Nataka kukuhakikishia kwamba dira uliyofungiwa haijachakachuliwa tatizo liko kwenye usomaji wa dira na kiukweli matumizi ya lita 2,000 kwa siku yaani ndoo 100 za lita 20 ni makubwa mno na hayawezi kuwa justified!
Pole sana ndugu
Mwaka jana mwezi june nilideposit laki moja Dawasco.Nilifanya hivyo kwa vile mimi mwenyewe siishi hapo, kuna kijana tu anayeishi hapo kama mlinzi.Na bill iliyokuwa inakuja sio zaidi ya sh. elfu nne kwa mwezi.Ajabu mwezi oktoba nikapewa taarifa kuwa nadaiwa sh.elfu sabini na tisa,hapo ukizingatia mwezi August na Sept maji hayakutoka.Nilipokwenda kuwalalamikia wakadai hawana kumbukumbu,nikawaonyesha zile lisiti bado wakawa wanaleta ubishi,wanalazimisha nilipe kwanza hilo deni.Kwakweli mamlaka za maji mjini ni shida tupu!
Mwaka jana mwezi june nilideposit laki moja Dawasco.Nilifanya hivyo kwa vile mimi mwenyewe siishi hapo, kuna kijana tu anayeishi hapo kama mlinzi.Na bill iliyokuwa inakuja sio zaidi ya sh. elfu nne kwa mwezi.Ajabu mwezi oktoba nikapewa taarifa kuwa nadaiwa sh.elfu sabini na tisa,hapo ukizingatia mwezi August na Sept maji hayakutoka.Nilipokwenda kuwalalamikia wakadai hawana kumbukumbu,nikawaonyesha zile lisiti bado wakawa wanaleta ubishi,wanalazimisha nilipe kwanza hilo deni.Kwakweli mamlaka za maji mjini ni shida tupu!
Kwanza wakuu najua kabisa "thread" hii ilipaswa iwekwe kwenye jukwaa la sheria, lakini kwa vile wadau wengi wanakuwa kwenye jukwaa la siasa na jukwaa la habari na hoja mchanganyiko imenibidi niirushe huku labda nitapata msaada wa haraka.
Ndugu wataalam wa sheria naomba mnisaidie.
Nimekuwa nikiletewa ankara za maji ambazo ni wazi kabisa kuwa zimekaa kiwizi wizi vile. Kila nikienda kulalamika wananiambia hayo ndiyo matumizi yangu nikiwaomba waje waangalie dira yao huenda ni mbovu hawataki.
Matumizi yenyewe yale ya ndani tu eti inafikia lita karibia 2,000 kwa siku (yaani mapipa 10), nimewalilia sana na kuwaambia niefanya audit kwenye mfumo mzima wa maji pale nyumbani kwangu hakuna bomba linaliovujisha maji inakuwaje ankara kila kukicha inapanda tu? Sijapata msaada wowote kutoka kwa hawa wataalam wetu ambao ndo tunawategemea maana siyo wote tumesomea mambo ya maji. Nilichoamua kukifanya napanga kununua tanki la lita 1,000 ili nilijaze chini ya usimamizi wangu mwenyewe nione dira yao itasoma lita ngapi hadi litakapojaa.
Sasa nikiona hiyo dira inasoma lita 2,000 na huku ilipaswa kusoma lita 1,000 (kitu ambacho nahisi hawa jamaa kabla ya kuzigawa hizo dira kwa wateja huwa wanazichakachua), kuna sheria yoyote itakayonisaidia kuishitaki mamlaka ya maji safi (kama yapo) na maji taka mjini kwetu?
Naomba msaada wenu wakuu!!!!!
Yes utakuwa na kesi. Kwanza kuna negligence hapo under tort law. Wakulipe fidia. Nikukutajia nyingine itabidi unilipe...
kwa heri na kila la kheri. hope utafanikiwa kusuluhisha hilo jambo.
Ndugu yangu usibanie ujuzi!!
Kama unafahamu sheria nisaidie mwezenu, ndo maana nimesema kama kuna sheria itakayonisaidia kuwakomesha hawa wezi wa mchana! Na hilo litakuwa fundisho kwa mamalaka zingine, maana najua wananchi wengi tu wanaibiwa kwa mtindo huu. Unajua hawa jamaa wana ki-utaratibu fulani hivi cha kulipana bonus kunapokuwa na makusanyo mengi ndo maana hawa jamaa wa ufundi hapo kwenye mamlaka za maji wanatuchezea mchezo mchafu ili wapate bonus.
Nisaidie ndugu tuwakomeshe, ili hizo wanazolipana bonus ziwatokee puani.
hahahaaa jela inanukia upande wangu loolAsante kwa ushauri wako! Nitaufanyia kazi. Sasa si uni-PM kama unawafahamu hao jamaa watakaonisaidia kuichakachua hiyo mita, nami nitakuja nikufuate kama ulivyosema?
hahahaaa jela inanukia upande wangu lool
Sikulipa, walidai wangekuja kuangalia mita kama ni mbovu au la.Lakini hawakufanya hivyo hadi leo.Ulilipa? Mbona waTz tunageuzwa kuwa wajinga kiasi hicho?