kama ni fake kamuulize Bryan Michael kilichomvunja shingo alipo kutana na kane
Kila unachokiona pale ulingoni au nje ya ulingo kimepangwa
Kuna wataalamu wa kuandika script labda ya wiki mzima nk
Kilichotokea kwa Bryn ni kwamba alikua katika ya script na baba yake mzazi akafariki
Sasa ili kumtoa akazike ikapandikizwa script ya kane kuja kumvamia jukwaani na kumvunja shingo then baada ya wiki akarudi tena
Watu walipost hadi picha za kwenye mazishi ya baba yake yupo fit hana hata muogo shingoni
Jiulize inaruhusiwa kumvamia tu mtu jukwaani na kumpa kipondo kile cha zaidi ya dk 5 na hakuna security kuingilia?
Iliwahi kutokea eti Randy alikwenda nyumbani kwa baba yake Cena na kumpiga, nani aliwapiga picha za video na zipo very professional?
Kurukiana na kupigana na vitu mbalimbali ni mipango imepangwa, kila step jukwaani imefanyiwa mazoezi ya kutosha kabla ya kuingia ulingoni, na inapotokea ukikosea step ndio madhara uanatokea sasa
Hebu jiulize kamera zipo live zinaonyesha ze shield wanapanga nje ya jukwaa then mmoja wao anaonekana anenda kupanga deal na akina triple h awasaliti wenzake, kwaakili zako unaamini kunakamera zinachukua kila kitu huko backstage? Na kama ndio inakuaje yale matukio wanayotaka yafanyike uilingoni ndio yaonyeshwe yakipangwa back stage tena live?
Watu wanaupenda mchezo ule kwasababu ya jinsi jamaa wanavyoigiza kwa ufundi pale jukwaani na si kwasababu ni kweli
Ni sawa na wewe kuwa addicted na series ya Game of throne lakini ukajua ni uigizaji tu
Tofauti hii inafanyika live ulingoni na nyingine inafanyiwa mambo mengi kabla ya kurushwa
Nashaanga sana mtu na akili zako timamu unaamini huu mchezo ni kweli
Eti unakatazwa kupigwa ngumi lakini nyundo, viti, marungu nk ruksa, vile vyote ama si halisi na kama ni halisi basi wamefanya mazoezi namna ya kupigana kimtindo wasiumizane