Wizi unafanywa na TAXIFY

Wizi unafanywa na TAXIFY

x-factor

Senior Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
181
Reaction score
212
Habar za wakati wana jamvi.

Ninapenda kushare nanyi malalamiko ya watu wengi kuhusu Taxify na madereva wao kwa wizi wanaowafanyia watumia huduma.

Tukianza na Taxify wenyenye
Juzi nimesafir KM 7 kwa dk 13 na price ilikuwa 4000tsh
Nikachajiwa 10,000tsh safari ilikuwa ni ya kwenda. Cha ajabu kwenye risit inaonyesha nimetembea km 22 na ni sehem ambayo kila siku nasafir kwenda uko.
Wakati na rudi nimechajiwa sh 9000tsh kwa distance hiyo hiyo ya km 7 huku risit yao inaonyesha km 18.
Ni hii sio mara ya kwanza kutokea overcharging
Nikajirubu kupata mawasiliano yao kwa njia ya email
Wakanijibu ni GPS problem, nikawauliza kama hili tatizo mnalijua maana imekuwa hili ndo jibu lenu kila shida hii ikitokea mmechukua hatua gani lisitokee tena, nikapewa majibu mengine mepesi, ila wakaniambia wamesolve, nikasafir baada ya siku mbili KM 2 wakanichage 6000tsh na kunipa risit ya km 12. Nilienda offisin kwao nikakitana na dada mmoja akanijibu kirahis kwamba sim ya dereva ilikuwa ina shida ya GPS
My take kama mtanzania mmoja naweza kuibiwa sh 5000 kwa safari moja ni watanzania wangapi wengine wanaibiwa?

Jinsi madereva wa taxify wanavyoiba.
Kuna njia mbili ambazo nimezibain kutokana na experience yangu na huu usafir..
Ya kwanza, ukifika destination yako anakuonyesha screenshot ya bei kubwa kama una haraka unalipa af unaondoka af anaendelea na trip ya uber so distances inaendelea kusoma ilk baadae aki end bei iwe sawa au ikaribiane na aliyokucharge.

Pili inatokea sana ukifanya request kwajili ya mtu akifika anamwonyesha bei, af end trip kama amepata abiria wa uber anaendeleanae anakuja ku end baadae...

Pia kama kuna mtu mwenye utaalam wa sheria ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa na wizi wa aina hii ili kuwatetea watanzania wanaoibiwa.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi imetokea mara mbili,Mara ya ni sehemu ya Km 8 ,Ikasoma 17 nikachajiwa 8000 badala ya 5000.Mara ya pili sehemu ya Km 10 ikasoma 42Km Nikachajiwa 16000 ,Kiukweli hapo niliumia sana nikaondoaa hiyo application kwenye simu yabngu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa taarifa mkuu. Kiukwel kwa upande wa teknolojia watz wanapigwa sana na hakuna pa kusemea. Ili mtu usionekane mshamba unashindwa kulalamika au kudai. Hiyo ni moja wapo ya vizi, kuna sehemu nyingi sana wana utapeli au wizi wa aina hiyo.

Sent using smatskills group on telegram
 
Mkuu hii ni kweli kabisa

Bolt zaman taxfy ni wezi kinomaa...

Nilitoka mkoa nikashuka tangi bovu pale nikachukua uber hadi nyumban nikalipa sh elf tisa mia tano...
Week mbili baadae nikasafiri tena na kushuka pale pale tangi bovu nikachukua usafiri wa bolt mpaka nyumban,njia ile ile umbali ule ule nikachajiwa shi elf ishirini na tatu...nilishangaa sana,

Kuna kitu wanakiita surge bei huwa zinabadilika lakini sio kwa kiwango hicho.

Surge inatokea pale ambapo gari zipo chache na wahitaji ni wengi,mfano juz game ya stars gari nyingi hazikuingia mzigoni ndio surge hutokea kutokana na uhitaji wa watu kuwa mkubwa kuliko gari zilizopo lakini hata hvyo bado sio kwa gap hilo la bei.

Bolt ni wezi mnoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kuoneshwa screenshot ya safari za watu wengine kuweni making.
 
Habar za wakati wana jamvi.

Ninapenda kushare nanyi malalamiko ya watu wengi kuhusu Taxify na madereva wao kwa wizi wanaowafanyia watumia huduma.

Tukianza na Taxify wenyenye
Juzi nimesafir KM 7 kwa dk 13 na price ilikuwa 4000tsh
Nikachajiwa 10,000tsh safari ilikuwa ni ya kwenda. Cha ajabu kwenye risit inaonyesha nimetembea km 22 na ni sehem ambayo kila siku nasafir kwenda uko.
Wakati na rudi nimechajiwa sh 9000tsh kwa distance hiyo hiyo ya km 7 huku risit yao inaonyesha km 18.
Ni hii sio mara ya kwanza kutokea overcharging
Nikajirubu kupata mawasiliano yao kwa njia ya email
Wakanijibu ni GPS problem, nikawauliza kama hili tatizo mnalijua maana imekuwa hili ndo jibu lenu kila shida hii ikitokea mmechukua hatua gani lisitokee tena, nikapewa majibu mengine mepesi, ila wakaniambia wamesolve, nikasafir baada ya siku mbili KM 2 wakanichage 6000tsh na kunipa risit ya km 12. Nilienda offisin kwao nikakitana na dada mmoja akanijibu kirahis kwamba sim ya dereva ilikuwa ina shida ya GPS
My take kama mtanzania mmoja naweza kuibiwa sh 5000 kwa safari moja ni watanzania wangapi wengine wanaibiwa?

Jinsi madereva wa taxify wanavyoiba.
Kuna njia mbili ambazo nimezibain kutokana na experience yangu na huu usafir..
Ya kwanza, ukifika destination yako anakuonyesha screenshot ya bei kubwa kama una haraka unalipa af unaondoka af anaendelea na trip ya uber so distances inaendelea kusoma ilk baadae aki end bei iwe sawa au ikaribiane na aliyokucharge.

Pili inatokea sana ukifanya request kwajili ya mtu akifika anamwonyesha bei, af end trip kama amepata abiria wa uber anaendeleanae anakuja ku end baadae...

Pia kama kuna mtu mwenye utaalam wa sheria ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa na wizi wa aina hii ili kuwatetea watanzania wanaoibiwa.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa na majanga yote hayo bado unajipeleka tu,usikute na leo umeenda tena
 
Hilo limeshajadiliwa mara kadhaa humu.

Jamaa wanachofanya, mkishaanza safari, simu anaiweka kwenye "Ultra Power Mode" au "Low Battery Mode".

Mkikaribia kufika tu anairudisha vizuri, hapo akirequest balance inaonesha mmetembea kms nyingi, kwa sababu kwa kipindi ilipokuwa kwenye mode ile haiwezi kusoma njia vizuri.

Ukiomba ramani utashangaa kutoka Mwenge hadi Ubungo kupitia Sam Nujoma inaweza kukusomea maajabu, kwamba mmeenda mpaka Magomeni mkarudi Ubungo.

Hii michezo iko hadi Uber.
 
Bado tuna safari ndefu,kila mtu amekariri kuwa huwezi kufanikiwa kwenye maisha lazima uibe,hii mindset itachukua muda sana kututoka watanzania,kwani imetuchukua takriban miaka 30 kuishi ndani ya hiyo Imani...
 
Mim kuna mmoja jumamos tu, akawa ananipeleka sehem kwanza hana lugha rafiki pia alikua anatembea taratibu ili kuongeza muda plus akawa anaipitisha njia za folen ili gharama iwe juu, Mungu alivyomlaana alisahau kuwasha Data anakuja kuiwasha ile namaliza safar anajikuta ananidai elf 4 wakat nna uhakika kabisa gharama isingekua chini ya 15,000 nikamjibu utakula hyo hyo buku nne nkasepa.
 
Jamaa washenzi sana yani, weziiii!

Huwa nikitoka mihangaikoni siku ambazo nakuwa nimechoka sana huwa nakamata uber. Bei ya Uber kutoka job mpaka mtaa huwa bei ni 10,000 mpaka 12,000 tu. Umbali ni wa approximately 12.5 km

Kwa kuwa niliwahi pia kutumia Taxify kufanya comparison ya bei na mara zote ikawa inaleta bei nafuu na pia nishawatumiaga before wakawa poa kuliko Uber. Juzi kati nikajaribu kudownload upya app yao ya Bolt. Nika request trip from Clock tower to kitaani. Bei nilipewa 7000-9000 kufika mtaani nadaiwa 16000. Duh, nilishangaa sana ila ndio hivyo hela ilikuwepo nikalipa tu.

Sikujua ni nini kimefanyika ila nilihisi dereva amenihujumu tu kwa namna moja ama nyengine. Asante mtoa mada kwa kutupa tips!
 
Mimi niko hapa Mwanza. NAAPA sitatumia usafiri wa Taxify kuanzia sasa ni afadhali hiyo hela niwape waendesha taxis wa kawaida. kuliko kuwapa taxify. Mbona Uber hawana ujanja ujanja kama huu?.
 
Taxify walikuwa wanatuwin kwa kuwa bei ya makadirio inakuwa chini kuliko Uber, unajikuta unachagua cheap ila mwisho wake ndo majanga.... yamenikuta haya Mlimani City kwenda Kimara mwisho ilikuwa 4000-5000 trip inaisha nadaiwa 16000.
 
Back
Top Bottom