Wizi huu unarudi kwa kasi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi huu unarudi kwa kasi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kakuruvi, Mar 16, 2010.

 1. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kuna ule wimbo wa Msondo Ngoma ''ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo''
  nimezidi kuuelewa huo wimbo jana jioni wakati narejea nyumbani.
  Nilikuwa natokea IFM kupitia Shaaban Robert street, muda kama saa mbili hivi usiku, pale kwenye kona ya International House kuelekea Umoja House nilipishana na gari nyingine iliyokuwa inakuja kasi sana bila kujali yale matuta ya barabara. Nikahisi jambo ila sina uhakika.
  Baada ya kuendelea mbele nikakutana na jamaa anafukuza mbio huku anapiga kelele na kulia. Nilihisi huruma nikasimama ili nimuulize. Alinijibu kuna gari ilikuwa imepaki Ohio street wakati anavuka barabara kuja Garden Avenue hiyo gari ikakunja kuelekea aliko na ilimsogelea sana akadhani ni watu anaowafahamu labda watampa lift, haikuwa hivyo mmoja wa seat ya nyuma akachomoza na kukwapua bag lake likiwa na laptop tena mpya, kilichomfanya alie ni kwa vile laptop hiyo si yake na ina mafaili muhimu sana ya watu, masikini!
  Kwa kuwa ile gari hatukuona muelekeo wake hapakuwa na jinsi ila nilimpeleka kituo cha Police pale Gym Khana, baada ya maelezo Polisi altujulisha kuwa sio tukio la kwanza la namna hiyo mitaa ile, hivyo nawajulisha kuwa maeneo yale Samora, Ohio, Garden mpaka Posta si mazuri sana hasa usiku unapokuwa na bag linaloonesha umebeba laptop, tahadhari kwa Wanafunzi IFM, Wafanyakazi wa ofisi za maeneo hayo wawe japo hata wawili inaweza kusaidia wasiporwe.
  Wajulisheni wengine tafadhali.
   
 2. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,050
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  POLE ZAKE. Hiyo post hapa chini niliandika katika thread nyingine jana naona na hapa inafaa. Ni katika kutahadhalishana na kuhabarishana.

  ==========================================

  Pole sana muzachai,

  Mimi najua uchungu ulioupata na naamini ni kweli kuwa walijaribu kukupora. Hii ni aina mpya ya wizi hapa mjini. Mimi ilinikuta mwezi August ama Julai mwaka jana siku ya jumapili saa kumi na moja na robo alfajiri. Nikiwa namsindikiza binamu yangu aliyekuwa anapanda basi kuelekea kanda ya ziwa pale “Millenium Park” katika ofisi za Mohamed Trans nilipaki gari aina ya Escudo, nikashuka kumsaidia mgeni wangu kubeba mizigo yake, hadi kwenye basi ndani.

  Ilinichukua kama dakika tatu nikarudi kuchukua begi lingine lililobaki hapo ndipo nikaona mtu anatoka katika gari langu na kuanza kutimua mbio akiwa na begi, moja kwa moja nikajua ni mwizi, nikamkimbiza hadi kwenye gari lao kama hatua kumi hivi toka nilipopaki langu, ambapo aliwahi kuingia na kuanza kuondoka, Nami nikaingia kwenye gari langu nikaanza kuwafukuza, walisimama kupisha magari yaliyokuwa yanatokea Magomeni hivyo nikawa karibu nao kabisa. Gari hilo lilikuwa aina ya Escudo green Metallic likiwa namba zimefunikwa na karatasi ya njano ambayo bahati nzuri ilichanika nikaona baadhi ya namba hizo ambazo ni T4__ AFW.

  Basi haraka nikaanza kufukuzana nao, tulipofika Manzese, kabla ya daraja niliona kuna gari la Doria la Polisi ( Saloon zenye taa juu) likiwa upande wa pili nikaamua kuanza kupiga simu wakati naendelea kuwafukuza. Bahati mbaya simu ilikuwa haipatikani, nikaendelea kufukuzana na wezi hao, waliingia magomeni kuelekea kwa shehe Yahya, nikala sambamba nao, wakafuata barabara ya Kawawa kuelekea Kigogo.

  Walipofika Round about ya Kigogo wakaelekea njia ya kwenda Mburahati, Hapo ndipo nikakumbuka kuwa mimi nina tiketi ya Yule mgeni, pia kwenye gari sina hata manati, wakati huo ilikuwa kama saa kumi na moja na nusu alfajiri, na wao wako zaidi ya mmoja na watakuwa wapo tayari kwa lolote, hivyo nikaamua kurudia hapo


  Nikaenda kwenye basi nikamweleza, nikampa tiketi akaendelea na safari. Niliripoti kituoni pale Urafiki na kuwaomba wachukue alama za vidole za gari langu kwani walichukua power window na begi pamoja na vitu vingine. Niliambiwa kuwa huduma hiyo haipatikani kila mahali inapatikana Central hata hivyo ni ngumu pia kuwakamata, kwa njia hiyo.

  Niliwaeleza juu ya gari la doria la polisi ambalo kama wangekuwa na simu ya dharura inayofanya kazi wangenisaidia wakadai kuwa simu hiyo inafanya kazi kwa mtandao wa ZAIN tu!!!!. Mimi nilikuwa na simu (mchina) yenye laini mbili Tigo na Zantel.


  Lakini niliomba wachukue maelezo yangu kwani yawezekana nitakuja kukutana na wezi hao walikubali na kuandika maelezo hayo, walinieleza kuwa wataipangia mpelelezi na kunitaarifu. Baada ya wiki kama tatu hivi niliona gari hilo hilo pale Tabata, nilikumbuka kwani Yule mwizi niliyefukuzana naye wakati anatoka kwenye gari langu alikuwepo pia akiwa amevaa vile vile kama siku aliyovunja gari langu na kuiba.

  Alivaa fulana ya mistari ya pundamilia ya kulala rangi ya njano na mistari mingine blue/nyeusi, viatu vya safari boot, na Geans, pia gari hiyo ilikuwa imegongwa kwa pembeni kwenye bapa haya yote niliyaeleza kituoni yakaandikwa, Roho ilitaka kuniruka nikahamaki na kuendelea kufuatilia ambapo walipaki gari hiyo ktk gereji fulani, hizi gereji za nje na kumkabidhi kijana Fulani funguo nao wakaondoka wakiwa wawili, namba za gari hilo zilionekana vizuri T 430 AFW. Nilimuuliza kijana ni akina nani hao jamaa akadai ni washikaji wa fundi mwenzie yeye hawafahamu majina. Akanitaarifu kuwa gari litakuwa hapo kwa matengenezo.


  Nikaenda urafiki kuelezea kuwa nimewapata wezi wangu lakini majibu niliyopata pale ni kuwa uwezekano wa kuwatia hatiani wezi hao ni mdogo sana na kwa kifupi hakuna kwani watakuwa tayari wameishaficha vitu walivyoiba na hakuna ushahidi wa kutosha. “Tunaweza jaribu lakini uwezekano wa kumtia hatiani ni mdogo sana ama hakuna”


  Hivyo hao wanaoeleza kuwa siyo kweli ama ni chuki binafsi wajue mambo haya yapo sana wsubiri yawakute.

  Nimeamua kutoa ushuhuda huu ili watu wajue kuwa haya mambo yapo sana hapa Dar Es Salaam na wachukue taadhari mapema.
   
 3. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pole sana Nyati,
  Masikini hata vyombo vyetu vya usalama vina matatizo makubwa kukabiliana na changamoto za uhalifu. Je, tutafika?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Anarchy..

  Lakini kwa sababu moja au nyingine sisi kama wanajamii tunachangia ktk huu uwizi, achilia mbali mfumo mzima wa kujiendesha ulivo wa hovo. Sisi tunachangia sana uwizi kwa kuwa-encourage waizi kwa kupenda kununua vitu mkononi, bila risiti na kutojali bidhaa husika imepatikanika wapi. Mindhali kama tungekua wote sio watu wa tamaa, tungesababisha hivi vitu vya wizi kukosa soko, na hatimaye uizi ungeisha taratibu.
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Vile kuna haya magari ya makampuni ya simu...........ZANTEL, VODA, ZAIN, TIGO........... Hawa nao wajiangalie sana............ maana kinachoaminika na wezi hao ni kuwa kila gali la kampuni hizo lazima lina laptop............... katika hali halisi si yote......... Hivyo kwa mtazamo huo.... hata kama huyo mwizi hataikuta hiyo laptop.........KILICHOMO KITAKUWA HALALI YAKE.
   
 6. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Abdulhalim ndugu yangu,
  Kuna watu wanatamani gari ipige chini wapore au nyumba iungue wapore. Ni kweli tusiponunua vitu vya mazabe wizi utapungua japo kidogo.
   
 7. D

  Donrich Senior Member

  #7
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Asante kwa kutupa taadhari na pia poleni kwa hasara.
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kwa mtaji huu wa wana usalama wetu kutotoa msaada kwa wahanga wa wezi, kupigana viberiti hakutaisha kabisaaa. Lakini mbona ishu za mafisadi wanazibebea mabango? kuanzia kukamatwa kwao, upelelezi na kufikishwa mahakamani e.g. issue ya vijisent na bajaj, mpaka mkuu wa upelelezi kanda ya kinondoni alikwenda eneo la tukio? mahakamani ndani ya siku 14, bidae mhh kesi kama kawa kila baada ya miezi 2, si upelelezi umeisha why kesi haiishi?
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mnafikiri ni kwa nini watu wanaamua kuwachoma vibaka moto, ni mambo kama hayo mtu ananibiwa na mwizi anaonekana, lakini tatizo linakuja police, mtu anapelekwa saa2 asubuhi saa nne asubuhi unakutana nae tena mtaani anaiba
  Dungu yangu nyati we ni mstaharabu sana, lakini kwa wengine hao jamaa wangechomwa humohumo kwenye gari lao
   
Loading...