Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaomba TSh 476.6 bilioni Bungeni, kamati yalilia fedha za maendeleo

Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaomba TSh 476.6 bilioni Bungeni, kamati yalilia fedha za maendeleo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Ashatu Kijaji amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025 / 2026 jijini Dodoma leo Mei 23, 2025. Dk Ashatu ameliomba Bunge lipitishe bajeti ya Sh476.6 bilioni yenye vipaumbele vinne ambapo kati ya fedha hiyo TSh 375.1 bilioni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeshauri fedha zinazotengwa katika bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo za wizara hiyo zitolewe kwa wakati kama zilivyopangwa ili waweze kufikia malengo waliojiwekea.

==

"Kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), vijana 106 wamewezeshwa kujiajiri kwa kupatiwa ekari 1,761 katika Ranchi ya Kagoma pamoja na mkopo usio na riba wa shilingi milioni 934 kupitia TADB. Tayari wameanza unenepeshaji wa ng’ombe, ambapo hadi Aprili 2025, wameuza ng’ombe 452 na kupata faida ya zaidi ya shilingi milioni 76. Hii ni hatua kubwa ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia sekta ya mifugo."

"Kupitia Programu ya BBT, vijana wetu sasa wanajiajiri kwa uwekezaji wa kisasa kwenye ufugaji. Tumewapatia ekari 1,761 katika Ranchi ya Kagoma na mkopo usio na riba wa zaidi ya shilingi milioni 934 kupitia TADB kwa ajili ya unenepeshaji wa ng’ombe. Tayari tumeshuhudia mafanikio makubwa – ng’ombe 627 wamenenepeshwa, 452 wameuzwa na vijana wamepata faida ya zaidi ya shilingi milioni 76. Hii ndiyo Tanzania tunayoijenga, inayowawezesha vijana wake kwa vitendo."

Mavuno ya Samaki yameongezeka kwa 55.3% baada ya kupumzisha Ziwa Tanganyika

“Katika kipindi cha miezi minne baada ya kufungua Ziwa Tanganyika, mavuno ya samaki yameongezeka hadi tani 38,999.82 zenye thamani ya shilingi bilioni 324.8, kutoka tani 25,113.43 za mwaka 2023 kabla ya upumzishaji. Hili ni ongezeko kubwa la uzalishaji na thamani."

Ameongeza kuwa: "Kutokana na ongezeko hili, mazao ya uvuvi yaliyouzwa nje kutoka Ziwa Tanganyika mwaka 2024 yalifikia tani 1,227.21 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 180, sawa na ongezeko la asilimia 84.79 ikilinganishwa na mwaka 2023."

Mauzo ya Nyama nje ya Nchi yameingiza Shilingi Trilioni 3.7

"Kupitia Bodi ya Nyama Tanzania, tumefanikisha kuuza tani 9,863.41 za nyama zenye thamani ya Shilingi Trilioni 3.7 hadi kufikia Aprili 2025, sawa na asilimia 89.9 ya lengo letu. Hii ni ongezeko la asilimia 5.75 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mafanikio haya yanatokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambazo zimeongeza masoko yetu hadi kufikia nchi 11."

"Kutokana na kuimarika kwa biashara ya mazao ya mifugo nchini kwa mwaka 2024/2025, tumeona ongezeko la ulaji wa mazao hayo kwa wananchi wetu. Kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja kimeongezeka kutoka lita 67.5 hadi 68.1, ulaji wa nyama kutoka kilo 16 hadi kilo 17.6, na mayai kutoka 107 hadi 119 kwa mwaka."

"Hata hivyo, pamoja na mafanikio haya, bado hatujafikia viwango vinavyopendekezwa na FAO, ambavyo ni lita 200 za maziwa, kilo 50 za nyama na mayai 300 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Tunaendelea na juhudi zetu kuhakikisha tunafikia viwango hivi."

Vipaumbele vya Bajeti yetu Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka 2025 / 2026

1. Kuongeza uzalishaji, masoko, na thamani ya mazao ya mifugo na uvuvi
2. Kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za mifugo na uvuvi
3. Kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Mifugo na Uvuvi
4. Kuimarisha utafiti, mafunzo na huduma kwa Sekta za Mifugo, na Uvuvi

"Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo, ambapo katika Mwaka 2024/2025, imetenga hekta 23,589.7 za malisho, na kufanya jumla ya ardhi iliyotengwa kufikia hekta 3,489,701.13 ikilinganishwa na hekta 3,466,111.43 mwaka 2023/2024."

"Hali ya upatikanaji wa malisho katika ardhi ya malisho nchini imeongezeka kutoka tani 110,659,032.16 mwaka 2023/2024."
 

Attachments

Ni kikao cha fisiem TU.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Hivi bado kuna watu wanaangaliaga bunge? Hongereni sana kwa moyo huo.
 
Back
Top Bottom