Wizi kupitia mitandao ya simu

Wizi kupitia mitandao ya simu

Tamaa zetu ndio sababu ya kuumizwa
Hapana mkuu sio tamaa sema ukiangalia unafanyaga miamala mingi so kwanini usipokee zawadi????

Neno zawadi au "bonus" halijawahi acha mtu salama.

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Washanipigiaga hawa jamaa nikawaambia kama ni bonus siwaitume kwenye line yang inamaana gani yakujua salio wakati nyie ndio mko uko kwenye system nkawaambia simchek salio wenyewe dah hawakurudi tena. Hivi vitu vipo wadau ni kweli kabisa....shukran kwa mtoa mada hope itawaelimisha wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tusambaze ujumbe mkuu ili watu wafahamu at least tutapunguza

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
-------___________________________------------
 
Mkuu mazoba mjini hawatakaa waishe kuna mpango wangu wa kando niliufungulia kibanda cha m-pesa juzi kapigwa za uso mpaka nimeshindwa kumuhurumia
HHahahaaaa....mchepuko alianzaje kukusimulia asee cpati picha jicho ulomwangalia

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Mkuu mazoba mjini hawatakaa waishe kuna mpango wangu wa kando niliufungulia kibanda cha m-pesa juzi kapigwa za uso mpaka nimeshindwa kumuhurumia
Alipigwa sh ngap

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Mpuuzi na mpumbavu ndio anaweza kuibiwa namna hiyo
Hahahahaa...ngoja yamkute ndugu ako ndo utajua kama mpumbavu au mpuuzi. Mjini ujanja ujanja

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Hao matapeli wanashirikiana na baadhi ya staff wa mitandao husika. Ndio maana wanaweza kuwa na details zako zote hasa transaction zako zote.
Kuna jamaa namjua ndio michezo yake hiyo. Na wanashirikiana na mtu m1 yuko customer care.
 
Hao matapeli wanashirikiana na baadhi ya staff wa mitandao husika. Ndio maana wanaweza kuwa na details zako zote hasa transaction zako zote.
Kuna jamaa namjua ndio michezo yake hiyo. Na wanashirikiana na mtu m1 yuko customer care.
Mtaje mwanangu, maana nnahasira nao kinoma

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Habari,
Tafadhari usivuke bila kusoma uzi huu ni muhimu hata kama sio kwako bali itasaidia watu wako wa karibu. Leo nimeona niweke wazi ni jinsi gani matapeli wanavyozidi kuwaliza ndugu zetu kupitia mitandao ya simu.

Takribani miezi 6 sasa wizi huu umeshamili na unakua siku hadi siku, nitoe angalizo tu uzi huu hauna nia ya kuelezea uzaifu wa mitandao ambayo wateja wake wanaongoza kuibiwa kwa kuwa mitandao yetu ina strong security ya kutosha katika kukabiliana na mianya ya wizi kupitia mitandao bali uzi huu ni kuweka wazi ili kama una ndugu yako usambaze ujumbe huu awe makini asije lia kilio cha maumivu na kisichokuwa na ukomo maana akishajua ameibiwa ataomba dunia ipasuke atumbukie ndani.

Wateja wanaoongoza kuibiwa ni wateja wa 075,076,074....nazani mnanielewa kwa hizo code.. ipo hivi matapeli hawa humpigia mteja simu na kujitambulisha wanatokea huduma kwa wateja wa mtandao husika na kumtaarifu ushindi wa zawadi au "bonus" neno linalotumika mara kwa mara na huenda mbali zaidi kwa kumuuliza maswali machache kuhusu salio lake muda huo na mteja akiuliza kwanini mnauliza salio langu wakati ninyi mpo mtandaoni mnaona salio nililonalo matepeli hujibu kwamba tunataka kuwa na uhakika kama wewe ni mmiliki wa simu hii tukumie "bonus" yako.

Baada ya mteja kutaja kiasi cha salio lake mfano Sh.895,000/= matapeli humtaka mteja atafute simu nyingine kisha atume ujumbe mfupi "sms" neno ZAWADI kwenda kwenye namba ya hao matapeli. mteja akishatuma sms hupigiwa kwenye hiyo simu aliyotuma sms na kuambiwa achukue simu yake na kufuata maelezo atayopewa hapa ndo utapeli unapoanzia.......

Mteja huambiwa apige menu ya pesa ya mtandao husika yaani *150*00# nazani mnajua code hii mnaielewa ni mtandao gani kisha kuambiwa achague kipengele cha tuma pesa mteja hushtuka kama anaibiwa kwa hayo maelezo lakini huambiwa kuna code zitatumwa kwahiyo akifika mbele akipata hizo code awasomee ili wamtumie bonus yake.

Mteja huamini na kufuata hatua ambayo itampa hizo code ili apokee bonus yake kisha Mteja huambiwa achague kutuma pesa kwenda mitandao mingine na hapa ndo ujanja na akili za matapeli hawa hutumika kuliza ndugu zetu.

Mteja ataambiwa aandike namba za bahati kwenye kipengele cha kuweka namba (ukiwa unatuma pesa) mfano wa namba zinazotumiwa mara kwa mara ni 654321456 usipokuwa makini huwezi jua hizo code ni namba ya simu ya mtandao flan.

Haijawekwa 0 tu hapo mwanzo lakini mtandao hutambua hiyo namba na kuruhusu muamala. Kwa kuwa mteja hajui ni namba ya simu huaminishwa kuwa kuna masage itakuja na code hivyo asonge mbele, baada ya kuweka namba hufuatia kipengele cha kuweka kiasi (nazani wote tunafahamu hatua hii) hapa matapeli humwambia mteja aweke code nyingine ambazo ni 00892111 ( juu nimeweka mfano wa kiasi kinachotapeliwa) mteja bado haamini kama anatepeliwa kwa kuwa kwa macho na fikla za kawaida tu huwezi jua kama hiyo ni 892,111/=Tsh.

Hatua inayofuata ni weka namba ya siri, mteja anauliza mboni namba ya siri? Hujibiwa kuna masage itakuja ututajie ili tukupe bonus yako na mteja huingiza namba ya siri na kuruhusu muamala....Dah masage inayofuata ndio humtoa mteja gizani

"imethibitishwa umetuma Tsh 892,111 kwenda namba 654321456 risiti namba 4HGY32Gl"

Kisha tapeli hukata simu na huwa hawaizimi kwa kuwa wanajua utakuwa ukipoteza muda kuwapigia na wao bila kupokea na huku alietumiwa pesa akiitoa bila wasiwasi wowote, mteja akiona jamaa hapokei simu huamua kupiga simu huduma kwa wateja wa mtandao wake na kwa kuwa ametuma pesa kwenda mtandao mwingine huduma kwa wateja hawana access ya kuzuia isitolewe na humshauri apige mtandao alikotuma. Akipiga kule huambiwa pesa imeshatolewa. Kilio kinachofuatia ni cha maumivu na kusaga meno.

My take :
Kuwa makini wezi hawa wanambinu nyingi sana na soon ntaweka hapa njia nyingine zinazotumiwa na hawa wezi wa mitandao kuliza ndugu zetu.

Ninawashukuru voda na airtel ambao ukipiga namba 100 huduma kwa wateja wanakupa taarifa za wizi huu kupitia maelezo ya awali, kwa kiasi flani wamefanikiwa kupunguza japo siyo kumaliza kabisa tatizo.

Wakuu.nawasilisha.
Asanteni
Mbona maelezo yooote hayo ni ya kuibiwa tuu inakuwaje mtu hashtuki? Daaa wajinga ndio waliwao!
 
Hao matapeli wanashirikiana na baadhi ya staff wa mitandao husika. Ndio maana wanaweza kuwa na details zako zote hasa transaction zako zote.
Kuna jamaa namjua ndio michezo yake hiyo. Na wanashirikiana na mtu m1 yuko customer care.


Ndio maana hawawapigii watu wasiokuwa na salio la pesa nyingi kwenye simu. Maana wana taarifa kwamba fulani ana hela. Lazma wanashirikiana na watu ndani ya mtandao wa simu husika.
 
Asante sanaaa mkuu na huu wizi hufanywa hasaa kwenye tigo pesa na m pesaa wanacheza sanaa ba akili za watu na details zote huwa zinatoka kwa hao jamaa wa IT kutoka mitandao nimetaja hapo juu....
Kwa wizi huu hakuna detail wanazopata kutoka kwa maservice provider bali ni ujanja wakubahatisha namba wanafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wahusika ndani kwani wanaweza block number yako na kutumia number yako kwa text message kumtumia ndugu au rafiki wakitaka hela asipokuwa mjanja anaetumiwa sms imekula kwake
 
Sehemu ya pili.

Habari wadau ...! juzi kati nilipost juu ya wizi unaoliza ndugu zetu kila kukicha kupitia mitandao ya simu.
Pitia hapa kwa sehemu ya kwanza

Wizi kupitia mitandao ya simu

Sehemu hii ntaonyesha ni jinsi gani wezi hutumia akili ama mteja huibiwa kijinga kwa kutokujua kupitia mawakala wausajiri (freelancer) fake au wasio waaminifu.

Ipo hivi upo nyumbani kwako umetulia sebureni ukipiga stor na wife au kucheki kideo mda si punde wanapita mawakala wa mtandao wowote(tigo,voda,aitel n.k n.k) wakijifanya wanasajiri laini,kusajiri huduma za nivushe,m-pawa, timiza au kukamilisha sajiri za laini ya mitandao husika, ukiwa mmoja wa wanaohitaji huduma kati ya hizo unawaita na kuwaeleza shida yako na wao watakuomba utoe laini yako uwape ili waweke kwenye simu yao kwa kuwa lazima watumie simu yao ya kazi ili kukuhudumia. Tuchukulie mfano. Mteja anahitaji kusajiliwa m-pawa ya vodacom, msajiri huchukua laini ya mteja na kuiweka kwenye simu yake ya usajiri na kujifanya anasajiri. Itafika kipindi atakupa simu uweke namba ya siri ili kukamilisha usajiri wako. Pasipo kujua kama wakala usajiri ameingia katika menu ya m-pesa na kufuata hatua zote za kutuma pesa na kinachosubiriwa ni namba ya siri ili kuruhusu muamala. Mteja ataingiza namba ya siri na kumrudishia wakala usajiri aendelee na zoezi kumbuka ukiweka neno siri namba hubakia zilivyo (hazifichiki). My friend kama una laki tano au milioni zote zitahamishwa na sms zote zitafutwa muda huo huo ili kuficha ushahidi, kumbuka huwa wanauliza salio la mpesa ili kukuhakikishia huduma ya m-pawa kukamilika. Wakala huenda mbali zaidi na kubadili namba ya siri ya mteja kisha kumwambia kuwa zoezi limekamilika baada ya saa 24 m-pawa itakuwa active ili mteja aendelee kutumia. Mwisho huomba malipo ya huduma na kutokomea. Mteja akija kushtuka ni pale anapo fanya muamala na majibu huambiwa namba ya siri sio sahihi Akipiga simu huduma kwa wateja atapewa taarifa ya fedha zake kuhamishwa na upande wa pili umeshatoa hizo pesa. Kinachofuatia ni kilio kwa uchungu sababu ya kutokujua au uzembe

My take: tuwakumbushe watumiaji wa mitandao hii kuwa makini kwa kuwa kila kukicha mbinu zina badilika na wizi unashamili kila iitwapo leo. Next time ntaweka sehemu ya tatu kuhusu mawakala wa tigopesa, airtel money au m-pesa wanavyolizwa na kupoteza mitaji yao .


Asante

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Shukrani mkuu.

Hayo masuala ya sijui niunge mpawa, mara 4G, sijui nini yataendelea kuishia masikioni tu.
 
Shukrani mkuu.

Hayo masuala ya sijui niunge mpawa, mara 4G, sijui nini yataendelea kuishia masikioni tu.
Pamoja sana chief.

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Huwa nipo makini sana akisema weka namba ya siri napiga OK hapohapo kwa kuwa ni SIRI haitakiwi aijue
 
Back
Top Bottom