X wangu anataka nikutane nae! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

X wangu anataka nikutane nae!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by silaha, Jun 25, 2012.

 1. silaha

  silaha Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi naombeni ushauri wenu,uyu dada niliwah kumchumbia,nikamsomesha toka form four mpaka mwaka jana kamaliza degree yake ya education pale SAUT,akantosa miezi sita kabla hajamaliza chuo kwa kunipa live kuwa alikuwa hanipendi miaka yote ile bali alikuwa anataka kusoma tu amalize,sasa juzi kanipigia sim kwa no mpya nisiyoijua,akaniomba nikutane nae na tena anataka kuja nyumbani kwangu baada ya kujua bado sijaoa,na alivyonimwaga alinikashifu vibaya na sina hata ham ya kumuona walau kwa bahati mbaya,na ye ndo anang'ang'ania kuja kwangu,nifanyeje?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa si umuone tu ujue kwanza nini anataka?
  why guessing?
   
 3. k

  kisukari JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  watu wengine ndivyo walivyo,huwabwaga wenzao kwa vishindo vingi,maybe hutegemea huko kunapowazuzua ndio kila kitu,baadae yanawashinda.ni vizuri kuachana kistaarabu,
   
 4. N

  Neylu JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Usikate wito, kataa maneno.. Nenda tuu usiogope..
   
 5. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,285
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kumuua nyani usimtizame machoni.
   
 6. GITWA

  GITWA JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Kubali kuonana nae,msikilize lakini ubaki na msimamo wako kuwa humpendi tena na umwambie hivyo kama nia yake ni kurudisha mausiano,waweza kuta anataka kukufidia gharama zako za kumsomesha.
   
 7. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Huyo anataka kurudi,aliyekuwa anamzuzua kaingia mitini baada ya kumchakaza,SAUT kwanza imejaa malaya.Pia akuna huakika kuwa mkirudiana atakuwa mtulivu kwako,ujui pia at this time kiafya yupoje,kwenye mapenzi akuna huruma wewe chapa lapa achana nae,japo ulikuwa unampenda lakini ataweza kukuhumiza tena huko mbeleni,inaonekana yupo after money so akipata kazi na bosi akamtokea ajakumwaga tena? Huu ni ushauri tu wewe achana nae look for some one you can trust and love.achana na hicho kimeo
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hapo pekundu na hasa kwenye mstari ni jibu tosha kwamba unapaswa wewe mwenyewe uzingatie hayo.
  1. alikuambia yeye shida yake kwako ilikuwa ni mali yako na hakuwahi na wala hakupendi.
  2. Alikukashfu sana.

  Mimi binafsi, ni kwamba katika yote fanya lkn suala la kunikashfu ni fedheha sana. Hivyo, nakupa pole sana kwa yaliyokukukuta. Ulijinyima kwa kiasi kidogo ulichokuwa nacho badala ya kuwasaidia ndugu zako au kufanya mambo ya maendeleo, lkn kwasababu ulisikumwa na upendo kwa huyo dada ulijinyima kwa vyote ili afanikiwe kufikia malengo yake. Si ajabu hata wewe labda hayo mafanikio ya elimu haukujaliwa kama ulivyomfanikisha (samahani kama nitakuwa nimekukwaza hapa, lkn ni hasira ya kutokana na alivyokutenda huyo dada). Lkn katika yote mwishowe ulikuja kuambulia Fedhea na si ajabu hata matusi ya nguoni.


  Ndugu yangu, mimi nakuambia jibu moja tu kwamba huyo dada HAKUWAHI KUKUPENDA NA HATATOKEA KUKUPENDA, lkn sasa mambo yake hayajanyooka na anakumbuka ulivyojitoa kile kipindi anasoma, hivyo anaamini kwamba utampokea tu.Hivyo mimi nakupa ushauri ufuatao,
  1. Kamwe usionane naye, kwani hakuwahi kukuhitaji na kama anakuhitaji sasa ni kwasababu kakwama au katoswa na sasa kwako ndiyo pakumalizia stress na matatizo yake.
  2. Na kama utaamua kuonana naye, jitahidi sana isiwe kwako unapohishi.
  3. Kuwa na tahadharii zaidi, kwani si ajabu ana matatizo hata ya kiafya anataka akugawie. Hili likitokea itakuumiza zaidi, kwani itakutonesha kidonda ambacho kilishaanza kupona.
  4. Kuwa na msimamo kama mwanaume na usikubali kurudi nyuma,kwani kuna hatari mabo yake yakishamnyokea ATAKUMWAGA TENA:
   
 9. The last don

  The last don JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Mkuu woga wa nini au ujiamini?...Nenda kamsikilize tu huna haja ya kukataa wito au bado kapande ka moyo wake kapo kwako hivyo unahofia kujikuta unarudisha majeshi?.....hata hivyo kusamehe na kurudia pia sio dhambi mkuu kama bado yupo moyoni na yeye kaisha jifunza,muwekee terms na condition zako mapema,then baby comeback kama kawa kwa uangalifu wa hali ya juu,faida ni kwamba kama case ni hiyo,this time you have the cards on your hand.
   
 10. S

  SANING'O LOSHILU Senior Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we mteme ujue aliekuwa anamdanganya akakuacha nae kamtema so anatafuta pa kupumulia
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ungekuwa hutaki kama unavyodai hapa wala unsingekuja omba ushauri hapa maana amuzi liko so 'naked'
   
 12. by default

  by default JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kubali appointment yake mpeleke kwenye restaurant ya gharama ya kawaida then ukifika mwambie awe huru kutumia chochote atakacho wewe tumia maji yanatosha then ukikaa nae kidogo fanya mchakato mtoroke bill iwe juu yake.usimuonee huruma mkuu mi nilishamfanyia m1 hadi leo akiniona heshima depe wanapenda kula vya bure,then tafuta msichana mwingne mkali zaidi yake .dawa ya mwanamke ni mwanamke mwanzake
   
 13. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Case of the ex....how u gonna act, how u gonna handle that...what u gonna do if she wants u back...
   
 14. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kaka kamsikilize huwezi jua labda anataka mrudiane tena ili umsomeshe masters alafu akutose tena
   
 15. s

  sumni7 Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  dah!pole kwa ilo,wengi 2nashauri 2 lakini ww ndo wamjua vizuri uyo eksi wako mtreat according to the way unavyomfaha ofkoz wawezaona ilitereza,ilibweteka,hakufiria kesho ama shetani alimpitia na ss amejifunza.ila ningekuwa mm nicingependa hata kumuona wala kuongea naye kabisaaaaa!mtazamo tuu.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280

  Msikilize labda anataka kutubu makosa yake....anataka kuja kwako ili kufanya assessment nyumbani kwako kama umekolea au la kabla ya kuamua kurudisha majeshi kwako kwa mashambulizi ya nguvu.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hili ndio jibu. Thread closed!
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Maisha siku yamekuwa kama Tamthilia tu hata ya kuwashauri sasa tunaona watu, kama alivyosema Kongosho majibu ya maswali ya mambo kama haya tayari yeye mwenyewe anayo.

  Kwa watu tuliokubuhu kama sisi ambao tumeweza kumudu kumtafuna Mama mtu na mtoto wake hivi ni sawa na vikesi vya kumchungulia mtu chooni.

  Bwashee hivi kujitwika jukumu la Baba Mzazi na bodi ya Mikopo toka o level mpaka Degree level? aisee kama kuna motoni kweli basi huyu demu ni lazima aende motoni, huu ni zaidi ya ukatili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Do not meet with her. Full stop.
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu angekuwa mkeo ningekwambia u rithink but never ever think twice kwa ishu ya gelfrend kama hii. Wanawake ni species za tofauti sana mkuu tena ni katili kuliko simba lakin ni mtamu kuliko asali.

  Asije akakuhadaa kwa maneno matamu, nafikiri kama kuna mahali usipotakiwa kukosea ni hapa unayo only one chance of making selection so it has to be the the correct and perfect selection. ambayo you wont regret in your life.

  sikatai yawezekana kabadilika but kumbuka uaminifu wa mtu hukaa moyoni mwake wala siyo usoni au mdomoni na kwa kuwa moyo hausomeki do not risk it anymore.Kama Mungu kapanga awe ni ubavu wako kweli atamleta kwa njia yake mwenyewe but naamnin Mungu anao watu wengi sana na ukileta mchezo kwake hashughuluki na wewe kwani kwake wengine wakipanda mlima wengine wanashuka.
   
Loading...