juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,041
Me nakataa Mkuu, kwa sababu wamewafunga Korea kwa goal 4?
Uliangalia game ya usiku ya Nigeria Vs Bosnia? Ghana Vs Germany je?
Ya Nigeria ya jana nimetazama kidogo tu.Ghana nimewaona mechi zote,Nigeria nilitazama ile ya kwanza,Ghana na Nigeria wana plans nzuri,lakini siridhishwi na execution,hasa Mobility na accuracy kwenye pasi za mwisho na ufungaji.Algeria naona wako vizuri eneo hilo,na hii ni style ya uchezaji ya timu nyingi za north africa,na hii inawafanya wawe wa kipekee Africa,maana tatizo la pasi za mwisho na ufungaji ni kubwa mno Africa.ukitazama na profile za wachezaji wa Algeria in reference to other african teams in this competition,nadhani hawa Algeria wana kitu cha kipekee.hata hivyo tukirudi maeneo mengine tofauti na attacking,nao wana mapungufu yao in comparison to Ghana,Ivory Coast,etc!Nigeria wanamiliki mpira vizuuri sana,tena nimewaona tangu kombe la mabara wako vizuri eneo hilo,tatizo lao ni mipira ya mwisho na umaliziaji.matokeo yake timu za aina ya Nigeria zikikutana na wapinzani wanaotoa nafasi chache kushambuliwa,itakuwa shida.note;nazungumzia zaidi ushambuliaji,hasa plan and execution.usisahau nafasi ya Algeria kwenye ranking ya Africa,nadhani hawapo pale kwa bahati mbaya.