everybody
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 337
- 103
Jamani kwa wale ambao mnatumia njia ya chini, Old bagamoyo road a.k.a Mwai Kibaki road, na kuweka mafuta kwenye petrol station ya OILCOM iliyopo maeneo ya Reinbow pale panapouzwa samaki (Njia inayopandisha kwenda kutokea Tangi bovu), kuweni makini na wale wauzaji.
Zaidi ya mara mbili jamaa walitaka kuniibia mafuta. Style wanayotumia ni kuanzia pale ambapo mteja wa mwisho aliweka na wanaendeleza zile units. Mfano kama mteja wa mwanzo aliweka 10,000 na wewe unataka mafuta ya 50,000 hawarudishi mashine yao ikasoma 0 kabla ya kuanza kukuwekea. Kuweni makini na muangalie kama units zimerudi kwenye sifuri (0) kabla hawajaanza kukuwekea mafuta.
Mara ya kwanza nilidhani bahati mbaya, ila nikawashtukia mara nyingine mbili ikabidi niwakoromee. Kuna na mtu mwingine alishaniambia kwamba hili limemtokea. Kuweni waangalifu.
Nimeona niwape hili angalizo msije na nyie mkaliwa.
All the best.