Ndugu yangu Elli nashukuru kwa kuwataarifu wajumbe.
Kusemakweli huo ni ukweli mtupu, maana yapata mwezi mmoja sasa mdogo wangu yalimkuta pale Ikulu kuelekea kituo cha Kivukoni toka wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Laptop yake ilivutwa na mkanda wa lile bedi ulimnasa shingoni, alianguka akapiga kichwa kwenye tairi kabla ya kuburuzwa umbali mrefu kiasi kisha akapoteza fahamu, Chakushukuru ni kwamba hakupoteza maisha.
La muhimu
Wale Mabrazamen na Masista du, wanaopenda ujiko kwa kujidai wamebeba laptop huku ndani ya begi kukiwa na makaratasi tu tena yasiyo na ishu nawaombeni sana muwe makini. Mtakuja poteza maisha bure wakati laptop hamnazo. Hii ni ishu serious wazee kuweni makini.