Chungurumbira
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,170
- 571
Kuna uwezekano kuwa imetokea na si makosa ya FJ, labda kutokujua, kuna siku binti alikuwa anakwenda Mbeya alfajiri, nilimsindikiza hadi JNIA nikamwelekeza vizuri kuwa apange foleni ya kwenda Mbeya na akisha-check in anipigie simu ili nami niondoke kuelekea kazini
Basi nimesubiri hakuna kitu, kuchungulia nikakuta binti yupo kwenye foleni ya kwenda Mwanza wakati huo Mbeya karibu wanafunga gate, ikabidi nimwombe jamaa akamwambie ndo ikawa salama yake vinginevyo angeishia kulalamika kaonewa.
Mhhh hawa jamaa ni wahuni sana last week, mwanza to dar reporting time saa 6:05 am tumefika 6:10 am tukakuta check in tayari ndege badala ya kuondoka 8:05 am tukandoka 7:05 am nahisi kuna watu waliachwa wasio enda na muda
kama ni kutalii wewe nunua wese tu,shing ngapi bana tukazunguke zunguke serengeti..!!
mwanangu hii ni zaidi ya daladalatueleweshane mkuu apo kwenye 95,500 ni bei ya kukodi au mnakuwa na abiria wengine?
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), imeitaka Menejimenti ya Shirika la Ndege la Fastjet kuorodhesha na kuwasilisha katika mamlaka hiyo majina ya mawakala wake, wanaoruhusiwa kuuza tiketi za shirika hilo kwa wateja wake tofauti na ilivyo sasa ambapo kila mtu ana uwezo wa kuuza tiketi hizo kwa wateja wao kwa bei isiyoeleweka, FikraPevu imejulishwa.
Agizo hilo la TCAA kwa kampuni hiyo ya Fastjet, limetolewa na Mkuu wa Ukaguzi wa Usafiri wa Anga katika mamlaka hiyo, Daniel Malanga kutokana na madai ya kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wateja wa sekta hiyo ya usafiri wa anga juu ya mawakala wa teketi wa kampuni hiyo kutoeleweka vyema kwa wateja wao.
Kwa mujibu wa TCAA, bei za tiketi za usafiri wa ndege za kampuni hiyo zimekuwa hazieleweki kwa wateja wake hata kwa mamlaka hiyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usafiri wa anga, lakini pia hali inayowachanganya wateja wa kampuni hiyo.
Soma zaidi FikraPevu kwa muda mrefu sasa imekuwa ikipokea malalamiko..
mwanangu hii ni zaidi ya daladala
tunataka haya mambo yawe ya kawaida sana...lakini tcaa wanatumaindi.
We kama unakwenda mwanza au iringa au kigoma sema tupange muda.
Una bahati sana! siyo hawa FAstjet! wakati wanaanza walikuwa wanabembeleza wateja sana ila siku hizi sheria kali na nyingi ni kuongeza kipato zaidi! Unafika pale check in 40mns kabla ya ndege kuondoka unaambiwa umechelewa!
Angalia wamebadili hata muda wa kubuku tiketi na kulipia! Kwa sasa ni ndani ya dkk 20 tu !
Kama mnaweza kujustify hiyo scenario, wasiliana na TCAA-CCC. Ofisi zao ziko PPF tower, hawa ndo wanahusika moja kwa moja na kumlinda mlaji wa huduma za anga. Otherwise poleni sana wakuu.
Wewe ni mwongo.Haiwezekani mtu akiwa kwenye foleni akaambiwa muda umeisha.
What if check in Clerk alikuwa too slow katika kazi yake?
Hilo unalolisema halipo.As long as upo kwenye mstari, au umeikuta foleni ni lazima ucheck in.
Usitake kutufanya wote humu wajinga.
Alikuwa bado ndani ya muda kama dk tano hivi. Kwa upande wangu wananichosha kupora watu Perfume zao hata kama umeweka kwenye begi inayolipiwa na kupakiwa na wao. Mchezo huu upo sana mwanza jamaa wanakomaa kichizi eti hairuhusiwi, naamini ndani ya muda mfupi watafungua duka maana wanaiba kweli.
we nipe kilo 2 tutapata ya kidebe yatatutosha masaa 8 anganimi mgeni mambo haya, wese kama la bei gani ?
Naaum yale yalee..''which lead to''....wakasema kupelekea...kabaaatiiEbu lindeni lugha jamani! Kuna MLAJI WA HUDUMA ZA ANGA? Nani anaweza kula huduma za anga? Kwanini usiseme mtuamiaji wa huduma za anga?
Nao bei zao si rafiki,Dawa yao ndogo sana.
Onyesheni uzalendo kwenye ndege yenu ya Precision Air. Mbona imesharudi hewani na inafanya kazi vizuri tu
MIkampuni kama hii iko radhi kuhonga mamilioni kwa wenye dhamana ili tu,Air Tanzania isifufuke.Haya matatizo ya hii kampuni sijui yataisha lini kwamaana kuna haya pia........
we nipe kilo 2 tutapata ya kidebe yatatutosha masaa 8 angani