Wizi wakati wa kuweka pesa kwa wakala

Kuishi mjini. Fedha haiwekwi bila kuhesabiwa. Huo waliokuibia ni wizi wa zamani sana Manzese Msufini (kwa sasa darajani). Ilikuwa unauziwa suruali ya Rocky baadaye anasema aah, hela yako kidogo bwana inabidi tutoe mkanda...kwa kuwa hutakuwa radhi, utadai urudishiwe pesa yako. Muda huo tayari keshatoa noti ya ndani kaweka karatasi. Ukipokea tu hela ananyakua suruali yake, hutamuona kamwe.
Nashukuru kwa kunifungua kiakili
 
...DSM hii hii umepigwa kizamani hivyo?..
..pole mkuu.,hapo kisomo tu atazirudisha mwenyewe!
 
Du ni ya kukusikitikia jinsi Hali ilivyongumu Du pole sana.

Ni kweli kwa hali hii ya biashara,ukame wa hela na faida ndogo zitolewazo na hiyo mitandao kwa miamala wakala aifanyayo huyu tapeli kamrudisha nyuma sana.Nakubali mazingaombwe ya namna hii yalishawahi kuletwa na kujadiliwa hapa Jf siku za nyuma ila sio lazima isomwe na kila mtu.Hayo ni mazingaombwe alifanyiwa na huyo tapele na hata angerudia kuzihesabu mara tano asingeweza kugundua ni noti za elfu mbili mbili alipewa.Dawa ya kumpumbaza ilikuwa mfukoni mwa tapeli na hadi aondoke ndipo unaposhtuka.Huyo tapeli hawezi kuwa amejisajili kwa majina yake halisi hivyo sio mitandao wala tcra wanaoweza kumsaidia bali ahesabu tu ni hasara imetokea kwenye kazi yake na bahati yamemkuta mwenyewe na sio mke au mfanyakazi.Hili liwe ni funzo kwa watoa huduma wote wa fedha kuwa mteja akishakukabidhi hela umeshazihifadhi akighairi na kuzitaka usikubali tena kuzipokea na kumwekea.Tena huyo huenda bado hajafuzu vizuri au alikuwa na kachembe ka huruma.Wengine wakali zaidi pamoja na kumrudishia hela yake na za kwako ulizokuwa nazo anaondoka nazo kimazingaombwe hivyo hivyo.Pole sana ndugu yangu.
 
Ni sheeda
 
Pole sana ndugu ,niliwahi kusikiliza clouds matapeli wa mtindo huo wanaongea live jinsi wanaiba ,kwanza wanakuwa zaidi ya mtu mmoja ambaye atafanya kazi ya kubadilisha huo mfuko original wa pesa na wengine wa kuamulizia ugomvi kama itatokea watamstukizia unapewa hizo pesa kama walivyokupa then alipokwambia umuwekee na zakutolea ndio alipokuchanganya na mwenzake akampa mfuko au pesa fake,alipoghaili ndio alipobadilisha ule mfuko au pesa na kukupa fake baadae akasema basi ngoja tu nimtumie ndio alikuwa ameshakubadishia ,kwakuwa ulikuwa umeshazihesabu utakuwa huna wasi unaziweka kwenye droo ndio inakuwa basi tena Plz let be careful na watu wanaghaili malipo then wanakubali tena.
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mfanya biashara katika biashara yangu pia nimeweka mambo ya huduma za kipesa za mitandao (Wakala), sasa jana majira ya saa tisa kuna mtu alikuja akasema:

Jamaa: niwekee Tigo pesa laki 8 na voda niwekee laki moja
Mimi: poa (jamaa akanipa pesa nikazihesabu zikawa sahihi laki 9).
Jamaa: Ah niwekee na 7500 tigo pesa na 3000 voda nifanye kama ya kutolea maana baadae nitazitoa.
Mimi: poa (jamaa akanipa 10500)
Jamaa: Ah sikia basi nipe hizo pesa nimeghairi (mimi nikamkabidhi)
Jamaa: lakini poa we niwekee tu maana kutembea nazo pia naona ovyo (jamaa akanikabidhi tena).

Mimi nikazichukua zile pesa nikazieka katika droo nikamuekea kisha akaondoka dah! Nakuja kuzicheki zipo laki mbili zilizojaa 2000 na 10000 tatu, nikajaribu kuwapigia Voda wamesema jamaa kashazitoa ila nenda polisi alafu nenda TCRA, nikwapigia Tigo wamesema jamaa kashazitoa nikwauliza mtanisaidiaje wamesema hatuna cha kukusaidia.

HIVI WAKUU NINI NAWEZA KUFANYA?
Pole sana. lazima uwe makini na kuzingatia pale unapofanya miamala ya pesa nyingi. Kumbuka kufuata maelekezo ya kudai kitambulisho na pia waelewe wateja wanaeza kupoteza.
 
Akikupa mara ya pili nafikiri ni vyema ukarudia kuhesabu.
Mcukulie kama mteja mpya, dont trust any body pale Cash inapo-exchange hands. Kuna dadangu alipigwa nayo hiyo mwaka 2013. Long time
 
Jamaa (tapeli) atakuwa alikuwa na mafungu mawili ya fedha moja lenye fedha taslimu za elfu kumi kumi na jingine lenye noti za elfu mbili mbili katikati. Fungu la kwanza lililotimia ndilo alilompa wakala mara ya kwanza. Tapeli aliporudishiwa akatoa fungu la pili likiwa na elfu kumi kwa juu huku katikati kuna noti za elfu mbili na kumrudishia tena wakala ambaye aliamini kuwa fungu ndilo lile lile la kwanza alilokwisha hesabu. Kampa... Kampa.... Kampa tena! Pole mkuu.
Na sometimes huwa wawili pia. Ukimpa anampa mwenzie, mwenzie anampa fungu feki na kukurudishia. UNAPIGWA
 
Vitambulisho na picha za kusajilia wanatoa wapi?
haaa wewe wakati wa kujisajili wala hawako makini ,,,shida yao ilikua kuuza line tu wapate volti,,kwanza data basse ya kusave hizo picha nani atagaramikia,,,
 
Kuna the same case iliripotiwa humu kutoka Zanzibar..Pole sana
 
Hapana nadhani hapa hakuna kumlinda mlaji.mbona watu wakitukana kwenye mitandao kuna kumlinda mlaji na kumjua ni nani anayehusika sasa niulize kitu kimoja wanashindwa nini kumfuatilia aliyechukua pesa
Hii kesi ni ngumu, kwanza watathibitisha vipi kuwa huyo mteja ndio mwizi na sio ww wakala ndio unataka kumwibia mteja? Suala lako huwezi saidiwa popote halina ushahidi kwasababu kwanza wakiamua kukurudishia, what if ww ndio wakala unayetaka kumwibia mteja baada ya kumwekea!!! Hili suala lina pande mbili. Hata hivyo ushahidi pekee ni muda uliotumika kati ya kuweka fedha na kutoa, zikipatikana taarifa kama hizo polisi wanaweza kum-interogate kwamba kwann aweke fedha na kuwithdrawal muda huohuo.... Changamoto ni je atapatikana?? Huenda hata hizo simcard keshazichoma moto.
 
Back
Top Bottom