WOMEN'S DAY

WOMEN'S DAY

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
Happy International Women's Day.

Zama hizi zimejaa wenye jinsia ya kike… kuliko wanawake.

Wanaojifunza kuonyesha mwili kabla ya kuonyesha akili.
Wanaotafuta nje yao sifa za dunia kabla ya kuijenga thamani yao ya ndani.

Sauti zao zimekuwa nyingi kuliko busara...

Maonyesho yamekuwa mengi kuliko heshima....

Na attention imekuwa muhimu kwao kuliko utu wao....

Leo wengi wanajua kuvaa mitindo mipya,
lakini wachache wanajua kuvaa, adabu na utu.

Wengi wanajua kuvutia macho ya watu,
lakini wachache wanajua kulinda thamani yao.

Zama hizi za mitandao wanatoa siri zao za ndani kwa kigezo cha attention na content..


Zimepunguza sana uzito wa adabu.

Ndiyo maana leo wenye jinsia ya kike ni wengi kuliko Wanawake

Ukitafuta Uwanauke na ile heshima iliyokuwa ikiambatana na hadhi ya kike, utagundua imekuwa adimu kama dhahabu....


"Si kila mwenye jinsia ya kike ni mwanamke kama jinsi ilivyo sio kila mwenye jinsia ya kiume ni mwanaume"...


✍️ Abuu Abdillah

Siku hizi wanaona wenye jinsia ya kike na kiume kisha wanaanza kuhubiri ndoa mbaya...
 
Back
Top Bottom