kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,317
- 17,581
Mwl. Nyerere alikuwa akiwaasa viongozi wa nchi kuhusu ubaya wa kiongozi kuwa karibu sana na mke wake katika kuiongoza nchi. Mwl alikuwa anaeleza ubaya wa kiongozi kupewa ushauri na mke wake juu ya masuala ya nchi.
Alitoa mfano wa mfalme Kaisari alivyomfukuza mkewe kwa tuhuma tu za ngono. Wakati wake hakukuwa na first lady.
Nyerere aliamini kuwa kiongozi anaemkumbatia sana mkewe hafai kuwa kiongozi, maana atashindwa kumkatalia atakapompa ushauri wa kipumbavu kwa nchi. "Kiongozi kupata ushauri kutoka kwa mkewe wananchi hawatajua nini kitatokea kesho, maana hawajui mkewe atamwambia nini usiku".
Kwa mujibu wa Mzee Nyerere kiongozi mzuri ni yule anaemchukulia mkewe sawa na Raia wengine. Tumeona namna ma first ladies walivyowayumbisha waume wao kwenye uongozi.
Huenda Mzee Mugabe angemskiliza Mwl. Nyerere yasingemtokea haya ya sasa.
Mwl Nyerere alikuwa ni zaidi ya kiongozi bali mtu mwenye maono.