Wizara ya Mambo ya Ndani inahitaji mtu kama Mrema. Deo Filikunjombe ndio jibu...

Majeshi yaliyo wizara ya mambo ya ndani matatizo yao mengi yanafanana. Ni vizuri kumpata mtu anayeyatambua matatizo sugu na utendaji wa majeshi hayo.
 
Tunahitaji ex police juwa waziri sio ex jambazi
Kwani MOHA ni ya polisi tu hadi tuhitaji ex police? Kuwa ex police peke yake haitoshi, inawezekana alikuwa ni 'polisi mzigo'. MOHA inahitaji mtu aliyebobea katika masuala ya security na intelligence kwa ujumla. Hii ni kwamba ana-record iliyosimama katika hayo, sio tu kuwa ex-nanihii, haitoshi.
 


Wewe Ccm huijui! Watu sampuli hii huwa hawatakiwi CCM kabisa. Magufuli na yote aliyoyafanya miaka ya mkapa alishapelekwa wizara ya kitoweo ili acha kuongea. Matokeo yake sasa hivi amekaa anamsifia raisi tu asubuh mchana na jion. Whole of CCM is pure ----.
 

Chris Lukosi
Katika post kadhaa huwa unaonekana kuegemea kwenye ushabiki na pengine mipasho, katika mada hii umeonyesha sura halisi uliyo nayo, nakuunga mkono kwa hoja ulizoleta. CCM inao vijana wengi wachapakazi, werevu na wenye kujituma na pengine kuunganisha vizuri utaifa lakini mazoea ya kuangalia majina na nani anatoka familia gani ndo yametufikisha hapa tulipo.

Binafsi nakubaliana nawe kwa asilimia 100 Deogratias Filikunjombe vema Kikwete akampa wizara ambayo inahitaji mtu makini kama hiyo ya Mambo ya Ndani na kwa vile alishakuwa mtumishi katika wizara hiyo pasi na shaka anajua vema yanayoendelea na wapi kwa kufanyia kazi.

Mbunge Filikunjombe
Nimebahatika kuonana naye mara moja katika pitapita zangu, ni mtu wa kawaida sana asiyependa kujikweza, si mpenda makuu, mtulivu, mpenda kuongea maendeleo na kuonyesha mapungufu asiyoyavumilia bila woga na mpenda ushirikiano. Anajali hoja na ukweli badala ya kile moyo unapenda. Ni mchapakazi kwelikweli na anayejituma.

Anaonekana ni mtu mara nyingi anayezama katika wimbi la kufikiria mambo mengi awapo popote, naana utaona ghafla kama amekaa kimya na kuzama kwenye fikra, mtu wa aina hiyo ni chanda cha dhahabu kwenye kisahani, dalili ya kuwa mtu wa watu anayewafikiria watu wake, sawa na baba anayehangaika usiku na mchana na kufikiria watoto wake wavae nini, wale nini, wasome nini na wapi, nk.

Nimewahi kumsikia mimi mwenyewe akisema wapinzani licha ya uchache wao wana hoja nyingi nzuri tunatakiwa tuwape nafasi yawasikiliza na mazuri tuyafanyie kazi, nadra sana kupata mbunge wa CCM au kiongozi wa serikali kutamka kitu kama hicho.
 

Nimecheka sana, huyu huyu deo apewe uwaziri ndani ya CCM... Wanaopewa uwaziri ndani ya CCM ni yale matoyoyo wale watakayo kuwa tayari kuifia CCM siyo tanzania.. Pole sana Deo Kwani Ndani ya CCM sahau uwaziri hata ubunge mwaka 2015 utausikia tu na kama watathubutu kukupa uwaziri au unaibu watakuweka sehemu ya kukumaliza au ya kukutega....
 

Ni kweli Candid Scope,

Pia tatizo ni la kimfumo inabidi awe tayari kupambana na mfumo.Inahitaji courage ya hali ya juu hasa unapokua chini ya waziri Mkuu anayejua kupiga stop walioko chini yake na Rais ambaye anapenda umaarufu binafsi kuliko umaarufu wa kimfumo

Yupo tayari kuwa popular at the expense of our motherland.
 
Last edited by a moderator:
Wizara ya mambo ya ndani imekuwa chaka la wahuni na kugeuzwa kundi wa wahuni badala ya walinzi wa raia. Inatisha, si sura ya mtu kufaa kuwa waziri bali uwezo na kuangalia utendaji wa mtu. Hadi sasa kashfa yamabomu inazidi kulindwa, bora aondoke huyu Nchimbi huenda kivuli chake ndio kinachowakinga waovu.

Waliochafuka kwa damu kama akina Kamuhanda wanapandishwa vyeo kwa sababu ya mauaji, sijapata kuona uchafu aina hii tangu nchi hii tupate uhuru.

Namfahamu baba ya Nchimbi ambaye alikuwa anaitwa John Nchimbi ambaye alikuwa Mbunge wa Songea, aliwahi kufanya maovu kama huyu mtoto wake, akamtia jela padre aliyekuwa anawasaidia vijana kujitegemea, alipotaka kuingiza pua na padre kumshupalia aisonoe mali za vijana wavuja jasho akatuma askari na kumtia jela padre, hatimaye haki ikatendeka viogozi wa mkoa wamtoa bila masharti kwamba huyu anasaidia vijana kupata ajira na ufundi sisi tunaingiza ubinafsi.

Hivyo basi mtoto wa simba ni simba tu.
 
Kwa style hii c bora wampe hata kangi lugola x-cop wa idara nyeti wa enzi za mkapa na pia haogopi mtu
 


Pamoja na ukweli huo, kumbuka CCM inamapokeo ya kunyamazishwa wenye kuwanyooshea vidole nafasi za uwaziri ili waingie kwenye mfumo wa kuwajibika kwa pamoja. Nadhani hili pia lilitumika kipindi kile alipoingizwa Mrema katika baraza la Mawaziri. Kuna wachapa kazi kama Mwakiembe angekuwa mtu laini kama siagi sidhani angethubuti kufanya afanyayo baada ya kufanyika kila jitihada za kumwadabisha hata kwa njia za kijasusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…