Wizi wa vyandarua na dawa zahanati ya Kerenge Wilayani Korogwe mkoani Tanga

the kind

JF-Expert Member
Nov 6, 2019
776
573
Habarini wanajamvi,

Kabla ya kupoteza muda tuende kwenye mada moja kwa moja,kuna wizi wa vyandarua/neti robota 2 ambao ulitokea usiku wa kuamkia jana katika zahanati ya kerenge lakini mshukiwa akawa amekamatwa na jana akawa amefikishwa kituo cha polisi wilaya.

Lakini baada ya tukio kutokea watumishi wa zahanati hiyo walipokwenda stoo ya dawa kukagua ndipo walipokuta upungufu mwingine wa vyandarua robota nne ukiacha zile mbili zilizokamatwa lakini pia baadhi ya dawa iligundulika kuwa zimepotea pia.

Kabla ya hapo kumekuwa na matukio mengi ya wizi katika zahanati hiyo na mali nyingi zinazoibiwa huwa zinahifadhiwa stoo ya dawa ambapo kunakuwa na mtumishi mmoja ambae anakaa na funguo ya stoo ya kuhifadhia dawa na siku zote wizi unapotokea huwa hakuvunjwi.

Lakini jambo jingine mshukiwa aliekamatwa na robota 2 usiku wa kuamkia jana ni mtu mwananchi ambae huwa anashirikishwa katika shughuli mbalimbali katika zahanati hiyo mfano usafi wa mazingira, ugawaji wa dawa za mabusha na matende.

Pia kwenye kampeni ya chanjo ya surua ya kitaifa iliyofanyika mwezi wa 10 pia alikuwepo kwahiyo ni mtu ambae amehudumu kwa muda wa miaka hata 10 iliyopita. Lakini pia mshukiwa alishitukiwa na kukamatwa na wananchi.

Sasa kitu kinachonishangaza au pengine mimi ndio sifahamu, leo baada ya mtumishi mmoja kuchukuliwa maelezo akaambiwa jumatatu aende na mashahidi ambao ni wananchi waliomkamata yule mshukiwa aende nao ofisi ya upelelezi wakahojiwe.

Sasa ni sahihi wale mashahidi kwenda kuhojiwa ofisi za upelelezi au ni sahihi kwenda kutoa ushahidi mahakamani?

Pia mshukiwa aliyekamatwa ana undugu na diwani wa kata hiyo na pia mtu mwingine ambae alikua kwenye tukio ambae yeye alifanikiwa kukimbia japo wananchi wamemfahamu ila bado hajakamatwa kutokana na kutokuwa na uthibitisho uliokamilika pia na yeye ana undugu na diwani wa kata hiyo.


Je wanajamvi nini maoni/vision yenu katika jambo hili?
 
Kerenge panasifika sana kwa uchawi. Kinachonishangaza badala ya kumroga mwizi fasta na kumshusha george busha wanakuja kushtaki kwa Ummi Mwaimu. Mkiona vipi mpigeni hata zongo aumwe na tumbo au mpigeni ndere amalizie hiyo pesa kwa wake za watu. Au mpigeni MMA mmalize ukoo wake.
 
Back
Top Bottom