Xplasters, Nini dhambi kwa mwenye dhiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Xplasters, Nini dhambi kwa mwenye dhiki?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mwanakili90, Jan 3, 2012.

 1. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  (Faza Nelly)

  From the album 'Maasai hip
  hop' (Out Here records, 2004) Swahili lyrics (English intro): All my people
  East Africa
  Tanzania, Uganda and Kenya
  Dar es Salaam, A town
  Wherever you are
  Piga magoti, tuombe Mungu Hii ni siasa, dini, vita, ubwana,
  utwana, au kiama ghalika,
  sodoma na gomora?
  Simama imara, zunguka kila
  kona, kila anga angaza
  Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia

  Na hapo ulipojishikiza
  g'ang'ania, sikilizia, vumilia
  baadae usije jutia Hii ni mahususi na maalum
  kwa watu wangu
  Walemavu, vipofu, zeruzeru na
  wendawazimu
  Watoto wa mitaani, fukara,
  masikini na wenye akili zao timamu

  Hii kamba ngumu
  Mjue tunavutana na wenye
  nguvu
  Vitambi na mashavu
  Hakuna tena fair game Refarii kauzu
  Uwanja wenyewe mkavu
  Ujira mgumu, malipo finyu
  Kilichobaki kucheza rafu
  Tumechoshwa na ukabaila,
  ubepari na ubeberu

  Wakati ndo huu
  Ukombozi ndo huu
  Na sasa naamuru mliopo chini
  wote mpate divai ya vinibu
  Mtetezi wenu nikaze gidamu

  Nimwage sumu ya ----- juu yao
  Wajikune bila aibu
  Kwanza saluti kwa
  waliyotangulia kuzimu
  Pili tuombe Mungu
  Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku
  Utujaze nguvu
  Tupate kudumu ndani ya game
  Tutakapofika kuzimu siku ya
  hukumu
  Utupe nafasi tupate kutubu Kwani tunajua tunatenda
  maovu
  Tunakula haramu
  Tunatumia kila mbinu
  Juju, uhalifu, upanganyifu
  Ili tuweze kujikimu Lakini isiwe kisingizio kwa
  wanadamu wengine
  kunyimwa haki zetu
  Kutuzibia riziki zetu
  Kutuita makafiri, dharau na
  kutukashifu Kwani nini dhambi

  Chorus :
  Nini dhambi kwa mwenye
  dhiki,
  Kipi haram, kipi halali,
  Kila mmoja anaitaka hii riziki
  Kitendawili, vurugu mechi Huwezi tabiri Kwa nini ?

  Uliza swali, kama
  sote tungekuwa wasomi,
  matajiri
  Ni nani angelifanya kazi za
  kutisha na hatari mfano ya
  mochwari Kila mmoja wetu hapa mjini
  kaja kwa dili
  Kila kitu, kila mahali
  Na hata ngozi ya mtu dili
  Wengine wachawi, waganga
  feki Matapeli, wasafiri ------
  Wakati wengine wapole kama
  walokole

  Mchana pirika nyingi maofisini
  Kumbe night kali, kahaba
  Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri
  Ah!
  Wapo waliopoteza maisha
  katika kufight life
  Kumbukumbu zao zimebaki
  makaburini Na wapo waliopoteza kabisa
  tumaini la kuwini
  Hao roho zao utadhani
  wamezitoa rehani
  Wakikutight mahali fulani
  Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi

  (Chorus)

  Kweli Bongo kutafuta braza
  Utajajuta utakapojikuta huna
  hata bukta
  Shauri yako we tegesha tu
  kama golikipa
  Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa
  Huna elimu, hun fani
  Lakini nguvu, hulimi, uchumi
  unao unaukalia
  Kumbuka
  Kupata au kukosa yote ni kawaida
  Sometimes unalala unaota
  unakula
  Unakunywa, unapiga denda
  Na kula uroda na demu bomba
  Ukikurupuka tu unakuta patupu
  Hakuna kitu

  (Chorus, Yamat singing a
  traditional Maasai song)
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu,hawa jamaa nimebahatika kuwa nao karibu kipindi bado nipo Arusha! Faza Nelly alikuwa anaaminika ndio the best Hiphop Artist ever in Arusha! Binafsi mpaka kesho naamini hivyo na ndio alikuwa kichwa wa kundi! Mafanikio ya kundi lao hayajawahi kuvunjwa rekodi na kundi lolote Tanzania hii! Ndio wasanii wa kwanza wa Hiphop video yao kurusha Channel O! At that time our video quality was extremly poor lakini hawa jamaa walikuwa level nyingine! Walikuwa wanaitwa kupiga shows Senegal,SA,USA,Holland etc while hapa Bongo walikuwa hawaitwi sababu wanyonyaji walikuwa hawawezi kuwalipa wanavyotaka! Hawa jamaa walikuwa wanakutana na kuheshimiwa na Ma legend kibao wa Mbele! Na amini usiamini hawa ndio waliofanya huko duniani kujua Tanzania kuna Hiphop! Jamaa style yao ilikuwa ni hiphop masai na walifunika sana tu ila tatizo Faza Nelly ndio alikuwa mtunzi na mbunifu sana ndio maana kama alikufa na kundi.Muulize mwanahiphop yeyote wa Arusha kuhusu Faza Nelly uambiwe! Msiba wake ni moja ya misiba iliyopata mahudhurio makubwa mno Arusha.RIP FAZA NELLY!
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  I miss Faza Nelly!
  Wimbo wa nini dhambi kwa mwenye dhiki hadi kesho huwa nausikiliza na kutafakari falsafa iliyo ndani yake
  RIP bro!
   
 4. Rayz of Diamond

  Rayz of Diamond Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R. I. P Father Nelly kwa kwel huyu jamaa na Kundi lao la Xplastaz ni icon nzur sana kwa Hip Hop ya Bongo nawakumbuka sana na Hip Hop Masaai yao....Wimbo kama USHANTA, HAAAA HAAAAA na kadhalika kadhalika..naona sasa hivi kuna Madogo wanaliendeleza vizur kundi..
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,618
  Trophy Points: 280
  naomba mwenye kujua jina la albam yao ya kwanza. nimeshindwa nipateje nyimbo zao hawa jamaa. Msaada jamani. Mia
   
 6. Rayz of Diamond

  Rayz of Diamond Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kwel hata mie sikumbuk Albam yao ila nakumbuka baadhi ya nyimbo zao za wakati ule Miaka ya 90 kama vle USHANTA, HAAA, MSIMU KWA MSIMU, NINI DHAMBI KWA MWENYE DHIKI na BAMIZA...
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nilikuwa nakisaka kinasa,sasa nimekipata,raffu....raffu nelly ...na mneli....
  wakuu hawa ndio artists wa ukweli tanzania.
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  USHANTA! Umenikumbusha mbali sana mkuu! Wakati Arusha ikiwa Arusha kweli na machizi wa Mbuguni!
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  Ayaaa! Umeua chali angu! Dah!
   
 10. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kuna rapa kutoka Xplastaz ivi karibuni alipafomu kwenye tuzo za BET ile sehemu ya freestyle battle,simpati jina..huwezi amini hawa jamaa wanafahamika nje zaidi ya bongo.
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  bongo(hasa dar) wanapenda porojo sana.ile freestyle alikuwepo KRS ONE!
   
 12. Rayz of Diamond

  Rayz of Diamond Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli Matumbo hata Me nliiona hyo kwenye zle segments za BET freestyles, kama nakumbuka vzur atakuwa anaitwa GSAN..
   
 13. Rayz of Diamond

  Rayz of Diamond Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taften Wimbo mpya wa XPlastaz unaitwa AFRICA wamemshirikisha Fid Q na Mshikaji mwingine cjui wa Marekani yule, hauna cku nying sana nadhan umetoka Mwez wa 9 au 10, 2011..
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  Dar imefanywa ipende kile wanyonyaji wanapenda! Hawataki watu wenye misimamo mikali ili wawatumie! Fikiria mtu kama Dogo Hashim anapotea!
   
 15. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Ukweli huu wimbo kwangu mimi ndio bora kwa Hip Hop ya Tanzania,siwapendi sana Xplastaz but hii track ndio bora kwangu hata Video yake iliendana na mazingira ya Tanzania
  R.I.P Nelly
   
 16. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  safi hiyo ..nawakubali sana jamaa
   
 17. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280


  Rest In Peace Faza Nelly.

  Hawa jamaa ndio wa kwanza (na ninafikiri haijawahi tokea mwingne) kuwa kwenye album collection na wana hip hop wa marekani kama kina 50 Cents. Nazungumzia collections za west huko.
   
 18. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kuna rapa kutoka Xplastaz ivi karibuni alipafomu kwenye tuzo za BET ile sehemu ya freestyle battle,simpati jina..huwezi amini hawa jamaa wanafahamika nje zaidi ya bongo.


  anaitwa G SAN alifanya cypher na kina KRS 1
   
 19. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Rest in peach faza nelly. Ulikuwa MC wa ukweli
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,522
  Likes Received: 5,668
  Trophy Points: 280
  kwa ambao hawakufanikiwa kuwaona Xplasters wakiperform live wakiwa wamekamilika na Faza Nelly nawasikitikia kwa kukosa burudani ambayo usingeamini kama jamaa ni wabongo!
   
Loading...