Tamaa yao ya hela itawafanya wasijue kama unawasumbua, kuja kushtuka ushawaharibia sikuNiliwah kuwafanyia hivo wale wanaojifanya wana nafasi za jeshi
Hii imewah kunikuta pina yangu sikua na salio kubwa walilosema wao maana wao walinambia nimepokea laki5 na Mimi sikuwa na hyo ela wakaumbuka
Utatapeliwaje kizembe na mbinu za mwaka 70 wewe usiwe kama mwanaume wa dar
HahaaaNa wanaoibiwa kihivyo ni wamikoani
Sio kwamba sikua na pesa kabisaa ilikuepo ila si laki5unaakaje bila akiba ?
4HM7SRKH Imethibitishwa. Umepokea Tsh485,000.00 kutoka 255752623855 - LIVING LEKULE mnamo 5/5/18 saa12:16 PM Baki yako ya M-Pesa ni Tsh1,035,320.00.
Huu ni wizi mpya...wanakupigia wanakuambia wamekutumia hela kimakosa,
1. wanakuuliza umeona msg, unawaambia hapana..
2. Wanakuuliza kwani ulikuwa na salio la sh. Ngapi...unawatajia ..let say 550,000/=
3. Wanadraft msg ...Kama hiyo.. umepokea Tsh.485,000/= kwenye M-pesa yako ,salio lako ni 1,035,320/=
4. Wanakupigia tena wanakuambia umeona msg, unasema Ndio , wanakuambia ukate elfu 10 ya usumbufu ubaki nazo na hiyo nyingine watumie.
5. Inakula kwako
Nawasilisha.
we janjaro chalee ya mamtoniSio mimi
Wanasema mbinu za kizamani wakati watu wanapigwaWalinipigia wiki mbili zilizopita, jamaa akajitambulisha kuwa ni customer care wa vodacom, akaniuliza kuwa "kuna pesa umepokea sasa hivi?" Nikamwambia sijui....
Akaniuliza "kwani mara ya mwisho kutuma au kupokea pesa ni lini?" Nikamjibu "niliacha kutumia miamala ya fedha kwa simu mwaka wa tatu sasa".
Jamaa akakomaa "hebu angalia salio kuna hela umetumiwa kimakosa!"
Nikamwambia "mpumbavu wewe.....wewe si customer care wa voda hamisheni wenyewe hiyo pesa."
Akakata simu...