duh, najihisi kutafuta mume wa kunisaidia mambo haya, maana hadi nyumba yangu inaisha ntakuwa nimenyonywa mpaka basi.
duh, najihisi kutafuta mume wa kunisaidia mambo haya, maana hadi nyumba yangu inaisha ntakuwa nimenyonywa mpaka basi.
Ni vizuri kupeana uzoefu hata kama ni mdogo hasa kwa mambo mabaya yanayoendelea ktk jamii yetu. Mpendwa kama unakwenda kununua mbao a.k.a treated timber hasa Buguruni na kwingineko weka akili sawa. Kuna wizi kiasi cha kukatisha tamaa. Ukiweza nenda na futi kamba yako,na ikibidi hata calculator,futi zinapopimwa na kusomwa na wewe andika,maeneo wanayopenda kuwaliza watu ni haya yafuatayo.
Moja, watakwambia mita moja(kwa sasa) ni Tsh 1600/ kwa hiyo kwa hesabu za haraka utasema futi ni 1600/3 badala ya Tsh 1600/3.3 kwa hiyo kama ni mbao nyingi hiyo 0.3 ni hela nyingi sana umeibiwa.
pili, zile futi zao wamekata pale ktkt kipande cha kati ya futi moja mpaka mbili na kukiondoa, kama hujashituka kila ubao (one pc) utakuwa umeibiwa hizo futi. Ukifika wanakupa futi kagua, kisha watazunguka zunguka mpaka wakubadirishie futi.
Tatu, wanapotaja futi na point zake,wanaongeza ktk kuandika zile point,kama huandiki wewe,basi utaibiwa hadi basi.
Nne, eneo la kujumlisha ni hatari pia, watakupeleka speed kwa lengo maalum.
Kwa upande wa mabati, kuna wahuni wanachanganya gauges, juu wanaweka 30 na ndani wanaweka 32.
Kama unataka kununua vifaa hivyo, basi usiwe na haraka kabisa.
Mkulu.. wamekuchekecha na uzoefu wako wote...?:evil:
Nimekoswa koswa kwa ncha ya sindano, ile nafika tu,nakuta kisanga cha kufa mtu, mjeshi mmoja karudi na mbao zote na wajuba na fundi wake. Palikuwa padogo mkuu. Kingine ninachofanya mara nyingi, ni kufanya survey kwanza, ndio nikayaona haya ya soko la dunia.
Vifaa vyangu nanunulia Yemen enter/Wahenga, ni warasimu lakini walau unapata genuin.

Asante mkuu kwa taarifa.nilishajiuliza sana kwa nini mibongo inapenda utapelitapeli tu sipati jibu
Mara ya mwisho wakikuingiza chaka nijuze.. nina kikosi kazi Tandale kwa mtogole.. mabaka cha mtoto(jk)...!!!:evil:
Mkuu hiyo kwenye red wako wapi hao mkuu maana nami najiandaa kuanza ujenzi.
Ukitaka mbao za dawa kabisa nenda pale sao hill wana mbao nzuri za dawa au mtafute agent wao mbezi beach Enea hardware simu 0784207307