Wrong no ananichanganya

Wrong no ananichanganya

twende kazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
1,520
Reaction score
461
Yaan kuna binti kakosea namba katuma msg kwangu,nikamwambia soory ni wrong number but akasema please pamoja na hayo let keep in touch nikamjibu okeey haina shida.Baada ya hapo ni mfululizo wa msg na calls mpaka nazima simu muda mwingine.Binti anasema ananipenda sana na nisipomuita mpenzi ananipigia simu analia kabisa,ana wivu sana juu yangu.Nimemwambia siwezi hata kuflirt na wewe, hataki kabisa kunielewa kifupi najuta kumfahamu.Ananitumia msgs utadhani tunajuana na tulishawahi kuwa wachumba mbaya zaidi anataka mpaka kuja ninapoishi(mikoa tofauti).Yaani naona kama ngekewa nimemuomba anitumie picha amesema simu yake ya torch na hajajiunga na mtandao wowote wa kijamii.Wakati mwingine mpaka namuuliza wewe ni jini ama.Haya yote ndani ya siku 3 tu.Nimfanyeje jamani?
 
Weka namba yake hapa jukwaani wataalam wa ICT tukupe jina na picha yake....usitume PM weka hapa...
Maana kuna mahali nimeona kama umeonesha interest hivi ya kumjua...
 
weka namba yake hapa
vidume vya jf vikuondolee usumbufu
 
Ahahahahah..wakuu wabaya nyinyi.Nikiiweka nahofia kumpotezea haki yake ya msingi kuwasiliana na watu anaowahitaji.
 
ni-PM namba yake nikusaidie. hizi bahati mbona haziji kwetu :confused2: :confused2:
 
Hapa ndio ukidhani umepata kumbe umepatikana comes to mind....

Usishangae ukianza kuhudumia soon au akija akikwambia huende kwake au mkutane ukafumaniwa au kuvamiwa na kuibiwa kila kitu in short mwisho wa hii kitu 80% itakuwa ni maumivu kwako... just use good old fashion moves za kudate people you know
 
Ahahahahah..wakuu wabaya nyinyi.Nikiiweka nahofia kumpotezea haki yake ya msingi kuwasiliana na watu anaowahitaji.

Weka namba kaka...au umeanza kulainishwa na maneno yake kama ndizi mbivu tengani
 
Sa lazima uje upige kelele hapa kama unapendwa, wanaume wengine noma kweli :biggrin1:

We badala kumalizana naye kimya kimya, umeona uje ujisifu hapa.

FYI kuna wengi tu wanakutana na hayo, sijawaona wamekuja kupiga kelele JF.
 
Baadae atakuomba airtime na mshiko mwemdelee kuwasiliana kwa manufaa yake
 
Hapa ndio ukidhani umepata kumbe umepatikana comes to mind....

Usishangae ukianza kuhudumia soon au akija akikwambia huende kwake au mkutane ukafumaniwa au kuvamiwa na kuibiwa kila kitu in short mwisho wa hii kitu 80% itakuwa ni maumivu kwako... just use good old fashion moves za kudate people you know
mkuu umewaza kama mimi.ahs sana
 
Weka namba kaka...au umeanza kulainishwa na maneno yake kama ndizi mbivu tengani
ahahahahah..mkuu mtoto anabembeleza hatareee,siwezi kutoa namba yasijewakuta mabaya nami nikaingia kwenye mtego.Nipeni mbinu za kujinasua.
 
ahahahahah..mkuu mtoto anabembeleza hatareee,siwezi kutoa namba yasijewakuta mabaya nami nikaingia kwenye mtego.Nipeni mbinu za kujinasua.

mhhhhhh msaada wahitajika kweli hapa mbona yaonesha umenogewa
 
kipofu kaona mwezi

wakati wengine tunaona nuksi na kuwa wakali kwa simu za wrong number, wengine wanaona ngekewa.

Dunia haiishi vioja

Sa lazima uje upige kelele hapa kama unapendwa, wanaume wengine noma kweli :biggrin1:

We badala kumalizana naye kimya kimya, umeona uje ujisifu hapa.

FYI kuna wengi tu wanakutana na hayo, sijawaona wamekuja kupiga kelele JF.
 
Yaani hakujui/Hamjuani alafu ndani ya siku tatu mmeshapanga hadi aje mkoa wako, ndani ya siku tatu hadi analia machozi kwa wivu? Anakusumbua hadi unazima simu? Na unadai umeshamkataza? Hivi vyote ni ndani ya siku tatu tu?

Aaaah Baba Twende kazi hapo umezidi aisee, turudishie chenji aisee
 
Natamani kusema sijui ndo wewe,ila unaonekana una heshima sana hasa ukizingatia ukongwe wako JF.Kweli mkuu inawezekana kumpenda mtu usiyemuona hata sura?Tena kwa mawivu tele na mbwembwe kibao?Inakuingia akilini kweli?Mtoto wa kike anajiachia vibaya mno na anataka nimgegede anytime nitakapohitaji.Kama sio utapeli ni nini?Sina sababu yoyote ya kujisifia ujinga kwa mtu ambaye hata sura yake siijui.Nimelileta Jf kwa ushauri zaidi kabla sijakutana na hatari mbele yangu.
 
Yaani hakujui/Hamjuani alafu ndani ya siku tatu mmeshapanga hadi aje mkoa wako, ndani ya siku tatu hadi analia machozi kwa wivu? Anakusumbua hadi unazima simu? Na unadai umeshamkataza? Hivi vyote ni ndani ya siku tatu tu?

Aaaah Baba Twende kazi hapo umezidi aisee, turudishie chenji aisee
mkuu hata mimi nimeshangaa sana seriously haya yametokea..ni maajabu lakini ni kweli.Yaani sijui nitumie intelijensia gani nimkamate huyu binti pengine kuna mchezo mchafu unataka kuchezeka.
 
Anaweza akawa ni mtu anaekufahamu vizuri,she is just playing with ur mind
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom