Wizi wa kura katika zoezi la kura za maoni CCM hadi ngome ya JK ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa kura katika zoezi la kura za maoni CCM hadi ngome ya JK !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Aug 6, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ngome ya JK kusambaratika?

  [FONT=&quot]Na Waandishi Wetu, jijini - Dar Leo.
  [/FONT]​

  [FONT=&quot]KATIKA ngome ambayo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, anaishi na kufanyia kazi, Kivukoni, imeibukwa na mitafaruku kwa kulalamikiwa kuwa ni miongoni mwa maeneo yaliyohusishwa na wizi wa kura.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wakizungumza na gazeti hili kwa masikitiko, baadhi ya wanachama wa chama hicho wa shina la Edward Moringe lililopo Kata ya Kivukoni, wamedai kuwa vitendo vya wizi wa kura katika zoezi la kura za maoni vimewasikitisha kwa kuwa ni ngome ya rais JK. [/FONT]

  [FONT=&quot]Wameongeza kuwa tawi hilo lilikuwa likifanya uchaguzi kwa amani kwa miaka mingi, lakini hivi sasa limeinigiwa na dosari inayochafua jina na umaarufu wake ambapo ndipo penye ofisi kuu ya Serikali.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wamesema kata hiyo imeonesha ni jinsi gani katika kura za maoni kulikuwa na ukiukwaji wa sheria uliosababisha baadhi ya wanachama kushindwa kupiga kura.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mwenyekiti wa shina hilo, Saidi Likoko, ameliambia gazeti hili kuwa amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wanachama kushindwa kupiga kura kwa sababu zisizofahamika.[/FONT]

  [FONT=&quot]Amesema shina lake lina wanachama 26 wenye vitambulisho lakini cha kushangaza wanachama 17 ndio walioruhusiwa kupiga kura huku wengine majina yao kutoonekana.[/FONT]

  [FONT=&quot]"Nilipeleka majina ya wanachama 26, lakini waliopiga kura ni 17 tu, na nilitoa taarifa kwa uongozi husika lakini suala langu halikupatiwa ufumbuzi," amedai Likoko.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mbali na kero hiyo, pia shina hilo limedai kusikitishwa na kauli ya baadhi ya wasimamizi ya kumkatalia Mzee Mkwepu Kaburimoja (71) kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi huo ni wa vijana na siyo wa wazee.[/FONT]

  [FONT=&quot]Akisimulia mkasa huo, mzee huyo alidai kuwa uchaguzi huo haukuwa uhuru na wa haki kwani kitendo cha kukataliwa kushiriki si cha kiungwana.[/FONT]

  [FONT=&quot]"Nilishangazwa na kauli hiyo kwani hata Rais Kikwete anafanyakazi kwa kushirikiana na wazee, hivyo kitendo cha kunikatalia kushiriki kimenisikitisha sana," amesema mzee huyo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katibu wa tawi hilo, Mohamed Mpanda, amedai kuwa ili haki hiyo iweze kupatikana hakuna budi uchaguzi huo ukarudiwa na kwamba isipiofanyika hivyo wako tayari kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vingine kuliko kuendelea kukaa katika chama hicho huku wakinyimwa haki zao.[/FONT]

  [FONT=&quot]Naye mjumbe wa shina hilo, Selemani Nkumburwa, ameomba uchaguzi huo urudiwe ili kila mmoja aweze kupata haki yake kwani wana wasiwasi kutokana kuchaguliwa mtu ambaye hawamtaki.[/FONT]

  [FONT=&quot]Pia baadhi ya wana-CCM walioongea na gazeti hili wamemuomba Rais Kikwete kumuondoa haraka iwekanavyo Katibu wa Mkoa wa CCM, Kilumbe Ng'enda, ili kukinusuru chama kisimeguke.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wamedai kuwa katibu huyo ni sehemu ya hujuma za taratibu za uchaguzi wakati yeye ndiye msimamizi mkuu wa chaguzi hizo.[/FONT]

  [FONT=&quot]"Kama chama hakitatoa uamuzo wowote, ifahamike kwamba ipo siku hili tawi letu mtakuta tumelivunnja na kuweka rangi za chama cha upinzani," amesema mwanachama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.[/FONT]

  My take: Rotten to the core, that's what ! Na kuna watu wanapendekeza hili genge liongezewe miaka mingine mitano - kaazi kweli kweli !
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa ni wezi...kuanzia kwnye Kura mpaka katika Rasilimali za Taifa...na kwa sababu wanajua mfumo wao mzima wa utendaji kazi ni kuiba then hata upatikanaji wao ni kwa Wizi...WIZI NGAZI YA TAWI, SHINA, KATA, WILAYA, MKOA hadi TAIFA. na kutukiwarudisha madarakani ndo wataiba kufidia Gharama zao...Kama Gharama ya kugombea ubunge ni Mil. 100 then watauwa wanawaza watazirudisha vp mara baada ya kuchaguliwa kuwa wabunge au mawaziri.....

  This time NEC itakaa miezi miwili kuhukumu kesi nyingi zilizopatikana katika Kura za maoni...... WEZI WAKUBWA WA NCHI HII NI CCM
   
Loading...