Wizi wa vipuli vya magari Dar-es-salaam na ukimya wa polisi na Serikali

Mzalendo07

Member
Feb 24, 2014
71
120
Nimerudi kutoka kazini mida ya saa 12 jioni, nikapaki gari langu ndani ya fence, nikaamua niangalie TV na nakufanya shughuli zangu za ofisini.

Baada ya kula mida ya saa mbili, nikaenda kulala mapema tu.

Naamka hasubuhi, nakuta gari limesogweza karibia na geti na limeibiwa vipuli vya gari, (kuanzia taa za mbele na nyuma, site mirror, bumper la mbele na nyuma, na vitu vya ndani).

Nikaamua kwenda Police kuripoti, nikaambiwa awa watu wako sana na hizi kesi tunazipata kila siku ya mungu, na Police wawili wakakiri ata wao wameshaibiwaga.

Baada ya kuongea na rafiki zangu kuhusu tukio langu, nikaambiwa kitu hichohicho kwamba ata maeneo yeo wamepiga magari kama manne siku za karibuni, na wengine wakinisimulia matukio hayo ya uwizi yalivyowatoke kwao au kwa familia/rafiki zao miezi michache iliyopita.

Kitu kimoja walichokuwa wanaongea sawa na kukubaliana (Police and Raia) ni kwamba wote wanajuwa hivyo vitu vinapopelweka “GEREZANI MNADANI”. Na ata vya kwangu nikaambiwa viko na mpaka wanajuwa vimeibiwa wapi na lini.

Swali langu na natumaini watu wengi wanajiuliza!

Kwa hiyo hii taabia itaendelea mpaka lini? Tunazungumzia vifaa vyenye thamani mpaka zaidi ya million 7 saa nyinginee watu wanaibiwa na visivyopunguwa laki 6.

Hii ni biashara kubwa yenye mtandao mkubwa na inaaribu uchumi wa wananchi wema na kama sio wa Nchi.

Tunashindwa nini kwenda kupafunga Gerezani Mnadani na kuwakamata wausika watoe ushirikiano kuhusu watu wanaofanya uwizi huwo. Kwa ujumla ni eneo linalo ifadhi vitu vya ujambazi, Mpaka wanajigamba kwamba “Si Serikali ya Magufuli wala ya Mtu yeyote itakayoweza kuwafanya kitu”.

Hii ni kauli ya Dharau kwa vyombo vya Dola na Serikali ya Rais wetu Mchapa kazi Magufuli asiyependa watu kama hao wanaotaka kuishi kwa majasho ya watu wengine.

Ombi langu kwa wananchi wenzangu:

Mie nimeanza kupaza sauti , lakini sauti yangu ni ndogo sana, tukishirikiana mimi na wewe hii sauti itakuwa kubwa na itasikika, na Amin’ na waambia RAIS WETU MAGUFULI Hashindwi kuwashughulikia awa watu na hii tabia ikapungua ama kuisha kabisa.

Note: HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KATIKA DUNIA.
 
Wahusika wapo humu wanasikia na uzuri Mkuu SIRRO ni kiongozi mbunifu tunaamini atalifanyia kazi.
 
Hii organized crime imekuwa serious. Nadhani ni fursa nzuri ya RC wetu kudhihirisha uenyekiti wake wa kamati ya usalama!
 
Niliwahi kuangalia documentary ITV kuhusu hii ishu aisee...Cha kushangaza baadhi ya polisi wanawajua ila wanadai mtandao wao ni mkubwa sana...unaibiwa kifaa chako halafu unakuja kukinunua mwenyewe
 
Nimerudi kutoka kazini mida ya saa 12 jioni, nikapaki gari langu ndani ya fence, nikaamua niangalie TV na nakufanya shughuli zangu za ofisini.

Baada ya kula mida ya saa mbili, nikaenda kulala mapema tu.

Naamka hasubuhi, nakuta gari limesogweza karibia na geti na limeibiwa vipuli vya gari, (kuanzia taa za mbele na nyuma, site mirror, bumper la mbele na nyuma, na vitu vya ndani).

Nikaamua kwenda Police kuripoti, nikaambiwa awa watu wako sana na hizi kesi tunazipata kila siku ya mungu, na Police wawili wakakiri ata wao wameshaibiwaga.

Baada ya kuongea na rafiki zangu kuhusu tukio langu, nikaambiwa kitu hichohicho kwamba ata maeneo yeo wamepiga magari kama manne siku za karibuni, na wengine wakinisimulia matukio hayo ya uwizi yalivyowatoke kwao au kwa familia/rafiki zao miezi michache iliyopita.

Kitu kimoja walichokuwa wanaongea sawa na kukubaliana (Police and Raia) ni kwamba wote wanajuwa hivyo vitu vinapopelweka “GEREZANI MNADANI”. Na ata vya kwangu nikaambiwa viko na mpaka wanajuwa vimeibiwa wapi na lini.

Swali langu na natumaini watu wengi wanajiuliza!

Kwa hiyo hii taabia itaendelea mpaka lini? Tunazungumzia vifaa vyenye thamani mpaka zaidi ya million 7 saa nyinginee watu wanaibiwa na visivyopunguwa laki 6.

Hii ni biashara kubwa yenye mtandao mkubwa na inaaribu uchumi wa wananchi wema na kama sio wa Nchi.

Tunashindwa nini kwenda kupafunga Gerezani Mnadani na kuwakamata wausika watoe ushirikiano kuhusu watu wanaofanya uwizi huwo. Kwa ujumla ni eneo linalo ifadhi vitu vya ujambazi, Mpaka wanajigamba kwamba “Si Serikali ya Magufuli wala ya Mtu yeyote itakayoweza kuwafanya kitu”.

Hii ni kauli ya Dharau kwa vyombo vya Dola na Serikali ya Rais wetu Mchapa kazi Magufuli asiyependa watu kama hao wanaotaka kuishi kwa majasho ya watu wengine.

Ombi langu kwa wananchi wenzangu:

Mie nimeanza kupaza sauti , lakini sauti yangu ni ndogo sana, tukishirikiana mimi na wewe hii sauti itakuwa kubwa na itasikika, na Amin’ na waambia RAIS WETU MAGUFULI Hashindwi kuwashughulikia awa watu na hii tabia ikapungua ama kuisha kabisa.

Note: HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KATIKA DUNIA.
Mh. Mwigulu Nchemba kwanini unashindwa kuthibiti kitu kidogo namna hii???
 
Nimepita mitaa ya sinza jana asubuhi, nimekuta hao jamaa wameiharibu IST ya mtu kwa kung'oa bumper ya mbele, show grill, taa zote za mbele na nyuma, side mirrors na bado wamevunja kioo kidogo cha pembeni nyuma ya gari. Walichofanya ndani ya gari sikijui. Cha kushangaza, huo mtaa "unalindwa na walinzi shirikishi" ambao kila mwezi wanavuta mshiko wa ulinzi.
 
mkuu pole sana..kwa kweli wizi huwa unatia hasira sana..coz wanaturudisha sana nyuma hawa wshenzi...naomba unijibu hili swali, Wamewezaje kusogeza gari ambayo umepaki..walikuja na crane? au waliinyanyua kwa mikono? naomba tuaznie hapo
 
Jamani kupigwa vifaa vya gari inaumiza sana sikieni tu,yaan umepaki gari umeingia sehemu wanakuibia hadi vitu ndani ya gari na sehemu nyingine walinzi wanashirikiana na hao mwezi.haipendez na inaumiza
 
Back
Top Bottom