Wizara ya Mambo ya Nje yabadili kauli na kusema Rais wa Iran Ebrahim Raisi atawasili nchini kesho

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Maswali yameibuka kuhusu utendakazi wa maafisa wa Wizara ya mambo nje inayoongozwa na Waziri Dkt. Alfred Mutua, baada ya kutuma taarifa nyingine mpya kwa vyombo vya habari ikisema kuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi atawasili nchini kesho kwa ziara rasmi.

Awali msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed alithibitisha kuahirishwa kwa ziara hio lakini hakueleza ni kwa nini.

Aidha taarifa mpya sasa iliyotumwa inasema ziara ya Ebrahim Raisi nchini Kenya itakuwa ni rasmi, tofauti na taarifa ya wiki Jana kwamba itakuwa ni ziara ya kikazi.

Kadhalika Wizara ya Mambo ya nje imeeleza kuwa mkanganyiko ulitokana na kuchelewa kidogo kwa maandaliazi ya Hati ya Makubaliano(MoU).

20230711_132524.jpg
 
Back
Top Bottom