Chama cha madereva wa usafirishaji kwa njia ya mtandao (Toda) kimetoa siku saba kukutana na wamiliki wa kampuni za Uber na Taxify

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
546
1,000
Chama cha madereva wa usafirishaji kwa njia ya mtandao (Toda) kimetoa siku saba kukutana na wamiliki wa kampuni za huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao za Uber na Taxify ili kujadiliana kuhusu changamoto zinazowakabili madereva.

Kimesema kama itashindikana kukutana na wamiliki hao watawafungulia kesi mahakamani.

Toda imetoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa madai kuwa wamiliki hao wanachukua asilimia kubwa katika kila safari anayofanya dereva, kushusha bei za safari kila siku bila kuzingatia gharama za usafirishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 19, 2019 mwenyekiti wa Toda, Linus Chuwa amesema awali biashara hiyo ilikuwa ikivutia kampuni nyingi na kipato kilikuwa kizuri lakini kwa sasa hali ni tofauti.

“Wakati kampuni hizi zinaanza biashara nchini benki nyingi ikiwemo CRDB zilivutiwa kutoa mikopo ya magari kwa madereva ambayo walikuwa wakiilipa kwa miaka miwili lakini sasa suala hilo limekuwa gumu kutokana na bei za usafirishaji kuwa ndogo,” amesema Chuwa

Amesema wakati mwingine ni ngumu kujua dereva anavyoumia kwa kuwa kampuni hizo hazimiliki magari na baadhi ya madereva waliokopa wakishindwa kulipa madeni na magari yao kupigwa mnada.
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,828
2,000
Tatizo hayo makampuni yanaangalia sana Wateja. Hafu siku hizi yamekua utitiri na madereva siku hizi wamekua wengi sana.

Niliwashi andika uzi kuleta mrejesho baada ya kuendesha Uber na Taxify kwa muda mfupi. Nilikua nalaza hadi 150,000/= na hapo nimeanzia saa 12 usiku hadi saa 12 asubuhi.

Enzi izo hakuna usumbufu wa jiji wala plate number ata ya njano fresh.
 
cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
3,268

Mzee ulikua unavuna kabla wadau hawajashtuka.....sasa hapo sijui watamshitaki nani wakati hapa dar pana meneja tu....ila hawa jamaa uber in a way ni wanyonyaji ndo maana uingereza wamegoma kurenew licence ya uendeshaji uber nchini mwao
 
Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,225
2,000
Uber = B & B etc

"terms and conditions" wengi wetu hatusomi, ama tukishasoma tunakubali mwanzoni, tukijiaminisha huko baadae tutarekebishana,
 
TEGETA KIBAONI

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
651
225
Tatizo hayo makampuni yanaangalia sana Wateja. Hafu siku hizi yamekua utitiri na madereva siku hizi wamekua wengi sana.

Niliwashi andika uzi kuleta mrejesho baada ya kuendesha Uber na Taxify kwa muda mfupi. Nilikua nalaza hadi 150,000/= na hapo nimeanzia saa 12 usiku hadi saa 12 asubuhi.

Enzi izo hakuna usumbufu wa jiji wala plate number ata ya njano fresh.
Unamaanisha 12 Maghrib Hadi 12 alfajiri? Ilikuwaje ukaacha kazi nzuri hivyo?
 
Pelly

Member
Mar 26, 2013
55
95
yaani hiyo buku 3 ni free kabisa hata bodaboda hapakii alafu bado unawapa free yaani huyu mzungu kaja kutunyonya na kututawala kwa style nyingine kabisa, history inasema walipokuja mara ya kwanza walituletea shanga tukawapa gold leo usafiri wa bure gari si zao hii ni zaidi ya zile shanga na gololi alafu wakachukua gold na almasi, pumbavu zao kabisa uber wajipange wakizingua uncle Magu anasikia waulize accacia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom