Wizara zinazofutwa hadharani

Wizara zinazofutwa hadharani

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,681
Reaction score
59,181
Nyingine ni Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Nchi.


Rais Dk. John Magufuli.
Wakati kukiwa na taarifa kwamba Rais Dk. John Magufuli, anatarajia kupunguza karibu nusu ya wizara zilizokuwapo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, imefahamika kuwa wizara zinazolengwa ni zile zilizopo Ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Chanzo kimoja kutoka serikalini kimeiambia Nipashe jana kuwa wizara hizo zitaunganishwa kwenye wizara mpya zitakazoanzishwa na Rais ambaye ameweka mkakati wa kuwa na baraza dogo la mawaziri.

Wizara zinazotajwa kufyekwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Wizara Ofisi ya Waziri Mkuu na Sera, Uratibu na Bunge.

Nyingine ni Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Wizara ya Nchi, Ofisi Makamu wa Rais Mazingira na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Kadhalika, katika mabadiliko hayo, wizara nyingine zitaguswa ili kufikia malengo ya kubakia na wizara chache kutimiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.

Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Dk. Magufuli atalitangaza Baraza la Mawaziri ndani ya wiki hii ingawa bado kumekuwa na usiri wa siku halisi atakayotangaza.

Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, mwaka huu ikiwa na wizara 30. Vile vile, alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na naibu wao zaidi ya 60.

Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5, mwaka huu, tayari ameshamteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa serikali yake na Ijumaa iliyopita alizindua rasmi Bunge la 11.

Juzi, chanzo kimoja kililiambia Nipashe kuwa tayari Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato wa kuunda baraza lake la mawaziri na kwamba kinachosubiriwa sasa ni kulitangaza wakati wowote kuanzia sasa.


Chanzo: Nipashe
 
Baraza dogo la watu wenye elimu, utashi na weledi litamsaidia president kuleta maendeleo ya haraka yaliyokwamishwa kwa kuteuliwa watu wasio na ubunifu katika utendaji. Ubarikiwe Rais JPM
 
Punguzaaa baba fukuzaaa watu walio kuwaa wanakulaa nchi bilaa mafanikioo
 
Actually hapo watakaopungua ni Mawaziri na Manaibu waziri. Hao watumishi wengine watabaki hapo kama sekta fulani au watapangiwa kazi nyingine, na salary kama kawaida
 
Kupunguza wizara 15 siyo mchezo. Wanaouliza pesa za elimu zitatoka wapi hawakuyajuwa haya. Nadhani tutaheshimiana tuu. Eti kuna watumishi walikuwa hawauhesabu mshahara wanakula posho tuu. Maguuuuuu! Bado Tanesco.
 
Actually hapo watakaopungua ni Mawaziri na Manaibu waziri. Hao watumishi wengine watabaki hapo kama sekta fulani au watapangiwa kazi nyingine, na salary kama kawaida
Mkuu salary haziitii serikali hasara, na wala salary siyo matumizi yasiyo ya lazima. Kinachoondolewa ni yale matumizi yasiyo ya lazima ndo maana unasikia ameokoa kiasi cha pesa na kukipangia shughuli za kutoa huduma kwa wananchi wenye uhitaji. Kupunguza mawaziri 15 na manaibu wao ni pesa nyingi sana zingetumika kuwahudumia hawa ukichanganya na dili zao ni balaa.
 
Actually hapo watakaopungua ni Mawaziri na Manaibu waziri. Hao watumishi wengine watabaki hapo kama sekta fulani au watapangiwa kazi nyingine, na salary kama kawaida

Sasa kama zinakatwa hata 10 unahisi ni pesa ndogo hiyo? watu 20, mishahara yao na magari yao jumla ni pesa kiasi gani na usisahau na ma PS wao pia.
 
Hongera Rais Magufuli kwa kutekeleza maoni ya wananchi yaliyoko kwenye Rasimu ya Warioba, serikali ndogo chapa kazi.
 
Sasa kama zinakatwa hata 10 unahisi ni pesa ndogo hiyo? watu 20, mishahara yao na magari yao jumla ni pesa kiasi gani na usisahau na ma PS wao pia.
Hao ma PS wako pale pale, hata zikipungua hawataachishwa kazi hivi hivi
 
nami najuta kwa nini kura yangu niliipeleka kuleeee kwa hasira ya kuchoka umangimeza wa chama kubwa

kila kura imesaidia iwe ilienda upinzani au ilienda tawala,
we unadhani bila hofu ya upinzani magufuli angepeperusha bendera ya chama kubwa?
 
Wizara ya michezo ibaki peke yake asichanganye na vitu vingine maana kilichofanya michezo kushuka kwa kasi ni kutokana na wizara kubeba majukumu kibao yakiwemo ya utamaduni na habari.
 
Hongera Rais Magufuli kwa kutekeleza maoni ya wananchi yaliyoko kwenye Rasimu ya Warioba, serikali ndogo chapa kazi.

Wizara ya Michezo iwe peke yake iwe kama wizara ya fedha, wizara ya maji yaani michezo iwe na wizara ya pekee isichanganywe na vitu vingine kabsa. Hii itasaidia michezo kukua kwa kasi kubwa.
 
Uzuri mawizara hayana issue wala hayana sheria ya kuyaanzisha kama zilivyo idara, mamlaka, mikoa, wilaya na wakala za serikali. It's just by the President's pleasure that ministries are established and, in the same means, can be dissolved without any query or issue.
 
Sasa kama zinakatwa hata 10 unahisi ni pesa ndogo hiyo? watu 20, mishahara yao na magari yao jumla ni pesa kiasi gani na usisahau na ma PS wao pia.

Safari hii mawaziri watatumia Vitz hakuna kutumia magari ya bei kubwa.
 
Dr hamis kingwa asikose kwenye baraza lako plz...
 
Back
Top Bottom