WIZI wa dhahabu

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
Habari

Poleni na shughuli za kulijenga and kulikomboa Taifa la Tanzania kutoka katika
mikono isiyo salama. Kuna tatizo ambalo nimeliona majuzi wakati nikiwa katika
shughli zangu za utafiti wa madini katika mkoa wa Shinyanga wilayani Bukombe.
Kwa kifupi ni hivi, kampuni ya utafiti ya Tancan mining ambayo ina leseni ya
utafiti katika msitu wa kigosi imeanza kuchimba dhahabu kimya kimya kwa
kushirikiana na mafisadi wazoefu katika nchi hii. Wanaotajwa katika scandal hii
ni Joseph Kaham na Jim Sinclair Founder and Owner. taarifa zisizo rasmi zinasema Joseph Kaham huwa anaenda kuchukua mzigo (dhahabu) kwa siri kutoka Bukombe nyakati za usiku.

Maswali ya kujiuliza ni je lini serikali imetangaza kuwa Tanzania ina mgodi
mwingine hata kama ni mdogo kiasi gani unazalisha dhahabu? Na ilikuwaje mpaka
Joseph Kahama either mara zote au siku moja moja awe ndio mbebaji wa hiyo dhahabu
kuitoa msituni?

Yawezekana taarifa mnazo kuwa hicho kitu kipo kinaendelea na mnakifanyia kazi,
ila kama bado hamjapata taarifa rasmi itakuwa vizuri kuwasiliana na mbunge wa
Chadema Bukombe ili apate taarifa sahihi. Yangu ni hayo tu yaliyonikera sana
kama ambavyo wananchi wachache nilioongea nao wanavyokerwa na wizi huo wa wazi.
Wenu mwanaharakati katika kulikomboa Taifa.
 
Back
Top Bottom