Mbona maneno makali we Mzee ?
Unachokiandika kwenye huu uzi haliendani na uhalisia wa maisha yetu, Jamii ya Watanzania halafu rudi tena soma post # 15 mbona nilieleza vizuri tu ?
Nakuona unaleta ukoloni na ubabe mpaka hapa ? 🤣 Ingekuwa ni face to face si unaweza hata ukampiga mtu risasi ?
Hata hayo maisha yenu Watanzania unaongelea Watanzania masikini wasio na elimu washamba.
Kwa hiyo usiseme wanawake wako hivi.
Sema wanawake Watanzania masikini wasio na elimu washamba wako hivi.
Na hayo matatizo unayoyaona ya wanawake mengine si ya wanawake, ni matatizo ya utamaduni.
Huko Tanzania mnawanunua wanawake kwa ng'ombe mkiwaoa. Mshawajengea utamaduni wa kujiona wao ni bidhaa ya kununuliwa.
Tangu mtoto mdogo mwanamke anajiona yeye ni bidhaa ya kununuliwa.
Kiutamaduni.
Sasa hapo mwanamke akijiweka kimaslahi zaidi, kutaka kuhudumiwa, kupewa pesa, kununuliwa, unaweza kuona wanawake ndivyo walivyo.
Kumbe hilo ni suala la utamaduni mliojiwekea nyie wenyewe, si suala la wanawake.
Kwa sababu, kuna sehemu nyingine wanawake hawako hivyo.
Ndiyo maana ni muhimu uijue dunia kabla ya kusema wanawake wako hivi. Huwezi kutumia mifano ya wanawake wako washamba wa Simiyu na Dar halafu ukahigimisha wanawake wote wako hivi au vile.
Mimi siku nyingi sana niliwahi kutongoza mwanamke, tena mweusi, Mmarekani. Hapo New York City.
Katika kumtongoza nikataka kumtoa out dinner. Akasema angependa twende out dinner, lakini anaona vibaya kwa sababu hana kitu. Sasa mimi kidume wa Kiaffika nikaona aah, hilo mbona jambo dogo tu, nitalipa kika kitu. Nitakuja kukuvmchukua ulipo, nitakupeleka dinner, nitakulipia kila kitu, halafu nitakurudisha kwenu.
Akanishukuru, akasema mimi ni mkarimu sana, ila yeye ana kanuni yake hawezi kwenda sehemu bila ya kuwa na pesa yake mwenyewe kujilipia yeye mwenyewe.
Yule mwanamke alinifikirisha sana. Nikafikiri ingekuwa wanawake wetu wa Uswahilini wasio na kanuni za kifalsafa kama hizi mbona ndiyo kwanza angefurahia sana offer hiyo.
Sasa hapo uaweza kuona utamaduni aliokulia huyo binti umemjenga hivyo, apende kujitegemea, asiwe tegemezi kupita kiasi cha kawaida cha kutegemeana kwenye mahusiano.
Sasa kama umezoea kukutana na wanawake low class wa Simiyu na Dar, unaweza kuwahukumu wanawake wote ukifikiri tabia za hao wanawake wako low class ni tabia za wanawake wote.
Wakati hata hapo Dar Oysterbay na Masaki kuna watoto wa kishua mimi nawajua hawana matatizo yenu, wanaishi katika ma continent tofauti, wana majumba Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Mbezi Beach na Mbweni, wametoka kwenye tamaduni zetu, na wanaziheshimu, lakini wameupita ushamba wa tamaduni zetu.
Wewe unafanya Hasty Generalization Fallacy na Composition Fallacy.
Unafikiri kwa kuwa wanawake unaowajua wewe ni washamba, basi wanawake wote ni washamba.
Kuhusu face to face wewe huwezi kukutana na mimi nje ya hapa JF.
Kukutana na mimi hapa JF ni privilege kubwa sana kwako, na face to face sehemu ninazopita mimi wewe huwezi fika, ila hujajua tu.