Wizi kichaa (Kleptomania)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,087
Kuna hiki kitu WIZI, wizi ni kujitwalia kwa njia ya kificho kisicho chako kwa njia ya kukimiliki kukitumia au kukiuza ili upate chochote au ufaidike.

Kuna aina nyingi za wizi lakini leo nimechagua wizi huu wa aina hii ambao nimeuita wizi kichaa au wizi majnuni, ni wizi usio na faida yeyote kwa mwizi mwenyewe, ni wizi wa vitu vidogovidogo mno, ni wizi unaofanywa na watu wenye kipato na kazi zao nzuri tu.

Member mmoja hapa jamvini alikuja na post ya kuomba msaada, yeye ni mwizi wa chupi za wanawake anaotembea nao, akishaziiba hana kazi nazo tena anazirundika tu uvunguni mwa kitanda chake.

Tunao wengi wa jinsi hiyo kwenye Jamii yetu na hata hapa jamvini tunao, wezi wa vijiko na uma na glass kwenye sherehe, wezi wa tishu stick na mapambo, wezi wa scent balls kwenye vyoo..

Ukiwaangalia wote ni watu wasio na dhiki yoyote!

Mtu anaingia bar anaagiza chakula cha gharama tu akimaliza kula analetewa toothpick na napkin/tissue .... Kichekesho anachukua stick kadhaa na tissue kadhaa tena kwa kificho unakuta kwenye gari kajaza toothpick na tissue nyingi tu, kalamu za ofisi, pini, kalamu za kuazima benki TRA au kwenye ofisi za umma wao wanabeba tu.

Huu ni ugonjwa, ni aina fulani ya uchizi au wendawazimu unahitaji tiba ya kitabibu...Ukimuona mtu wa hivyo msaidie usimcheke wala kumlaumu, ana tatizo.
 
Dr. Mwanjelwa wa CCM aliiba taulo hotelini akadakwa.

Huyu ukifanikiwa kufika kwake utamkuta na vitu vingi visivyo na faida kwake alivyoiba sehemu mbalimbali. Kuna jamaa alishawahi kuiba ule mkasi wa kufanyia operation pale Muhimbili, ukamdondoka wakati anatoka
 
Mi nilikuwa na glass zaidi ya 20 aina tofauti, nilikuwa na tabia nikitumia glass bar lazima niondoke nayo. Ila siku hizi nimeacha kabisa tabia hiyo
 
Mi nilikuwa na glass zaidi ya 20 aina tofauti, nilikuwa na tabia nikitumia glass bar lazima niondoke nayo. Ila siku hizi nimeacha kabisa tabia hiyo

Hahaha Jimena kuna rafiki yangu yeye naye alikuwa kama wewe ila baada ya kupata jiko akaachana na hiyo tabia
 
Last edited by a moderator:
Hahaha Jimena kuna rafiki yangu yeye naye alikuwa kama wewe ila baada ya kupata jiko akaachana na hiyo tabia

Mi ilikuwa mpaka aibu, na mpaka sasa sijui niliachaje labda mazingira yalinibadilisha au nimekuwa mkubwa sasa lol
 
Last edited by a moderator:
YES, huu ni ugonjwa wa kisaikolojia, unaitwa Kleptomania.

A Kleptomaniac is a person who is afflicted with Kleptomania, a compulsion to repeatedly steal "worthless" items, such as keychains and small fruit. It is classified in psychiatry as an impulse control disorder.

It is unclear whether it is due to depression, or people who are seeking more control of their life, but there are very few cases where diagnosed kleptomaniacs have stolen expensive items along the lines of jewelry and automobiles.
 
Kuna yule Rais aliyeiba pen. Alikuwa wa wapi yule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…