Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,160
- 157,207
Kumekuwa na ongezeko la wimbi la wizi wa magari hasa jijini DAR ES SALAAM.
Kwenye groups za WhatsApp hazipiti siku kadhaa linaletwa tangazo kuwa Kuna gari limeibiwa.
Magari ambayo yamekuwa yakiibiwa zaidi Ni TOYOTA IST na mengine yenye injini za 1NZ na 2NZ.
Hapa ni baadhi ya mbinu zitumiwazo na wezi wa magari.
1. Kufunga GPS kwenye gari wanalotaka kuliuza ili waliibe in future
Kuna mchezo hua unafanyika, aliekuuzia mmiliki/dalali Gari anabaki na Funguo au hata kuchonga.
Kama huo funguo hauna Sensor halafu gari linakua lina GPS tracker somewhere after sometime wanakuja kuchukua kama yao itakapokuwepo.
2. Car wash/ garage kuchonga funguo za gari yako
Garage na sehemu za kuoshea magari kukiwa na watumishi wasio waaminifu wanaweza kuliwekea alama gari yako, wakachonga funguo na kuanza kukufuatilia na kisha kuiba gari yako. Pendelea kuoshea gari nyumbani au uwe na sehemu moja tu ya kuoshea. Na pia Ni vyema ukawa na sehemu moja tu na fundi wako mmoja wa kushughulika na gari yako.
3. Special app hutumika kwa keyless vehicles
Kwa magari ambayo ni keyless, Yale yasiyotumia funguo kuingia ndani wezi hutumia special app ambapo hizi mbinu hutumika:-
Signal relaying
Signal jamming
Key programming
Code grabbing