Sukari Yenu
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 1,698
- 1,255
Habari za asubuhi waungwana,
Kuna kitu kimenishtua sana. Nimefuatilia deni langu ninalodaiwa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu au HESLB kama inavyofupishwa kwa kimombo.
Nimepokea statement ya mchanganuo wa deni hilo ili kuarrange malipo, kimsingi una kasoro moja. Vitu vingine vyote viko sawa.
Kuna pesa ya Research tulipokuwa mwaka wa mwisho wa masomo. Katika kumbukumbu zangu mimi na wanafunzi wenzangu tuliitwa kusaini na aliyekuwa Loan Officer wa chuo. Tuliishia kusaini tu, hiyo pesa haikuingia kwenye akaunti zetu. Sasa Loan Board watuambie kama walizituma fedha hizo vyuoni ili tujue kule chuoni kuna majipu yakatumbuliwe au ni nyinyi Loan Board hamkutuma mkatubambikia deni. Pesa yenyewe ni TZS 100,000 tu, lakini kwa idadi wa wanafunzi wote waliosaini kisha wasiwekewe ni fedha nyingi sana. Hii si sawa kulipa fedha ambayo hakuitumia na haipo kimehesabu na kimkataba.
Mheshimiwa Rais Magufuli na Waziri wa Elimu tunaomba muichunguze hii board kwa umakini. Inawezekana kuna wanafunzi hewa wanaolipwa mikopo kama ilivyo wafanyakazi hewa wanaolipwa mishahara na halmashauri. Na kule vyuoni nako kuchunguzwe, kuna mahali watu wanafanya sivyo ndivyo.
Kwa wale wanaotaka kutumiwa details zao za madeni, use the following email adress. Andika namba yako ya mtihani wa O level na mwaka uliomaliza, Chuo ulichosoma na detail zingine muhimu.
emtavangu@heslb.go.tz