yanayoendelea kati ya kampuni ya Dangote na serikali kuhusu mgogoro wa kiwanda cha Dangote cha kutengeneza saruji kusitisha uzalishaji wa bidhaal hiyo na kauli tata za mawaziri husika,ni ushahidi tosha kuwa mikataba kati ya serikali na wawekezaji inapaswa kuwa wazi na ni lazima ipite Bungeni kupata ridha ya Bunge.

Watanzania wenzangu, kwa mwendo huu,ni wazi tumechelewa kuwa na sheria ya aina hii na sakata hili lilipofika sasa ni dhahiri linahitaji intervention ya Bunge kuchunguza mkataba huu kupitia kamati ndogo itakayoundwa na Bunge na ambayo itapaswa kuwa na wajumbe kutoka upinzani na pia kuongozwa na mbunge kutoka upinzani.

Ni ajabua pia Raisi Magufuli anaesititiza kuwa serikali yake ni serikali ya viwanda mpaka sasa yuko kimya kuhusu sakata hil huku akituaminisha watanzania kuwa anataka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Watanzania wenzangu,wakati haya yanaendelea tunapaswa kwenda mbali zaidi na kujiuliza kama kiwanda hiki kweli kinamilikiwa na bwana Dangote kwa asilimia mia moja maana inashangaza kusikia waziri anaongelea swala la kiwanda hiki kutaka kuendelea kupewa nishati makaa ya mawe bure.

Kwa kifupi jambo hili linahitaji uchunguzi na pia waziri anapaswa kufafanua kauli yake hii na anapaswa pia kuuleza umma wa watanzania ni kwaninin siku zote wamekuwa kimya ila leo hii ndio anaamua kueleza haya na yatupasa pia kuanza kujiuliza ni nini kimetokea hapa katikati mpaka waziri anafikia hatua ya kusema kile alichokiri kutuficha watanzania na tujiulize pia alituficha kwa maslahi ya nani wakati sisi ndio wenye nchi na yeye kapewa dhamana tu ya kusimamia sekta hiyo kwa niaba yetu.

Watanzania hatupaswi kuishia hapo bali inabidi tuanze kujiuliza ni nini kilichomo katika mikataba ilyosainiwa katika awamu hii(mikataba kati ya Tanzania na mfalme wa Morocco,n.k) na mikataba mingine baina ya wawekezaji na serikali za awamu zilizopita.

Watanzania tunahitaji kujua ukweli wa haya yote na si kusubiri mpaka waziri aamue kusema ukweli bali waziri anapaswa kubanwa na sheria kuweka kila kitu wazi vinginevyo mambo haya yataendelea kujirudia kila siku.
 
Ha ha ha. Kunavitu ni siri aisee. Gvt haiwezi weka kila kitu hadharani. Ndomaana ya dangote hakuna anayejua chanzo. Ukweli wanao wenyewe kwenye makaratasi yao
 
Binge la Tanzania limebaki kuokota makombo katika karamu ya mabwana waleee.
Limekuwa ni bunge la kujadili matukio mabovu baadala ya bunge la kujadili na kuidhinisha mikataba muhimu kama hii.
 
Kwa uswahili unaoendelea nachelea kusema huenda Dangote anamiliki 20% tu ya hisa.

Hicho kiwanda ni cha watanzania wanasiasa sasa ni kuonyeshana nani zaidi.
 
Na inawezekana na wanasiasa wa awamu iliyopita ila tu hatuambiwi ukweli na huenda haya ndio makaburi yenyewe.
 
Nampongeza mh.Rais kwa sababu ameamua kukaza ili ukweli ubainike watu wanavyotaka kutuibia.Wale Wa awamu iliyopita wangetoa tu hayo makaa bure na kuendelea kula maisha.Ila nashauri wakae chini wayamalize ,ila ya kutoa makaa bure hapana,bora wafunge tu.Rhino ,twiga, nyati na wengine mbona wananunua na hawalalamiki ?
 
kama wana mkataba,dangote waiburuze serikali mahakamani wakajizolee mabilioni ya fidia kama IPTL walivyovuna,tena sio mahakama uchwara za Tanzania,huko uswisi kwenye international arbitration court.
 
Maadui 3 wa maendeleo ambao ni wabaya kabisa nchi hii ni UOGA, UNAFIKI na UBINAFSI.

UBINAFSI: ndiyo umepelekea viongozi wa awamu ya 4 kusaini mkataba na Dangote kwa maslahi mafinyu ya kwao binafsi. Hawakuliweka taifa mbele.

UNAFIKI: kuna viongozi wengi tu waliokuwepo awamu ya 4 waliyajua haya na ubovu wa mkataba huu waliujua lkn wakajichekesha na kujipendekeza kwa mabosi wao. Hata hawakuthubutu kukemea wala kujiuzuru.

UOGA: watz ni waoga sana kutoa maamuzi ama kuchukua hatua pale mambo yanapokwenda kombo. Ukimya wa JPM ni ushahidi tosha juu ya hili. Jaribio waziri Mwijage kutaka kutudanganya ni ushahidi tosha juu ya hili. Na ukimya wa watz ni ushahidi mwingine. Tulipaswa Kutumia Haki Yetu Ya Kikatiba Kukemea Jambo Hili Kwa Maandamano.
 
Nampongeza mh.Rais kwa sababu ameamua kukaza ili ukweli ubainike watu wanavyotaka kutuibia.Wale Wa awamu iliyopita wangetoa tu hayo makaa bure na kuendelea kula maisha.Ila nashauri wakae chini wayamalize ,ila ya kutoa makaa bure hapana,bora wafunge tu.Rhino ,twiga, nyati na wengine mbona wananunua na hawalalamiki ?
Sio wafunge tu bali waliyowapa wanastahili adhabu.Huwezi kugawa maliasili ya Taifa bure katika mazingira yasiyoeleweka alafu ukaachwa hivi hivi tu
 
Nampongeza mh.Rais kwa sababu ameamua kukaza ili ukweli ubainike watu wanavyotaka kutuibia.Wale Wa awamu iliyopita wangetoa tu hayo makaa bure na kuendelea kula maisha.Ila nashauri wakae chini wayamalize ,ila ya kutoa makaa bure hapana,bora wafunge tu.Rhino ,twiga, nyati na wengine mbona wananunua na hawalalamiki ?

Dangote sio mjinga kudai Makaa bure wakati ameshajenga kiwanda.Huyu ni mfanyabiashara Bilionea tena wa Kimataifa na mzoefu wa Uwekezaji.Tujue kwenye Mkataba walikubaliana nini.Nahisi kuna uwezekano wa kuburuzana Mahakamani yakatokea kama ya TANESCO.
 
Maajabu haya ya kugawa maliasili bure utayapata Tanzania tu.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom