wote wamechoka

JOE58

Member
Jan 27, 2012
14
5
kiongozi wa nchi moja, alitembelea uingereza. katika maongezi na malkia alimuuliza siri ya mafanikio ya nchi yake. Naye malkia akamwambia kuwa hupima busara za wasaidizi wake, kabla ya kuwateua au kuwaapisha,kwa kuwauliza maswali madogo lakini ya mtego, ili kutoa mfano hai malkia akamwita waziri wake mkuu mbele ya mgeni wake huyo, akamuuliza swali lifuatalo. "Wazazi wako wana mtoto,mtoto huyu sio dada yako wala kaka yako,je mtoto huyu ni nani?" Bila wasiwasi waziri mkuu akajibu."Mtoto huyu lazima ni mimi". Malkia akafurahi akamwambia mgeni wake " hivyo ndivyo niwapimavyo wote!
Kiongozi huyu aliporudi kwao akaamua ajaribu nae kuwajaribu mawaziri wake.Akamwita waziri wake mkuu na kumpa swali lile lile, waziri akajikanyaga akaomba muda,akatoka akaenda kumuuliza naibu waziri mkuu, naibu waziri mkuu akamjibu,huyo mtoto ni mimi. Waziri mkuu kwa furaha akatoka akarudi kwa kiongozi wake akamwambia, "mheshimiwa kumbe mtoto yule ni naibu waziri mkuu". kiongozi akakasirika akamwambia "mpumbavu kabisa wewe, mtoto huyo ni waziri mkuu wa uingereza!!!!!
 
Ndo kusema waafrika hawapendi kufikiria bali wanakurupuka tuuu!!!!!!!
 
Back
Top Bottom