Wizi makazini umaskini unachangia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi makazini umaskini unachangia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babu Ubwete, Jul 19, 2009.

 1. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna wimbi kubwa la wizi katika kampuni za mjini Vodacom,Barclays, Stanbic,Tigo etc ambazo nyingi zimeajiri vijana waliosoma walau first degree. Swali kwanini wizi huu umeibuka nyakati hizi kijana kamaliza tu mzumbe au udsm kapewa kazi ya uhasibu unasikia kaiba million 700, kuna mtu baclays kapiga billion 3. Tatizo ni nini?
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kushuka ama kupotea kwa maadili ya Taifa. Na pia hatujawa makini katika kushughulikia wizi, ufisadi na kila baya. Manake kila fisadi ama mwizi anajipa moyo kuwa akiiba atatumia hizo fedha alizoiba kuhonga na kumaliza kesi yake. Lakini tutakapofikia kuwa kama China katika kuwashughulikia mafisadi, wezi, watoa rushwa nk kutakuwa na woga fulani.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Tatizo si umasikini hasa.

  Mimi nionavyo, kwa mtu aliyetoka Chuo, akaajiriwa, na ndani ya mwaka 1au 2 kaiba, hiyo ni shida yake binafsi, zaidi tamaa.Vitu vizuri vimekuwa viingi, na bei zake ni za juu, hivyo ni lazima shortcut zitumike.

  Na makampuni uliyoyataja nadhani mishahara yao si haba sana ukilinganisha na sekta zingine kama kwenye viwanda vya akina Kanjibhai.

  Lakini shida ambayo siyo rasmi sana, ni mfumo uliojengeka katika jamii yetu kwa sasa ambapo wizi unaonekana kama njia ya fasta ya kujisongesha mbele! Inafikia mahali mwibaji kama huyo anaonekana kidume, na anatanua mtaa wa 2!

  Viongozi wetu ndo kabisaaa, wanaiba mchana kweupe na kusababisha watu wengine kukesha wakipanga mbinu za "kutoka"!
   
Loading...