Xenophobia: Wanaigeria wavamia Shoprite kulipiza kisasi

Wanasema 80 percent ya mji Ni wageni ok tuseme Yuko sahihi je walitakiwa was attack wageni au was attack serikali yao? Sioni mantiki ya kuwa attack wageni.Huyu kiongozi hayuko sahihi.Pili Kuna miji hata Tanzania wenyeji hawaakai mijini hupenda kukaa vijijini Miji unakuta asilimia kubwa Ni wageni Sio wenyeji mfano Dar es salaam,zaidi ya 80 percent Ni wageni Sio wazaramo wenyeji.Kosa Sio wageni.South Afrika pia wenyeji wengi hukaa vijijini Sio mjini.Tatu miji mingi huanzishwa na wageni mfano Tanzania miji mingi ilianzishwa na wafanyabiashara wageni mfano dar es salaam wageni ndio walioanzisha kariakoo wamanyema wa Kongo,wahindi,wapemba na waarabu maeneo mengine walioanzisha watu wa morogoro kama kigogo na mburahati,kimara wachaga na singida,mbagala wamakua ,wamakonde na wamwera na warufiji ,gongo la mboto watu wa mkoa wa Mara ,kigoma nk anachoongea sikubaliani nacho.Wageni hawana kosa Kama Kuna shida wamalizane za serikali yao.Hao wameenda kufanya biashara sababu wenyeji SI wapenda kufanya biashara.Hiyo sababu SI sahihi
Wageni anaowazungumzia yeye siyo raia wa SA, bali ni raia wa nchi nyingine. Kwa hiyo usilinganishe na Kimara kuendelezwa wachaga wa Kilimanjaro ambayo ni sehemu ya Tanzania.

Ukimsikiliza vizuri unaona wanayo sababu ya kupambana na wahamiaji kutoka nchi jirani na zisizo jirani, tatizo njia wanayotumia kupambana na wimbi la wahamiaji haramu ndiyo mbaya.

Naamini kwa hali aliyoieleza huyo waziri, taifa lolote lililomakini na mustakabali wake na usalama wake lingechukua hatua kali kukabiliana na tatizo lakini kwa kutumia njia sahihi.
 
Kulipa kisasi au ni wizi tu..., watu wanafanya wizi wao kwa kisingizio cha visasi..., hio supermarket haina mchango wowote wa nchi yao ? au ndio kuchoma nyumba ili kufukuza viroboto...
 
Ukimsikiliza vizuri unaona wanayo sababu ya kupambana na wahamiaji kutoka nchi jirani na zisizo jirani, tatizo njia wanayotumia kupambana na wimbi la wahamiaji haramu ndiyo mbaya.
Hiyo ninkazi ya uhamiaji Sio yao wanajuaje kuwa Ni wahamiaji haramu wakati wao Sio uhamiaji?
 
Afrika kusini Huwezi sikia wazungu wakipiga waafrika weusi wa nchi zingine Ni waafrika wenzetu ndio wanatubagua.Kwa Mara ya kwanza niwaombe msamaha wazungu wa Afrika kusini kuwa tuliwaonea kuwaita wabaguzi kuwapiga mabomu na risasi kumbe wabaguzi Ni waafrika weusi Sio wazungu.Niwaombe Wanigeria waache kushambulia Mali za wazungu wa Afrika kusini zilizomo nchini mwao.Na niwaombe waafrika weusi popote wasiwashambulie wazungu Wala biashara zao
we hujitambui wala hujui unachokiandika! mastermind wa hiyo xhenophobia ni hao wazungu sasa ngoja nikuambie!
 
Naona wanaija wanakemea mapepo.hao wa xhosa wao ni alcohol na anasa kibao wageni wana take over wanawapiga.wawaache watu wapige mishe wao waendelee na uzandu.S.A sijaona Rais wakulimaliza hili wote ni failure ata mandela alichukua nchi sababu ya kuvumilia jela.Bado wana hangover za vita ya Soweto.




Wapunguze uvivu
 
Hajui diplomasia. Hajui hata cha kufanya. Mmempa majukumu makubwa kuliko akili yake
Kile cheo ni cha kupokezana kijiti ila ukweli ilipaswa ili mtu awe mwenyekiti wa SADC nchi yake iwe na utulivu wa kutosha wala haina historia ya uvunjifu wa amani.

Lakini sisi na Afrika yetu tunaona sawa tu hata kama umeng'ang'ania madaraka, nchi yako haina amani ya kudumu, demokrasia mbovu,hakuna freedom of speech zamu yako ikifika unapewa Uenyekiti wa SADC
 
Back
Top Bottom