Kuipeleka Brazili uwanjani bila Dinho ni sawa na Kuipeleka JF katika mapambano bila Mwanakjj!
Mnacho sahau ni kwamba Brazil wana dimbwi la vipaji. Kumbukeni 2002 Ronaldinho laichukua nafasi ya Romario. Watu walipinga sana na hadi kocha aka tishiwa kama asipo rudi na kombe la dunia. Matokeo yake yakawa nini? Ronaldinho mchezaji mzuri ila sidhani kama bila yeye Brazil si chocote. Labda kama tunaongelea ushabiki kwa sasa.
Watu mnaopinga uwepo wa 'The Little Ronaldo' jibuni swali hili: Je, mchezaji gani anaziba/ameziba 100% pengo la Ronaldinho katika kikosi cha sasa cha Brazil?
Ngabunho ni kweli Brazili wana gazillion of talents lakini hakuna hata mmoja aliyeziba pengo la Dinho mpaka sasa. Kabla ya Dinho kulikuwa na kina Denilson Machenga, Bebeto na wengineo. Mbadala wa Dinho bado hajapatikana!
Lakini huyu jamaa (Dinho) mi naona kama kiwango kimeshuka tofauti na kipindi kile cha world cup iliyopita.
ni haki yake kutemwa.