Woga wangu wa kuegesha gari Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Woga wangu wa kuegesha gari Dar!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, Feb 21, 2012.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Katika taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili jioni leo nimeona kuwa ile kampuni inayokamata magari ambayo yanayoegeshwa katika sehemu 'ambazo sizo', mkataba wake unaisha na hautaongezwa. Nimepokea taarifa hizi kwa furaha kwa vile nilishaanza kuogopa kuendesha nikiwa Dar kwa woga wa gari kukamatwa baada ya kuegesha sehemu ambayo haina hata alama kuwa usiegeshe. Kuna mdau mwanajamvi aliweka post humu asubuhi akilalamika aliipishwa shs. 195,000, naona kilio chake kimesikika
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mkataba wa kampuni porapora unaisha mwezi huu.....
  Tusubirie kampuni mpya.......
   
 3. M

  Ma Tuma Senior Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wale wanaokamata magari ni majambazi.na hawafai hawajaenda shule.ka wameagizwa na mabosi wao kwa ukamataji ule basi na hao mabosi ni hamnazo.
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi Jiji haliwezi kuwa na kitengo chake maalum cha kushughulikia jambo hili? Kunahitajika kitengo cha kitaalamu, kinachojua sheria na jinsi ya kufanya kazi hiyo na mafunzo kamili kutlewa. Ni janga kuchukua watu mitaani na kuwapa kazi ambazo matokeo yake yanaweza kuleta matatizo hasa ya kisheria.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kitengo maalum halafu wenzenu wataishije mjini? Acha wapeane tenda,

   
 6. M

  Mukalabamu Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wale wahuni wa kutupwa nikikuta wanapigwa mawe namimi nitarusha nina hasira nao sina mfano.Waliingia uswazi kwet saa nane usiku wakiwa na marungu na mapanga na breakdown kama nne.Kuna sehemu huwa tunapaki magari kama watu 7 hivi na kuna mlinzi tunamlipa.Waliyafunga yote na kuyaburuta mpaka yadi yao sinza kuwa tumetengeneza gereji bubu.Mlinzi aliniita nikakuta wameishaondoka nalo.Ina maana mlinzi asingekuwepo wala tusingejua magari yameenda wapi!kufuatilia kwenye yadi yao tukaambiwa tulitengeneza gereji bubu kwa sababu pale kulikuwepo na gari kukuu!gari lilipondeka na handbrake ikaaribika!hasira nilizokuwa nazo nafikiri kama ningekuwa na bastola mfukoni ningefanya kitu cha ajabu!nilimrushia wheel spana mlinzi ikamkosa baada ya kumuuliza kama mi nalipa gharama za ulinzi na uharbifu wa gari langu nani anahusika akasema hiyo haimhusu!nililipa 195,000 mpaka sasa nikizikumbuka zinaniuma sana!
   
 7. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ile kampuni iliyokuwa inafanya huo "uporaji" inaitwa Mwamkinga Auction Mart. Sitasahau siku ile walipopora gari yangu nilipokuwa nimeigesha pale Tarakea hotel, Mwenge. Na siku hiyo niliwaambia kuwa huo wizi wanaofanya utafikia mwisho na utawatokea puani. Mungu mwema amesikia kilio chetu!
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Afadhali tupumue, kama tulivyopumua na Yono. Mie juzi juzi walifunga mnyororo kwenye tairi pale ubungo terminal ya mabasi makubwa. Nina hasira nao ile mbaya
   
 9. landless

  landless Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh na walaanniwe wezi wakubwa wale,ninahasira nao hadi kesho,nikikutwa wanauliwa hata kama ni maiti mi ntaendelea kuipiga au hata kuzikata kata kwa msumeno butu hadi wakatike,haiwezekani mtu na akili timamu unaibiwa tena kwa lazima,pesa yenyewe tabu alafu unakutana na mambo ya kishenzi kama haya mjinga mmoja ninahakika hawezi kutushinda,wanaweka vikao vya kupeana tenda za kipuuzi,jamani namtafuta bosi wa hii kampuni mwenye kuwafahamu please nina shida naye sanaaaaa.195,000,nimepaki na mimi nipo pembeni mwa gari,gari limeshafungwa,halafu wanaomba rushwa ya 65000 wakuachie,wa mbele yangu sijui kaongea nao nini kaachiwa nayeye alikuwa mbali na gari pale ustawi opposite na hongera baa,10min imenitoka 195,000.Inauma sana,kibaya zaidi pesa ynyewe nlikuwa naendea hospitali so sick.Ni ujambazi wa hali ya juu.Im not ready to keep quit hata mkataba ukiisha kuwatafuta ni muhimu.
   
 10. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  Mi nadhani tatizo lipo kwa watoaji au wasimamiaji wa mkataba huu, kwa hio hata akimaliza huyu haitasaidia unless kufanyike marekebisho ya huo mkataba. Haiwezekani mtu akajifanyia mambo kivyake au bila kufuata mkataba na serikali ipo asisimamishwe haraka, ndo maana wanasubiri muda wake uishe coz hawawezi kuubadili juu kwa juu na ndio unampa mkandarasi faida kwa vile anakamata ovyo magari mengi kwa siku. Pengine fungu alilopewa awakilishe kwa siku ni kubwa na ukamataji usiozingatia uwekaji alama kwanza.
  Mimi kila siku hujiuliza hawa waTZ wanaopewa madaraka mbona kila sehemu wanakoroga tu? Tatizo ni nini Shule waliopitia wengi ni Magumashi?
   
 11. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni ubinafsi na ulafi. Kuna watu wako tayari kuwaibia wengine kwa njia yeyote ile ili mradi tu wao wapate. Hawa jamaa walichokuwa wanakifanya ni kukamata idadi fulani ya magari kwa siku ili hela itimie tu. Haiwezekani useme unasafusha jiji halafu unakamata magari mawili mengine unayaacha. Mfano pale Tarakea hotel Mwenge tunapaki magari kila siku, halafu siku moja nikakuta gari langu limechukuliwa na mengine yapo, hata leo watu bado wanapaki pale
   
 12. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Manispaa watenge maeneo ya parking, ni ajabu kuona wanatenga eneo kwa ajili ya soko kama pale mwenge then hawaweki parking, sasa mtu anaekuja kufanya shopping apaki wapi gari yake? Ninaamini sasa kwamba kuna watu wanapewa nafasi za kazi ila ni hewa kabisa kichwani (Tabula rasa). Siamini kama mtu mwenye akili anaweza kutoa order kama ile. Watenge maeneo ya parking ndo waanze kukamata magari. Mambo ya kufananisha bongo na sweden, finland hapa haiapply mji haujapangwa vizuri, mchafu, miundombinu mibovu, makelele kila kona then ufananishe na kwa wenzetu! Mambo ya ajabu sana.
   
Loading...