Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,466
- 2,860
Wasalaam wandugu wapendwa,
Nimesoma kupitia vyombo vya habari kuwa vibaka/wezi wameiba mikufu ya dhahabu, fedha na laptop nyumbani kwa Mengi.
Polisi wanafanya kazi yao, ila kuna mambo kama Taifa na familia ya Tanzania tuna jukumu la kujiuliza kwa sauti na ikiwezekana kuchukua hatua za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili mambo ya wizi kama huu wakati wa msiba huko mbele yasitokee tena.
Kabla ya kutoa hoja ya nini kifanyike, pengine nije na swali;
Msiba huu ungetokea "Masaki au Oyesterbay" na wakahudhuria wakazi wa mitaa hiyo, bila shaka hata wizi usingefanyika;
Msiba huo wangehudhuria hukohuko Machame, wazee na watoto wao wa kishua, bila shaka wizi usingetokea.
Ila msiba ambao unatokea na kila mmoja anahudhuria kama zilivyo tamaduni zetu, msibani kila mmoja anakuja. Inapoteka kuna watu wana njaa, hawana tumaini la kupata fedha kwa kazi za mikono yao, na mara wanaingia kwenye kasri kama la mzee Mengi na huenda hawajawahi kuingia na wanajua mle ndani kuna "shekels", kuna vito vya thamani na laptop; ushawishi wa kuiba ni mkubwa.
Cha ajabu wanaiba sio kuhifadhi, wanaiba ila wakauze na kupata hela ya kula ili ndani ya siku 2 au 3 hana hata mia.
Iko haja kutengeneza mfumo jumuishi ambao watu wengi waweze kufanya kazi endelevu hata kama ni kukata nyasi alishe ng'ombe, kuku, kupalilia au kufyaka; cha msingi ana uhakika kuwa kila asb kuna pahala pa kutumia nguvu na akili yake kufanya kazi.
Inapotokea kuna gap kubwa sana kati ya walala hoi wengi na walala heri wachache, aibu ya uporaji kama huo haitaisha.
Serikali ni baba na mama wa Watanzania; iko haja kuja na programu na project jumuishi ili kupunguza nguvu kazi ambayo iko idle kitaa. Wengi tunafahamu, maeneo ya watu walio idle hata ukipaki gari ukazubaa hutakuta taa, mlango umevunjwa wameiba laptop au vitu vingine.
ila kuna maeneo bongo hapa hapa unaweza kupaki gari au kutembea usiku, hutaibiwa wala kukabwa. Maeneo yenye umasikini rate ya uhalifu iko juu. Hata tukiongeza vituo vya polisi bila kupunguza rate ya unemployment, tunakuwa hatujatenda haki kwetu kama watu wazima, hali kadhalika kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi, akina baba na mama wa kesho ambako taasisi za familia zinaundwa ili kuleta malezi ya watoto katika jamii ambayo kwa ujumla inajenga taifa.
Tunao wajubu wa kufanya kwa pamoja. Hatukubaliani na uhalifu hata kidogo. Ila tuna wajibu wa kudhubiti uhalifu usitokee na vitendo kama hivyo kwa kuunda mifumo endelevu ya vijana wetu kufanya kazi kwa kadri ya nguvu zao na elimu yao pia.
Jumapili njema wakuu