Wizi wa vipuli vya magari Dar-es-salaam na ukimya wa polisi na Serikali

Siku hata wizi wa magari umeongezeka saaana..
Naona wahusika wako kimya sana..
 
Kipini flani Q Chief alikua anatuhumiwa kuwa sehemu ya huo mtandao wa wizi wa vifaa vya magari pale mlimani city sijui iliishiaga wapi.
 
Mtandao huo ni mkubwa sn....sisi tuliwahi kuwafukuzia wakat wameshaiba wakakimbia wakaacha gari waliyokuja nayo toyota carina tukaifungia sehem wiki 2 hamna aliyejitokeza kuja kuidai tukaenda kukata screpa tandale wale walioibiwa mwanzo wote wakapewa hela na tokea mwaka juzi mtaani kwetu hamna tena huo wizi
 
Ni wakati wa kupafunga hapo gerezani.

Na kuweka udhibiti wa maduka yote yanayouza used spare parts. ......

Inakuwaje wizi huu wa maka na miaka unashindwa kudhibitiwa???
 
Kwa kweli polisi inabidi wajipange haswa, yaani wanajibu kama vile acha waendelee kuwamaliza haiwahusu.

IGP anza kubadili tabia za polisi wako, inaelekea labda wanapata chao kutoka kwa hawa wezi.

Ni kweli huo gerezani pashughulikiwe haraka sana
 
Nimepita mitaa ya sinza jana asubuhi, nimekuta hao jamaa wameiharibu IST ya mtu kwa kung'oa bumper ya mbele, show grill, taa zote za mbele na nyuma, side mirrors na bado wamevunja kioo kidogo cha pembeni nyuma ya gari. Walichofanya ndani ya gari sikijui. Cha kushangaza, huo mtaa "unalindwa na walinzi shirikishi" ambao kila mwezi wanavuta mshiko wa ulinzi.

Kinachotakiwa nikushulikiwa hao walinzi shirikishi , mara nyingine wanausikaga, na kama nilivyosema hamna kinachoshindikana,
ukiwaminya vizuri ukweli utaupata, unatakiwa uwape mda kidogo wasahau,
 
bado unawategemea polisi wa hii nchi? tena saivi wana kiki yao moja wapo busy na kibiti wanasema
 
Hakuna mwizi anayehangaika Na vifaa vya VITZ maana nani atanunua? Ulishawahi kusikia duka la vifaa vya Bajaj?
 
Mweshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kaonywesha kuguswa na kafanya maamuzi juu ya uwizi wa magari kwenye jiji la Dar es salaam,akiongea kwenye Star TV

Tunaomba Mweshimiwa IGP naye asilifumbie macho ,

Ili ni JIPU, na wanaousika ni vijana wadogo , tena wana silaa, dawa za usingizi za kupulizia kwenye nyumba za watu, na dawa za kupulizia kioo ili kilainike kwa uraisi wa kukivunja.


walikuwa wanaiba kwenye mabaa, mahotel, maofisini, nje ya majumbani kwa watu kukiwa kuna sherehe au msiba na sasa wameanza kuingia kwenye nyumba za watu usiku na kupulizia dawa za usingizi alafu wanafanya mambo yao. vilevile wameanza kuingia kwenye yard za magari na parking za magari za CCM kwa kuwatishia walinzi na bastola.

Vitu wanavyoiba kama ifatavyo: Taa za mbele na nyuma, power window controller, dashboard, redio, side mirrow, bumper za nyuma na mbele, show ya mbele, wakipata mda wanachomoa control box, hadi milango ama kioo cha mbele

Mie kinachonishangaza ni kila mtu anajuwa vitu vinapatikana GEREZANI na mpaka imefikia watu wengine wakiibiwa ata hawariport police wanaenda moja kwa moja GEREZANI kununua vitu vyao na wakivipata wanarudi wakifurai kama mazuzu hivi, "Utasikia nimevipata bwana vilevile, nimetoa laki saba tu! " angali kwamba ni ujanja kuhuziwa mali yako mwenyewe

Tupige hesabu kidogo (kwa kukadiria tu):

mfano: kiwango cha chini tufanye magari 20 yanaibiwa spare parts kwa siku.

wastani wa bei wanazonunulia watu vitu vyao wenyewe ni 1,500,000/ kwa gari moja (magari mengine yakuwaga 3mln,mengine 2mln na mengi ni laki 6-8)

magari 20 x 1,500,000/ = 30,000,000/ kwa siku moja tu!
7 x 4 x 30,000,000/ = 840,000,000/ kwa mwezi mmoja
12 x 840,000,000/= 10,080,000,000/ kwa mwaka

( Tufanye wanaiba miezi sita tu miezi sita mingine wanapumzika), Hiyo hela tugawanye kwa mbili ni SHs 5,040,000,000/ kwa mwaka

Kwa wasiohelewa hiyo ni billioni tano na millioni 40 kwa mwaka , hela ambayo haikatwi kodi ya haina yoyote,

Tunashindwa nini kwenda kupafunga Gerezani Mnadani na kuwakamata wausika. Kwa ujumla ni eneo linalo ifadhi vitu vya ujambazi, Mpaka wanajigamba kwamba “Si Serikali ya Magufuli wala ya Mtu yeyote itakayoweza kuwafanya kitu”.

Hii ni kauli ya Dharau kwa vyombo vya Dola na Serikali ya Rais wetu Mchapa kazi Magufuli asiyependa watu kama hao wanaotaka kuishi kwa majasho ya watu wengine.

Ombi langu kwa wananchi wenzangu:

Mie nimeanza kupaza sauti , lakini sauti yangu ni ndogo sana, tukishirikiana mimi na wewe hii sauti itakuwa kubwa na itasikika, na Amin’ na waambia RAIS WETU MAGUFULI Hashindwi kuwashughulikia awa watu na hii tabia ikapungua ama kuisha kabisa.

Mkuu Wa Mkoa Ameanza , Je wewe !!!

Note: HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KATIKA DUNIA.
 
Nadhani hili swala makonda angelivalia njuga kama madawa ya kulevya ingemuongezea ufanisi
 
Dawa ni kuangalia kwa karibu hii biashara ya vipuri vya magari. Na hapo gerezani pafungwe na vibali vitolewe kwa watu maalum watakaokuwa monitored kirahisi. Polisi wachunguzwe sana kwenye hilo kuna askari wanashiriki kwenye huu uhalifu kama ilivyo kwa baadhi yao kushiriki kwenye uhalifu kama wa madawa ya kukevya na utapeli wa madini.
 
wakimaliza vifaa hivyo watakuwa wanaiba magari mazima na kwenda kuyachinja wapate vifaa
 
Back
Top Bottom