Nyetk
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,648
- 1,701
Kumezuka kamtindo kanakera kweli pale UCHUMI shoping mall ya Quality Center(Barabaa ya Nyerere) sehemu za kulipa bidhaa. Wanapokurudishia chenji wanakwambia huku wanabana pua "samahani chenji ya 'coin' sina". Hii tabia imekuwa ni mazoea yao si teller counter moja wala siyo siku moja. Sijui ni kitu gani kinachowafanya hao mabinti wadhani kuwa chenji ya mteja ni halali yao? Ndo utaratibu wa duka ua njaa ya vibinti hivyo? Kama wanataka kupokea"tips" za wateja si afadhali wakauze baa? Kwa kweli wanakera!