Xbox one mpinzani wa playstation 4

Xbox one mpinzani wa playstation 4

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,060
Reaction score
43,477
kama wewe ni mpenzi wa video games utakua unajua tayari sony wamezindua playstation 4 na microsoft nao wamezindua xbox one. xbox one sio game tu limezinduliwa na mambo mengi kama tv box, kinetic sensor mpya na games mpya za EA sport.hebu tuliangalie hili game jipya la microsoft lina nini cha muhimu?

HARDWARE

Tofauti na sony ambaye ameeka specification za playstation four kama siri wao Microsoft wameanika wazi specification za xbox one. Game hili litakua na chip za amd nanometer 40 zenye 8 core cpu, ram ni 8gb na hard drive yake ni 500gb. Ina usb port 3.0 na wifi yake ni 802.11. game console hili lina uwezo wa kuplay cd za bluray.

052413_1028_Xboxonempin1.png
Xbox one sio game tu bali ni top-box lina vitu kama hdmi na tv-box

watanzania tunapenda sana kitu kimoja kinachofanya mambo mengi (multipurpose). Na hili game nalo linafanya mambo mengi tofauti na kuwa game console tu. Ukiwa na xbox one utapata hdmi port (waya wa kupitishia multimedia kutoka kwenye game hadi kwenye tv) ambayo itakuwezesha kuunganisha vitu vyako kama ving’amuzi, receiver za satellite dish, dvd, home theatre vyote hivi. Hii inamaana xbox inaweza kuwa kama kipitishio cha vifaa vyako kwenda kwenye tv.
Haiishi hapo ukiwa na xbox utaweza kuliambia game kitu unachotaka kufanya kwa kutumia sauti. Mfano unaweza liambia open FIFA 2014 game then hapo hapo litafungua hilo game.

SOFTWARE

Xbox inakuja na muonekano kama wa windows 8 na inavitu vingi ambavyo sio vya gamers. Xbox inakuja na apps kama internet explorer na skype .
052413_1028_Xboxonempin2.jpg
Muonekano wa xbox ni kama ule wa windows 8

Hili game linasuport multitasking, uwezo wa kurun application zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ukiwa na xbox unaweza kugawanya kioo na ukafanya mambo mawili. Mfano upo nyumbani munatumia tv moja unaweza gawanya nusu tv ikawa upande unaonesha game na upande unaonesha tv.
GAMES

Xbox imezinduliwa na magame mengi sana yakiwemo FIFA 2014, NBA live 2014, EA sport UFC, call of duty; ghosts na mengineyo. Wamesema jumla kutakua na magame kama 15 yatakayotoka na xbox one.
052413_1028_Xboxonempin3.jpg
ARE YOU READY? Messi, Ronaldo, ibracadabra, hazard, vanpersie, falcao

Kuna tetesi kua game zitachezwa online tu na wengine wanasema zitakua online na offline kwa bahati mbaya Microsoft mpaka sasa hajasema habari ipi ni ya kweli.
GAME PAD

Pad ya xbox one itakua ndogo kidogo kuliko ya xbox ya kawaida na pia itakua na rangi nyeusi completely.
052413_1028_Xboxonempin4.jpg
Pad ya xbox one ikiwa na muonekano mpya

Pad hii itakua na vibration nne ambazo zitakua zinavibrate tofauti tofauti kutokana na matukio. Mfano kama ni game la gari kuna vibration ya speed kubwa, vibration ya kugonga mwenzako, vibration ya kuwasha gari nakadhalika.
SENSOR MPYA YA KINETIC

Kinetic ni feature ya Microsoft inayofanya mambo mengi kwenye hili game. Hii sensor ndio ambayo inakusikiliza wewe muda wote. Ukisema open tv hii inaskiliza na kuopen tv. Na inafanya kazi hadi maeneo yenye kelele nyingi.
052413_1028_Xboxonempin5.jpg
Kinetic mpya inayoreceive voice na camera ya mbele

Hii kinetic sensor pia ina camera ya mbele kwa ajili ya skype na camera hio inasuport full hd 1080p na kizuri zaidi sababu game inakua mbali ina maana ukiongea skype huonekani wewe tu bali na mazingira ya karibu na wewe kama makochi, zulia, meza na madirisha.

Bei ya hii console ni dola 400 around laki 7 kwa Tanzania.
 
Duh nice,naamini hata ambao walikuwa hawapendi magem nao kidogo watakuwa wamevutika.
 
Mkuu chief-mkwawa yaani ungejua tu kuwa people are not even excited in Xbox One hata usingesema. Embu fuatilia huu mjadala HAPA.

mkuu mimi si mpenzi wa x-box na wala ninapotoka hazipatikan sana watu wengi tunacheza ps.

ila hawa jamaa xbox wanajua kuvutia watu na gamers. xbox la 2005 hadi january mwaka huu lilikua ndo linauza sana kushinda hata game console za 2012.

hili limekaa kifamilia zaidi litazidi kuuza sana
 
Xbox 360 maybe...but Xbox One haijawavutia sana gamers. Sijui jamaa wameharibu wapi.
 
Xbox 360 maybe...but Xbox One haijawavutia sana gamers. Sijui jamaa wameharibu wapi.

ngoja nikuambie wameharibu wap. wanataka kufanya a gaming console iwe a multimedia hub. sony walivyotoa PS3, walianza kuuza kwa strategy ya blu-ray ila wakagundua kuwa gamers are not excited with all that pizzash. mimi kama gamer, am not interested in having an IE in my console, au media player or all the many other funny add-ons they push into the consoles. PC's and dvd players are downright cheap, I want a console that just games
 
Na vipi kuhusu swala la graphics and Processor specs? maana according to the above conversation wengi wanasema PS3 is better than Xbox One.
 
Na vipi kuhusu swala la graphics and Processor specs? maana according to the above conversation wengi wanasema PS3 is better than Xbox One.

watu wengi wanasema kuwa ps4 ni better coz like me hawajafurahia changes zilizowekwa kwa xbox. kuhusu swala la gpu na cpu, not much is known ila tu kwamba wote watatumia 8-core amd processors na video card za ati both za 8gb. xbox za kwao zitautimia ram ya DDR3 na sony watatumia GDDR5.

the difference..
DDR3 ni RAM type ya PC latest na GDDR5 ni RAM type ya video cards. kwa hesabu za haraka haraka you would expect the GDDR5 ishinde maana tunaongelea gaming , however cpu ndo huwa inawesha kuendesha na ku unleash potential ya video card na since both video cards ni integrated, the processors will determine everything. wakitoa proper specs tutaweza kujua which is better ila kwa sasa, speculation na fan boyism :rolleyez:
 
Yaani kwa lolote vile kama Pro Gamer hata walete ps20 na xbox20 yani PC ndo mwisho wa matatizo always!
 
Yaani kwa lolote vile kama Pro Gamer hata walete ps20 na xbox20 yani PC ndo mwisho wa matatizo always!

mkuu ujue tatizo sio pc tatizo hizi console zimekosa ubunifu kuanzia ps 1 hadi ps4 same way unafungua mlango wa cd unaeka cd unachukua pad unacheza. wakati vitu hivyo unafanya kwenye pc pia.

wanahitaji vitu vipya kama concept ile ya ilumiroom crazy things zitakazokufanya upagawe
 
Dah hyo conclusion yako balaa!!!

Thing is whatever you can do on a console I can do it on my PC plus naweza kucheza zile exclusive games za console on a pc using an emulator vile vile console games are freakin expensive geeez! Haya when new hardware comes along wale wa console you have to buy a new one example from ps2 to ps3 haya mimi the PC guy what do I do..simple I just upgrape my graphics card or ram anything that needs upgrade Thats y The PC will ultimately come on top
 
Now u r toking ile conclusion yako ya mwanzo ilikuwa iko limited ktk details
 
Back
Top Bottom