Wizi Mkubwa Tunaofanyiwa na Mamlaka za Maji Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi Mkubwa Tunaofanyiwa na Mamlaka za Maji Mjini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Job K, Jun 30, 2011.

 1. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Kwanza wakuu najua kabisa "thread" hii ilipaswa iwekwe kwenye jukwaa la sheria, lakini kwa vile wadau wengi wanakuwa kwenye jukwaa la siasa na jukwaa la habari na hoja mchanganyiko imenibidi niirushe huku labda nitapata msaada wa haraka.

  Ndugu wataalam wa sheria naomba mnisaidie.

  Nimekuwa nikiletewa ankara za maji ambazo ni wazi kabisa kuwa zimekaa kiwizi wizi vile. Kila nikienda kulalamika wananiambia hayo ndiyo matumizi yangu nikiwaomba waje waangalie dira yao huenda ni mbovu hawataki.

  Matumizi yenyewe yale ya ndani tu eti inafikia lita karibia 2,000 kwa siku (yaani mapipa 10), nimewalilia sana na kuwaambia niefanya audit kwenye mfumo mzima wa maji pale nyumbani kwangu hakuna bomba linaliovujisha maji inakuwaje ankara kila kukicha inapanda tu? Sijapata msaada wowote kutoka kwa hawa wataalam wetu ambao ndo tunawategemea maana siyo wote tumesomea mambo ya maji. Nilichoamua kukifanya napanga kununua tanki la lita 1,000 ili nilijaze chini ya usimamizi wangu mwenyewe nione dira yao itasoma lita ngapi hadi litakapojaa.

  Sasa nikiona hiyo dira inasoma lita 2,000 na huku ilipaswa kusoma lita 1,000 (kitu ambacho nahisi hawa jamaa kabla ya kuzigawa hizo dira kwa wateja huwa wanazichakachua), kuna sheria yoyote itakayonisaidia kuishitaki mamlaka ya maji safi (kama yapo) na maji taka mjini kwetu?

  Naomba msaada wenu wakuu!!!!! ​
   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndugu jambo la muhimu kama ulivyosema ni kuhakikisha kama matumizi wanayokubill yanafanana na dira ilivyosoma kwa mwezi na kama dira inasoma matumizi makubwa basi itakuwa vyema kama utafanya zoezi ulilolisema.

  Nashauri urecord meter reading siku msoma mita atakapokuja ili akija kusoma mwezi mwingine pia urekodi naye ili kuwa na uhakika kama reading zitakazowekwa ni sahihi.

  Nataka kukuhakikishia kwamba dira uliyofungiwa haijachakachuliwa tatizo liko kwenye usomaji wa dira na kiukweli matumizi ya lita 2,000 kwa siku yaani ndoo 100 za lita 20 ni makubwa mno na hayawezi kuwa justified!

  Pole sana ndugu
   
 3. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mzee unalo sema laweza kuwa kweli kuwa jamaa wanakuchezea mchezo mchafu......swali je ni kwa manufaa ya nani? ya mamlaka ya maji au mtu binafsi.............?

  Mi naomba nikwambie kitu kimoja...bili yangu ya maji mwaka fulani ilikuwa inakuja kubwa sana nikawa nawafata hawa jamaa wakawa wananizingua ...baadae sana baada ya majirani kusikia kilio changu walinitonya kuwa kuna masela furani wanafanya biashara ya kutengeneza na kuuza matofali walikuwa wanaiba maji through bomba langu.....so jaribu kufatiria bomba lako
   
 4. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu kwa ushauri!!

  Kwa kweli huwezi kupata justification ya lita 2000 kwa siku, pamoja na kwamba hao jamaa wananizingua tu lakini ukweli nitaupata tu na siku hiyo patakuwa hapatoshi. Maana wamekuwa wajinga sana hawa jamaa, huduma zenyewe mbovu kama nini sijui!!
   
 5. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  nakushauri tafta mtu aichokonoe mita kama hawataki kukuelewa make nji hii inabidi sometimes uwe kichaa kidogo ndo utaeleweka
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  i mean wanamwaga mboga we mwaga ugali.na ukishafanya hivyo unifwate
   
 7. T

  Teko JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mwaka jana mwezi june nilideposit laki moja Dawasco.Nilifanya hivyo kwa vile mimi mwenyewe siishi hapo, kuna kijana tu anayeishi hapo kama mlinzi.Na bill iliyokuwa inakuja sio zaidi ya sh. elfu nne kwa mwezi.Ajabu mwezi oktoba nikapewa taarifa kuwa nadaiwa sh.elfu sabini na tisa,hapo ukizingatia mwezi August na Sept maji hayakutoka.Nilipokwenda kuwalalamikia wakadai hawana kumbukumbu,nikawaonyesha zile lisiti bado wakawa wanaleta ubishi,wanalazimisha nilipe kwanza hilo deni.Kwakweli mamlaka za maji mjini ni shida tupu!
   
 8. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Yaani hawa jamaa wanakera kuliko maelezo!

  Ukiwa na vithibitisho vyote wanabaki wanakulazimisha tu uwalipe pamoja na kwamba vielelezo vyote vitakuwa vinaonesha wizi wao. Nilienda siku moja kulalamika wale watu wa huduma kwa wateja wakaona kweli kuna wizi nimefanyiwa, lakini wakashindwa kupunguza hilo deni hivyo wakanielekeza kwa meneja wa huduma kwa wateja (nikakuta eti engineer uchwala ndo meneja wa huduma kwa wateja) hakunielewa maana yeye anataka tu makusanyo bila kujali ubora wa huduma. Huko tulifika mpaka kutukanana, anatishia na degree yake ya engineering (ulishaona wapi?) Nikamwambia huko huko, maana hunijui na mimi wala sikujui hapa nimefuata huduma tu, ilikuwa balaa siku hiyo.

  Kuna ushauri nimepewa na dada Flora kwamba wao wamemwaga mboga nami nimwage ugali nafikiria kufanya hivyo lakini kwanza nione kama naweza kuwashitaki kwenye vyombo ya sheria.

  Nikikosa msaada wa kisheria itabidi nifanye kweli!!
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ulilipa? Mbona waTz tunageuzwa kuwa wajinga kiasi hicho?
   
 10. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ushauri wako! Nitaufanyia kazi. Sasa si uni-PM kama unawafahamu hao jamaa watakaonisaidia kuichakachua hiyo mita, nami nitakuja nikufuate kama ulivyosema?
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yes utakuwa na kesi. Kwanza kuna negligence hapo under tort law. Wakulipe fidia. Nikukutajia nyingine itabidi unilipe...
  kwa heri na kila la kheri. hope utafanikiwa kusuluhisha hilo jambo.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Now this is really serious,
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu usibanie ujuzi!!

  Kama unafahamu sheria nisaidie mwezenu, ndo maana nimesema kama kuna sheria itakayonisaidia kuwakomesha hawa wezi wa mchana! Na hilo litakuwa fundisho kwa mamalaka zingine, maana najua wananchi wengi tu wanaibiwa kwa mtindo huu. Unajua hawa jamaa wana ki-utaratibu fulani hivi cha kulipana bonus kunapokuwa na makusanyo mengi ndo maana hawa jamaa wa ufundi hapo kwenye mamlaka za maji wanatuchezea mchezo mchafu ili wapate bonus.

  Nisaidie ndugu tuwakomeshe, ili hizo wanazolipana bonus ziwatokee puani.
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Okay mkuu. Tutaongea kwenye PM.
   
 15. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  hahahaaa jela inanukia upande wangu lool
   
 16. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Wala hakuna jela hapo ndugu usihofu, ni katika harakati za kujinasua na hawa wezi wasiokuwa na hatia hawa!

  Watu wamekalia kulipana bonus tu kumbe ni zile hela wanazotuibia?!! Yaani nitaichakachua hiyo mita yao mpaka iwe inasoma zero, wajinga sana hawa.
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  ya kwet ya tanesco tuliichakachua baada ya kuletewa bill ya milion tatu wkt hatujawah hata cku moja kuchelewesha bill wakatuzungushaweeee wakataka laki na nusu ili warekebishe bi mkubwa kawapa then nayeye kasaka kishoka tukaiba weee mpaka sasa kaamua kuirekebisha baada ya mapene yake kurudi! nji hii jino kwa meno halaaa wao wale kwa raha af sisi tpate shida kwaninoi?
   
 18. T

  Teko JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Sikulipa, walidai wangekuja kuangalia mita kama ni mbovu au la.Lakini hawakufanya hivyo hadi leo.
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  wanajua makosa yao vilaza haoooo na ndo mana wanaleta ukenge wao nyakuzi wakubwa saaana
   
Loading...