Wizi, Ujambazi, Ujangili, Ukibaka, Uharamia

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wakubwa shikamoo, wadogo habari zenu,
naomba kufahamishwa tofauti au maana ya maneno haya:
  1. wizi = ?
  2. ujambazi = ?
  3. ujangili = ?
  4. ukibaka = ?
  5. uharamia = ?
  6. udokozi = ?
  7. utapeli = ?
  8. ......
Tafadhari nisaidie kujua maana, hata kama unajua moja jibu tu wengine watafafanua zingine.
Je,
ni yapi katika haya ni lugha fasaha katika Lugha adhimu ya kiswahili?
 
Wakubwa shikamoo, wadogo habari zenu,
naomba kufahamishwa tofauti au maana ya maneno haya:

  1. wizi = ?
  2. ujambazi = ?
  3. ujangili = ?
  4. ukibaka = ?
  5. uharamia = ?
  6. udokozi = ?
  7. utapeli = ?
  8. ......
Tafadhari nisaidie kujua maana, hata kama unajua moja jibu tu wengine watafafanua zingine.
Je,ni yapi katika haya ni lugha fasaha katika Lugha adhimu ya kiswahili?

1. wizi = Kuchukuwa mali au kitu cha mtu bila idhini yake kwa madhumuni ya kukimiliki moja kwa moja.

2. ujambazi = Ni aina ya wizi, ila wizi huu ni wa kutumia nguvu mf: Silaha kama visu au Bunduki.

3. ujangili = Ni neno lenye asili ya Kihindi "JUNGLI" na lina maana ya Mwitu au Poli (Nao wamelitohoa kwenye kiingereza "Jungle"). Kwa lugha ya kihindi pia utumiwa kwa maana ya mtu asiye staharabika asiye na adamu mwenye tabia za kinyama. Ukisema "jungli jaanwar" Una manisha Wanyama poli (Wild Animal).
Nasi wazungumzao wa kiswahili tumeli tohoa na kulitumia kwa maana ya wezi wenye kuiba nyara za serikali (Nyama poli).

4.ukibaka = Hali ya Wizi mdogo mdogo wa majumbani au mitaani.

5. uharamia = Huu ni wizi wa kuwaibia wasafiri na haswa kwenye vyombo vya usafiri wa majini, kama vile Meli (Pirate)

6. udokozi = Huu ni wizi mdogo mdogo sana na mara nyingi wadokozi uchukuwa vitu vidogo vidogo sana. NA ndio mwanzo wa kuwa kibaka na wengine ubakia kuwa wadokozi hivyo hivyo bila ya kupanda na kuwa vibaka.

7. utapeli = Huu ni wizi wa udanganyifu na kutumia uongo kujipatia mali.
 
Back
Top Bottom