Wizi kichaa (Kleptomania)

Mshana umenifumbua macho!Yule jamaa aliyeleta mada ya kuiba chupi za wanawake sikumuamini!Nilimuona kama mtu anayefurahisha genge.
 
Kumbee! Bank zile kalamu zao wanaweka kamba! Me nikajiuliza nani anaiba? Mtu ana deposit mil 15 then anaiba kalamu ya 200?
 
Wadau nasikia lipo tatizo kwa baadhi ya Watu Kuwa na Tabia ya Kuiba Vitu VidogoVidogo bila Kusukumwa na Mahitaji ya
Kiuchumi.Watu wa Aina Huwa Wanasukumwa Kutenda Matendo Hata Yasiyo ya Kawaida Bila ya Kuogopa Aibu Itakayowapa Kulingans na Hadhi iZao Katika Jamii. Kwa Mfano Unaweza Kuona Mtu Tajiri Anaiba/Anachukua Vitu Kama Viatu Vitatu Visivyofanana, Vijiko, Uma,Toothpick,Vitana Visu vya Mfukoni, Vitambaa vya Mezani,Vibiriti,Mikasi,Soksi, n.k. Vitu hivi Vyote Kiukweli Hana Matumizi Navyo Bali Huendelea Kuvikusanya! Inasemekama Hata Mhusika Huwa Hayupo Katika Bali ya Kawaida ya Kufanya Masmuzi Sahihi Wakati Huo.
Wakuu Sijui Kama Tatizo Hili Lipo Hapa Nchini Pengine Ni Vema Tukashare Uzoefu.
Karibuni
 
Hili mi pia hunishangaza, wapo pia watu huwaibia wadada siku zao, unamkuta mdada analalamika hazioni siku zake na ndani wanaishi wawili tu.
 
Unakuta mtu labda ameenda hotelini au mgahawani saa ya kula atachukua toothpick kadhaa, wengine hadi vijiko, glasi wanaondoka nazo... Hata sabuni pia wanachukua

[HASHTAG]#Kleptomania[/HASHTAG]
 
Hii ni moja ya personality disorder.
Zipo nyingi sana na nyingine za kushangaza .wakati mwingine tumezoea kuziona kwenye jamii na tunaona ni vitu vya kawaida.
Mfano kuna moja inaitwa hoarding disordey yan mtu anakuwa anatunza vitu hata kama hana matumizi navyo...kama nguo asizoziva,simu asizotumia,...unakuta nyumba imejaa vitu ambavyo hatumii lakini havitupi....

Nyingine ni pyromania - hii unakuta mtu anapenda kuwasha moto muda wote.
Akiwa na kibeliti lazima akimalize chote kwa kuwasha moto hovyo na kuchoma choma vitu
 
Back
Top Bottom