Wizi wa bodaboda watikisa Kilimanjaro

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Wizi wa pikipiki zinazosafirishwa kwenda kuuzwa nchi jirani umeutikisa Mkoa wa Kilimanjaro.

Wizi huo umekithiri zaidi katika wilaya za Moshi na Rombo pamoja na Mji wa Mirerani.

Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaji Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK) kinakadiria wastani wa pikipiki 100 huibwa kila mwaka, huku baadhi ya matukio ya uporaji yakiambatana na madereva kupigwa nondo, kunyongwa kwa waya au kuumizwa.

Hata hivyo, madereva wanakinyooshea kidole kitengo cha Intelijensia cha Jeshi la Polisi chini ya ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoa (RCO) kuwa kimeshindwa kuwajibika ipasavyo kuwabaini watu wanaojihusisha na matukio hayo.

Taarifa zinasema pikipiki nyingi za wizi huvalishwa namba zilizobanduliwa kwenye pikipiki za jijini Arusha na miji mingine, nyingine zinaendelea kuendeshwa zikiwa na namba zake halisi.

Uchunguzi unaonyesha zipo pikipiki zinatembea barabarani zikiwa hazina namba, huku baadhi ya wanaoitwa bodaboda wakiwa sio madereva halisi, bali wahalifu waliojificha katika mwavuli wa bodaboda ili kupora simu na mabegi.

Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa umebaini pikipiki aina ya Boxer zinazoibwa Kilimanjaro huuzwa Mirerani na Kenya, huku pikipiki aina ya Fekon zikiuzwa zaidi Rombo na maeneo yenye milima.

Siri yafichuka

Dereva bodaboda, Charles Mboya alisema kwa sasa hali ni mbaya, hasa kwa wenye pikipiki zenye hali nzuri, kwani kipo kikundi cha wahalifu huweza hata kufanya mauaji.

“Hii miezi imekuwa too much (imezidi), ni lazima polisi watumie intelijensia yao kuubaini huo mtandao na huu utaratibu mtu mnaenda kituoni kufungua jalada mnaandikiwa kujeruhi sio sawa. Huu ni wizi wa kutumia silaha,” alisema Charles.

Mwenyekiti wa CWBK, Bahati Nyakiraria alisema inavyoonekana kuna kikundi mahsusi kwa ajili ya kupora pikipiki maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro.

“Kuna kikundi kinafanya wizi wa pikipiki kwenye baa, maduka au hospitali. Kati ya mwaka 2017/18 na 2018/19 zaidi ya pikipiki 300 zimeibwa na soko kubwa ni Rombo na wanazinunua kwa ajili ya kuvushia magendo mpakani,” anasema.

“Ukiibiwa pikipiki Moshi sasa hivi wewe kimbilia Rombo au Mirerani. Hayo maeneo mawili ndio wanunuzi wakubwa wa pikipiki,” alifafanua mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa Madereva Bajaji na Bodaboda Wilaya ya Moshi, Hamad Bendera alisema wizi wa pikipiki kwa sasa ni changamoto kubwa na matukio yamekuwa mengi sana, ambapo waendesha bodaboda wanaumizwa na wengine kuuawa.

“Kuna mtandao ambao hatuufahamu lakini majibu tunayo. Kwa wiki mbili zilizopita, pikipiki saba zimeibwa. Juzi kuna kijana ameuawa, kabla yake kuna kijana aliporwa pikipiki. Matukio ya uporaji ni mengi,” alisema Bendera.

RPC afichua mbinu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema jeshi linaendelea kufuatilia matukio kwa kukusanya taarifa kutoka kwa wakuu wa vituo vya wilaya.

“Pamoja na elimu tunayoendelea kuitoa kwenye vijiwe vyao, waendelee kuchukua tahadhari pindi wanapokodiwa. Wasikubali kwenda njia ambayo hawana uhakika nayo. Wakiamua kwenda, watumie weledi mdogo kumpiga picha mteja kwa kutumia simu wanayetaka kumbeba na kuwaachia wenzake picha hapo kijiweni,” alisisitiza.

Kamanda huyo amewataka madereva bodaboda wanapobeba wateja wawili au watatu waanze kwanza kutilia mashaka vibegi wanavyokuwa wamebeba mgongoni, kwani mara nyingi huwa na zana hatarishi kama nyundo, kamba au nyaya zinazotumika kufanikisha uhalifu.

Umakini huo amesema utawasaidia madereva hao kujiepusha na uvamizi wanaoweza kufanyiwa hivyo kuokoa maisha yao.

Mwananchi
 
Asubuhi mmeleta uzi kuwa Moshi na Rombo Ni wakarimu au hao wezi Ni wazaliwa wa Chatooo.Mnatuchanganya jamani
 
Hii barabara ya kutoka kibosho road kwenda shirimatunda eneo la kwa boi safi ndo pa hovyo kuna vibaka wa kutisha sijui polisi mnasubiri nin kuja kuwabeba kila siku mtu anaibiwa boda hapa
 
Back
Top Bottom