DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Naandika hivi kwa masikitiko makubwa kwa kile kilichonitokea na ambacho nimekiona kabla pale Posta Mpya, Dar es Salaam.
Kwanza kila unapotuma mzigo, wanakwambia ukanunue tape kwenye duka moja pembeni na wanasisitiza lazima boksi zima lizungushiwe tape kitu ambacho hakina mantiki yoyote. Kuna hela nyingi inatengenezwa pale kwa jambo hilo tu.
Sasa leo ndiyo wameniweza kabisa. Nimeenda na vimizigo vyangu kutuma vikapu Marekani, baada ya kukaa siku nzima pale wakinizungusha mara hili na lile, mwisho wa siku wananiambia kila boksi la kilo 30 ni shillingi 600,000 na zaidi kutuma Marekani kama gharama za shipping wakati hapo kabla mizigo kama hiyo ilikuwa haizidi 40,000 kwa boksi. Hapo tayari nimeshaingia gharama za usafiri ambapo nimekaa na dereva siku nzima.
Nimerudi na mizigo yangu nikitafakari la kufanya ila kwa mtindo huu, sijui kama tutafika Watanzania wenzangu.
Kama wahusika wanadhani wamenikomoa, nawaambia wajitafakari tena. Maisha hayaendi hivyo kwa kuishi na uonevu, chuki na wivu usio na kichwa wala mguu.
Kama kuna mwenye ushauri, nipo tayari kuupokea.