DOKEZO Wizi kwenye malipo ya cash hospitali za serikali (imetokea Amana)

DOKEZO Wizi kwenye malipo ya cash hospitali za serikali (imetokea Amana)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna tabia mbaya inayofanywa na watumishi wa hospitali za umma.

Wakigundua mgonjwa (hasa wa kulazwa) anatumia cash na yupo kwenye hali mbaya, huwa wanawanunulisha ndugu madawa mengi ambayo mgonjwa hatoyatumia.

Kwa sababu ni ngumu kwa watu kujua, huwa wanalipia dawa nyingi na kuzikabidhi wodini, bila kujua kuwa wanakuwa wamewanunulia wale wahudumu. Je, wahudumu huwa wanazitumia wapi? Wanaziuza?

Hilo linawezekana sana kwa wagonjwa wanaotumia cash. Hawafanyi sana kwa wa bima kwa sababu bima ina wataalamu wa kukagua madeni ya kubambikiza.

Kama una mgonjwa wa kulazwa unatumia cash hospitali za umma kama Amana, jiandae kutumia hela zako kufadhili pharmacy za watumishi wa hospitali.
 
Hivi daktari si hukupa cheti tu na unakwenda kununua dawa mwenyewe na kumpa mgonjwa wako mwenyewe?. Isipokuwa mgonjwa wa operation tu ndio hukupa list na wao huchukuwa hivyo vitu na kuingia navyo chumba cha operation.
 
Back
Top Bottom