Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Selous inatajwa kuwa huenda ikapoteza tembo waliosalia ndani ya miaka sita ijayo iwapo hali ya ujangili itaendelea kwa kiwango kilichopo sasa.
Ripoti ya Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori na mazingira duniani(WWF) imesema Hifadhi ya Selous imepoteza asilimia 90 ya tembo wake, ambapo miaka 40 iliyopita kulikuwa na maelfu ya tembo.
Mahitaji makubwa ya Pembe za Ndovu katika nchi ya China,k wa mjibu wa ripoti hiyo inatajwa kuwa ni hali inayochochea ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo.
Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika utawala wake ametangaza kukomesha rushwa ambayo ndiyo imekuwa ikichangia kukua kwa vitendo vya ujangili.
"hifadhi hiyo ya Selous ni moja kati ya urithi wa dunia kufuatia kuwa na eneo kubwa la wanyama pori lililosalia Barani Afrika.
Chanzo: BBC Swahili